Waraka wa tozo

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,369
54,771
1: Yalipita majuma matatu tangu giza kutawala juu ya nchi, ndege na wadudu warukao waliruka kwa makundi ili kutafuta vijito vya maji ili kutaka kiu katika miili yao.

2: Nao wana wa nchi walikuwa wakimya tena wenye nyuso za kumpendeza BWANA, walikusanyika jioni moja na kupaza sauti zao kuelekea juu huku wakitukuza ukuu wa Mungu na kusema "hakika tumepata yule aliyekuwa sahihi katika taifa letu".

3: Naye alivyosikia hivyo aliinama na kusujudu mbele zao na kuwaomba watwae mikate kwenye vikapu vyao ili kupooza njaa ya miaka mingi waliyokuwa nayo, wana wa taifa lile kusikia hivyo wakakimbilia makapu yao ya hazina na kutoa vipande vya mikate na mvinyo kisha wakanywa na kuoga.

4: Sauti kutoka milima ya Uyunani iliyojaa mamlaka ikasikika "Eeeh Mkuu yawapasa kila mmoja kutupatia kipande kimoja kimoja cha mkate, tazama jinsi maghala yetu yalivyokosa chakula kwanini tusikwapue vipande hivi ili kuvihifadhi kwa ajili yao mkuu"

5: Wana taifa lile walitetemeka juu ya taifa lao na vizazi vyao vikakosa nguvu kwa siku mbili, makundi mengine yalisikika yakisema "hii sauti ya mamlaka ni ya yule mwana wa pili kutoka karibu na familia ya mfalme?" wengine wakisema hapana siye bali ni sauti kutoka ng'ambo iliyokuwa chini kwa miaka mingi na sasa imepazwa.

6: Zikapita siku 5 jua lazama na kuchomoza huku nuru ikiendelea kupotea juu ya misitu na wanyamapori pia wakapaza sauti katika nyika wakililia mikate yao ila mafalisayo wanne walisema "Hii ni kwa ajili ya vizazi vyenu"

7: Walipomaliza kupiga kelele zile ikanyesha mvua na kusomba kila kitu kwenye uso wa nchi ile na kuifanya kuwa mpya na yenye kupendeza kwa wote waliokuwa juu yake.
 
Naam,Bwana na atende kama lilivyokusudi lake,.Na watu wote wa humu JF waseme "Ameeeen!!!
 
Back
Top Bottom