Waraka wa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu Maendeleo ya Mkoa wa Kagera. "Kagera Twafa"

Nasikia wasukuma wananunua sana maeneo ya mapori ya Karagwe na Biharamuro wanakwenda kufanya kilimo na ufugaji.Soon Bukoba itapaa, wasukuma wanasukuma maendeleo sehemu mbali mbali maana ni watumiaji Wazuri na wawekezaji Wazuri.Angalia Katavi, Marinyi, Kilosa morogoro, Lindi, Mbalali, Kasulu.Sukuma hawana utani linapokuja swala la uwekezaji katika kilimo na mifugo
Wahaya wakubali kuachia ardhi wengine wawekeze.
 
Wahaya wanabadilishana nafasi na wenzao waha mmoja mwaka huu anakua wa kwanza mwingine anakua wa pili kutoka mwisho
Nchi hii sisi waha/Wamanyema tunaongoza kuukimbia mkoa wetu adhimu wa Kigoma.
Waha wamehama maelfu kwa maelfu , kigoma yetu sasa hivi imeshikwa na warundi huwezi amini.
Familia nyingi zimehamia Dar Mwanza, Dodoma Tabora Katavi, Shinyanga,Moro nk.
CCM wanaweza kujikuta wanawaongoza warundi wanaojifanya waha.
Watu wa kigoma walianza kuhama tangu miaka ya 70_80,90,2000 mpaka sasa.
Robo tatu ya ukoo wangu pande zote mbili walihama kitambo huko kigoma.
Watu wa ujiji kwao kumegeuka Dar na mwanza.
Serikali lazima ihakikishe inaiokoa Kigoma ni bora hata watani zetu wahaya wanalima ndizi na maharage wanasafirisha mikoa ya kanda ya ziwa, sisi ukilima ndizi/maharage unauza kigoma tu hakuna usafiri wa uhakika .
Kigoma maharage huwa yanauzwa mpaka 700 kwa kilo huwezi amini. zaidi ni mawese tu nayo ni mashamba ya mababu hakuna mashamba mapya ya vijana.
Kigoma imetelekezwa na kila awamu, tunapambana tunavyojua sisi ila msaada wa serikali haupo au ni slow.
imagine kutoka mwanza mpaka Dar kwa basi sh50000 ila Kigoma to Dar sh70000+ kwa sababu barabara ni mbaya.
Ila tutafika tu kwa kujikongoja.
 
... sana! Ni ajabu kusikia mkoa wa Kagera ni mkoa masikini; ajabu mno! Mkoa ambao ni evergreen throughout the year kwanini uwe masikini? Dah!
Uvivu, Roho mbaya, ubinafsi, nankibaya zaidi sasa hivi wamekuwa washirikina....

Wizi...upo usemi kule eti ukilima vanilla, zao lenye pesa na linalostawi Sana huko wezi wanakupa chaguo AU UWAACHE WAIBE AU UJIFANYE KULINDA WAKUUE!
 
Kwanza aache kumuita “mama“ pili hana nia (kuhusu uwezo wake sijui) ya kufanya chochote kupunguza umaskini Tanzania vinginevyo Bwawa la kuzalisha umeme lingemaliziwa lkn linapotezewa, umeme hakuna umaskini ataushughulikia vipi ?
U profesa wake hauba faida naona
 
Miaka 30 ijayo Kilimanjaro na Kagera itakua Kati ya mikoa duni nchini. Naiona Pwani, Morogoro Iringa, Mwanza, Geita, Mbeya Njombe kuaendesha uchumi. Shida ya Kagera na Kilimanjaro ni ukabila wazawa ni wabinafsi sana, wageni wanabaguliwa sana, ardhi imekumabtiwa na wenyeji.

Maendeleo huletwa na wageni. Miji/mikoa isiyokua na ukabila na uzawa itaendelea tu.

Kagera Wahaya waendelee na katelelo tu wamwagiane maji wao kwa wao. Na wilaya za Ngara na unayambo zitaendelea Buhaya itabaki duni mpaka waache ukabila

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
Sehemu yoyote ambayo wazawa hawataki kuchangamana na wageni hubaki duni hivyo hivyo

Hata mkoa wa Tanga nao kuna "usisi" hawataki wageni kabisa hasa handeni,kilindi,pangani,muheza,na mkinga na lushoto


Korogwe na tanga mjini at least mchangamano unaridhisha
 
Kwan mpaka mshike uchumi????

