Waraka wa wazi kwa mh. Raisi dr. Jakaya mrisho kikwete - kutoka udom

Apr 4, 2012
6
3
Siku za karibuni, UDOM kumeanza kutokea tena ukiukwaji wa sheria. Na kuna wimbi la kufukuza wafanyakazi kinyume na sheria. Kilichonisikitisha ni kitendo cha wafanyakazi kukata rufaa. na kushinda rufaa hizo, ila Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ukatumia ubabe ukakataa. hii ni baada ya kuona aibu. pamoja na kwamba tupo masomoni lakini tumeendelea kupata taarifa.

ila kilichonisikitisha zaidi, Mwenyekiti wetu alitoka kwenye kikao, akawataarifu juu ya kilichojiri kikaoni. na wakaandika barua kuonyesha kutoridhishwa. aliishia kupewa ONYO KALI, asirudie tena , na wakati wowote watamfukuza kazi. Sasa tumeamua kumjulisha Mheshimiwa na umma wa watanzania. Serikali isipochukua hatua Mwezi wa 5 wote tutarudi, tutaanza kupigania haki zetu. Kama suluhu ni migomo, ndiyo Serikali ifungue masikio Tutafanya hilo. nia na uwezo tunao.

Pitia attachement uone uozo mwingine UDOM, cjui pana laana. basi mi sisiemi tena:tape:
 
Attachments

  • UDOMASA Letter to President.pdf
    418.7 KB · Views: 339
  • LETTER TO CHAIRMAN OF UDOM COUNCIL.pdf
    211.6 KB · Views: 327
Siku za karibuni, UDOM kumeanza kutokea tena ukiukwaji wa sheria. Na kuna wimbi la kufukuza wafanyakazi kinyume na sheria. Kilichonisikitisha ni kitendo cha wafanyakazi kukata rufaa. na kushinda rufaa hizo, ila Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ukatumia ubabe ukakataa. hii ni baada ya kuona aibu. pamoja na kwamba tupo masomoni lakini tumeendelea kupata taarifa.

ila kilichonisikitisha zaidi, Mwenyekiti wetu alitoka kwenye kikao, akawataarifu juu ya kilichojiri kikaoni. na wakaandika barua kuonyesha kutoridhishwa. aliishia kupewa ONYO KALI, asirudie tena , na wakati wowote watamfukuza kazi. Sasa tumeamua kumjulisha Mheshimiwa na umma wa watanzania. Serikali isipochukua hatua Mwezi wa 5 wote tutarudi, tutaanza kupigania haki zetu. Kama suluhu ni migomo, ndiyo Serikali ifungue masikio Tutafanya hilo. nia na uwezo tunao.

Pitia attachement uone uozo mwingine UDOM, cjui pana laana. basi mi sisiemi tena:tape:

UDOM ni chuo cha CCM, hivyo maamuzi yao yapo ki CCM zaidi
 
Chuo cha Kishkaji sna hichi,kama hamtendewi haki gomeni maana ndo waliskialo.kwani Mlacha na Kikula bado wafalme?naskia pia udini unatenda kaz sna humo,ni kweli?
 
Nina mashaka kama jamaa atasikiliza kilio chenu. Ccm kero za wananchi ndio mtaji wao wa kisiasa ili come 2015 waje kuombea kura kwa ahadi''mkiwachagua watabadilisha uongozi wa chuo'' We fikiria pamoja na mihela yote mliyomchangia mkulu kuchukua form za urais lakini anawatelekeza?? Magamba ni sikio la kufa kamwe halisikii dawa
 
Sio wafanyakazi tu wanaofukuzwa.,even wanafunzi wanapewa suspension ovyo ovyo, matokeo colege ya education hawayatoi eti vikao vya kutoa matokeo vinaendelea. Jamani huu mchuo unakera mie!
 
Hawa wazee wamekuwa kama msalaba, hawa vijana wanaowasumbua leo. Ndio viongozi wa taifa hili, nadhani wanashindwa kusoma alama za nyakati. wamejaribu kutumia mwamvuli wa udini, inashindikana, wakaingiza siasa inashindikana. Cjui vizuri Mh. alitumia vigezo gani kumleta Mwapachu kuwa Mwenyekiti wa Chuo. Tuliwahi kusema hapa kwa umri hana jipya:yell:

Ni kweli amekuwa mstari wa mbele kuvunja sheria, ili kutimiza matakwa ya Mlacha, amepoteza mwelekeo kabisa. na hili linajidhihirisha viongozi wetu wamemwandikia barua iliyoambatanishwa akashindwa kujibu wakati hoja alianzisha yeye. akakimbilia kuita kikao na kumpa onyo Mwenyekiti. Hapa najiuliza upo wapi utawala wa sheria??:shock:

Wanaopata nafasi ya kuongea na Mh. Raisi, wamshauri sasa afanye mabadiliko, viongozi wote ukizungumza nao wamechoka na UDOM. Taarifa zinasema Mh. amekuwa akiwakingia kifua. swali ni kwa masilahi ya nani?? Na hili limepeleka CCM kupoteza mvuto kabisa vyuoni. na ikumbukwe huku ndipo viongozi wanaandaliwa.

