Kwanini Watendaji wa vijiji (VEOs na MEOs) Wanalipwa Mshahara mdogo ukilinganisha na majukumu yao?

camberlizer

New Member
Jan 10, 2018
4
4
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watumishi ngazi ya serikali za Mitaa hasa kada ya Watendaji wa Vijiji (VEO) na Mitaa (MEO). Malalamiko yanayotokana na Mishahara midogo isiyokidhi gharama za maisha. Ukilinganisha na majukumu yao na Mazingira yao ya kazi.

Malalamiko na vilio vyao vinaishia kupotelea hewani kama machozi ya samaki kwenye maji, bila kutafutiwa ufumbuzi. Na bado wanaendelea kuitumikia serikali kwa hali zao zote bila kuleta mgomo wala kufanya maandamano ya aina yoyote.

Hivyo naishauri Serikali iwakumbuke hawa watumishi wao walio wapeleka vijijini mbali na miji yao ya asili, kwajili ya kutekeleza majukumu yao. Kwa nyongeza za mishahara na hata ofa mbalimbali.

TUPAZE SAUTI KWA PAMOJA
 
Wale si wanafanya kazi Local Government - LGA ambao hulipwa kupitia scale zao za TGS

Ukiwa LGA kama una Bachelor degree utalipwa TGS D Kwa Watendaji wa Kata na

Kwa Watendaji wa Vijiji ambao wengi huwa na Diploma utalipwa TGS C

Kwahiyo sioni kama wanaonewa, hayo ni Malipo ya kawaida huko Halmashauri
 
huyu mleta mada alikuwa anapigwa vizinga na mtendaji sasa gia mtu lazima akuanzie mbaliii hasa ukiwa hujui mambo yao..
 
Bila namba hatuwez sema, unaweza dai wanapewa mshahara mdogo kumbe wanakunja 1M
Umenikumbusha Taasisi moja hivi,

Kuna dada alikuwa anaongea sana haki za watunza maua/bustani kwenye ile Taasisi kipindi hicho nilikuwa mgeni...

Nikawa interested kujua wanalipwaje siku moja nikaongea na jamaa kimtindo kucheki salary slip yake inasoma 1.2M.

Nilibaki na maswali mengi
 
Back
Top Bottom