Ishu ni kuhakikisha wew na ukoo wako mnatoka katika ujinga na umaskini.....

Wahaya wa Sasa walishatoka katika zama za kutumia nguvu nyingi akili kidogo kama ngoshaz...


Hebu tafuta makampuni ya ujenzi,wamiliki wa shule( karibu shule zote zinazofanya vizr tz hii zinamilikiwa na wahaya)
Tafuta engineering companies kama biotech,abemulo, luganuza, Rabininsia, Kairuki,kareju na mshumbusi zote zinamilikiwa na Koo za kihaya...

Koo za kihaya zimeenda mbali na kukuta maingeneer humo,madaktari,walimu ,wafanyabiashara humo.....

Ndo maana elimu inakumbatiwa sana

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Hao maengineer uchwara wamewasaidia nini? Kama wasomi mnao tokea uhuru lakini bado mnalialia hapa! Stend tu mmeshindwa kujenga!
 
Wahaya bhana kujitutumua! Niambie hata huko kanda ya ziwa wapi mmeshika uchumi!? Kwenye madini hampo,biashara za kawaida mpo wachache, yaani nyinyi mmekazania elimu tu lakini niwakumbushe elimu ya makaratasi bila maarifa ya kutafuta maisha kila sehemu mtabaki kama mlivo!
Elimu ndiyo kila kitu, huoni msukuma mwemzenu aliyekuwa anaiponda elimu anavyotambia phd yake feki.
 
Tibaijuka Yeye amekua Waziri katika Serikali, mbona hatujawai kusikia anawasemea wana kagera, amekuwa mbunge miaka 10, hatukuwai kuona hata akisemea zao kuu la biashara kahawa, wakati Nchi jirani Uganda kahawa ni bei ni zaidi ya mala 3, mpaka kagera tunatamani kuuza Uganda.Tibaijuka alichokifanya alipopata ubunge na uwaziri ni kujimilikisha aridhi tu,akuna alichosaidia chochote, Sasahivi eti anapiga kelele.
Wakati anasema kadiri unavopanua ndo watu wanazid kutaman ulikua wapi

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wazalendo wote nchini na Duniani kwa Ujumla

Nimeambatanisha Waraka Kutoka kwa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu uduni wa Maendeleo kwa Mkoa wa Kagera

View attachment 2082264

View attachment 2082267

View attachment 2082268

View attachment 2082269
Jamani tuwe wakweli.Huyu mama ameandika ukweli.Mkoa umetelekezwa.Hakuna shughuri za vijana kujipatia kipato.Maeneo ya ardhi ambayo yalitumika kulima mazao Kama njugu mawe, ulezi,Karanga, mtama, hayapo tena.Yamenunuliwa na watu ambao wanaishi nje ya mkoa na kupanda miti. Kwakweli hili ni janga kubwa. Wahaya wamebakiza kwenda nyumbani wakati wa misiba na Christmas kwa kuwanunulia vijana waliochoka gongo.Nyumba za kifahari zilizojengwa vijijini wanaishi popo.
 
Waraka unaosemekana umeandikwa na Prof Msomi wa kihaya Anna Tibaijuka ukionesha Dunia jinsi mkoa wa Kagera unavyorudi nyumba kimaendeleo ni waraka ambao umebeba ujumbe ambao haukustaili kuandikwa na Anna Tibaijuka, au mtu kama Wilsoni Masilingi.

Watu hawa wekuwa viongozi wa wakubwa katika serikali za awamu tofauti, mathalani mtu kama Prof amekuwa mbunge wa huko huko mkoani kagera lakini unaambiwa hakuna Alichokifanya zaidi ya kusambaza maji pale Muleba.

Ukienda kwa ta Mwami Wilsoni Masilingi aliishia kuchonga ndevu na kupaka piko bungeni hakuna aliro lifanya ,leo hii wapo nje ya mfumo wanaanza kuropoka ovyo pasipo kuja na suluhisho.

Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.