Au la wanasubiri itokee vurugu kubwa igharimu maisha ya watu,labda watatuelewa. na nimesikitika sana jana nimeambiwa kumbe Kikula alistaafu tangu mwaka jana. ila Utumishi wakamuongezea mkataba. Hivi hawa wazee wasipoachia haya madaraka vijana watapata wapi kazi? na tayari hawa wazee walikuwa na skendo ya kusababisha migomo, ilikuwaje akaongezewa mkataba? Hebu wabunge mtuulizie huko bungeni kwenye maswali ya papo kwa papo:nod:
 
Siamini macho yangu. Si nyinyi mlioandamana kumuunga mkono Vasco da Gama! Sasa mnalialia nini. Go eat the apple you picked.
 
Mpayukaji please look at who yourtalking too- hao ni walimu na sio wanafunzi ulisikia wapi walimu wakiimuunga mkono mgombea wowote Wa siasa- I think ur name suits u well
 
KWELI. JK anajua kwanini hawezi kuwatimua Mlacha na Kikula
Uko sahihi MwafrikaHalisi JK anajua wazi kwa nini hataki kufanya mabadiliko hapo Chuoni. Nasikia hata mmoja wa viongozi wa hicho chuo kwa jina la Prof.Mlacha huwa anawakejeli wafanyakazi wenzake kuwa "YEYE NI KUKU ALIYEATAMIA, KAMWE HAWEZI KUCHINJWA". Kama ndivyo swali la kujiuliza ni je "nini ni hicho alichoatamia ambacho akiondolewa kitaharibika?" na anakiatamia kwa maslahi ya nani? Ama kweli nchi hii ina wenyewe ambao serikali iko radhi hata kama watanzania wote wanakufa kutokana na matendo ya hao wachache itaziba masikio. Lakini, kila lenye mwanzo lina mwisho; SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA...DALILI HIZI NI ISHARA YA KIFO SERIKALI HII ISIYOTAYARI KUSIKIA DAWA
 
Sio wafanyakazi tu wanaofukuzwa.,even wanafunzi wanapewa suspension ovyo ovyo, matokeo colege ya education hawayatoi eti vikao vya kutoa matokeo vinaendelea. Jamani huu mchuo unakera mie!
Haya ndo matunda yakuongozwa na VC, principals and deans ambao ni wa staafu ama si muda mrefu wanastaafu. Sasa hivi education walimu wanapokuwa wanafundisha walinzi yaani suma jkt wanapitapita madarasani wakati lecture zinaendelea unajiuliza SUMA JKT wana wana-assess walimu? lakini pia walimu wanazuiwa na walinzi kwakufukuzwa kufundisha wakati wa weekend. Sasa huyu principal wao anawatakia nini walimu na wanafunzi hawa wa college of education
 
Sasa mbona hiyo ya chairman wa UDOM imeandikwa kwa Kiingereza na hii ya Muheshimiwa imeandikwa kwa Kiswahili......................!?
 
Lugha ya kiingeza ndo onatumika chuobi hapo pamoja na kuongozea vikao- lakini ya raisi ni waraka Wa wazi na ili kuwafikia watanzania wengi Kiswahili ndio Lugha sahihi ili kufikia jukumu Hilo
 
Udom ilikuwa na matatizo toka kuanza kwake. Wadau walionza na chuo hiki kilichokuwa na jengo moja bila hosteli. Matatizo hayo yanaendelea kutokana na kutaka kudahili wanafunzi wengi pasipo uwezo wa kuwamudu ndio maana walimu ni wachache na wanafunzi ni wengi. Kila mwaka wanaongeza idadi ya wanafunzi kasi ambayo haiendani na uajili wa wafanyakazi.
 
UDOM inaendeshwa kibabe sana na yule prof wa kipare aan no kiswahili. Amekuwa mbele kutishia wafanyakazi wake,anajiona Mungu mtu. Hajui km hata watu wake wa karibu wanamzunguka kwa sasa kiasi kwamba copies za malipo ya 10% zote wamewapatia viongozi wa chama cha walimu. Ilichobakia ni kumlipua vibaya mwezi wa 5,safari hii lazima aende na maji atake asitake. Hawa watu ndio wanaomuharibia JK!
 
Back
Top Bottom