Anna Tibaijuka akiwa mbunge alishindwa hata kuomba barabara ya lami leo hii barabara zinajengwa anaona wivu yeye aliishia kuongea lugha za ajabu ajabu bungeni mfano ile ya KUPANUA na nyingine atulie hata afanyeje Samia hawezi enda na kizee kama yeye apambane na Hali yake.
 
1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.

2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.

3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa 26; kama mtu ambaye ameona haya yote yakitokea.

4. Sababu ya kwanza ni demographic na nategemea Prof. aielezee hii point. Kupiga hatua katika elimu bila kukua kwa viwanda au estate agriculture kuweza kuwaajiri wasomi wake huko kumesabaisha brain drain ya watu wetu walio kwenye productive age kuajiriwa nje ya mkoa wetu na kwa hiyo kuchangia kuendeleza mikoa mingine ya Tanzania.

Tumeacha watoto na wazee ambao mchango wao katika uzalishaji ni haba wakibaki kulima mashamba ya migomba na mibuni iliyopandwa miaka 100 iliyopia. Wachache walio na uwezo wa kuzalisha wamezembea kuhamia mahala ambako wangejiongeza kiuzalishaji na kuendekeza land fragmentation; mojawapo ya sababu ikiwa kuishi kwa invisible earnings kutoka kwenye mishahara ya jamaa zao walioko nje ya mkoa.

5. Sababu nyingine ni historical disruptions za

(a) Vita ya Tanzania na Uganda au na Idi Amin. Wengi huiona kama athari katika miaka ya 1978 mpaka 1980;
wanasahau kwamba uhusiano na Uganda ulififia kwa miaka zaidi ya 10 kuanzia 1971. Mathalan uwekezaji wa Serikali/NAFCO katika shamba la Ngano Kibanda, Murongo, lililokuwa mechanised ukiwa na matrekta hadi combine harvestor, ulisitishwa kwa kuhofia Amin asipate target ya kupiga mabomu. Prof. atafiti agundue kwa nini Serikali haikuendelea nao baada ya vita.

(b) Pili, ni Vita ya Kiuchumi ya Sokoine ambapo tofauti na mikoa mingine, wafanyabiashara wote muhimu katika mkoa waliswekwa ndani, na malori zaidi ya 400 yalikamatwa na kuteketea Kaitaba Stadium. Prof. na wasomi wengine watupe kiwango cha economic disruption iliyotokana na vita hiyo na fidia ambayo haikutolewa. Sheria maalumu kutaifisha malori yasiyozidi miaka 5 ambayo ilihusu Kagera tu ilikuwa ya kibaguzi na fidia ilikuwa kiduchu,ambayo kutokana na inflation,hawakuweza kununua lori nyingine. Nilishangaa sifa alizopewa Nsa Kaisi miaka ya karibuni, bila watu kukumbuka ukatili(sadism) alioufanyia mkoa wa Kagera. Serikali na CCM walipaswa kutengeneza Marshall Plan ya kuwekeza katika mkoa kuurudisha kwenye maendeleo iliyokuwa nayo.

(c) Mathalan,mwaka 1967 serikali ilipotaifisha mabenki na Viwanda, kampuni ya West Lake Bus Service iliyokuwa na mabasi ya routes zote mkoani ilifilisiwa na wamiliki wa Kihindi na kukomba hela yote na kumwacha Mzee Daniel K Rwiza, mtu aliyedhamini watu kujenga nyumba za bati Karagwe, kubaki masikini. Shida zote za usafiri mkoani tangu hapo mpaka miaka ya 1990s zinaanzia hapo,na ziliathiri mkoa sana.

Nadhani nimempa Prof. Anna na wapenda maendeleo wa Mkoa wa Kagera nafasi ya kuanzia. Sijataja athari za kuhujumu BCU,kuleta Mamlaka ya Kahawa na kuanzisha BCU (1990) Ltd na KDCU bila mali za Union zote kupatikana nyingine zikichukuliwa na RTC na CCM kuchukua kiwanja cha Union ambako kumejengwa makao makuu ya CCM ambayo ni gofu ambalo halikwisha na halitaisha.

Wakati yote hayo yanatokea viwanda vinajengwa Mbeya, Mwanza, Moshi, Arusha tulikuwa na viongozi wazawa. Nani tumlaumu?
 
Back
Top Bottom