Waraka: Alphonce Lusako alias Emekha Ikhe kwako prof. Rwekaza Mkandala

comrade,,we are probable arleady dead man.so i will never fear any man in this world till i will die.
emekha.
 
Ndugu Lusako nilishakushauri sana kuhusu jambo lako na kwamba hawa wazee hawana sababu ya kulumbana na wewe au wenzio na nikimnukuu Mukandala kuwa wanajisikia vibaya kutimua mwanafunzi, hivyo nakusihi kuwa huna ubavu wa kulumbana au kupambana na baraza la chuo au taasisi yoyote.

Tuliza akili ndugu yangu, jitathmini nnje ya siasa na nnje ya uharakaharaka kisha urudi kundini kama Sauli aka Daudi.
 
Watz tunapenda kulialia mpaka tunakera ooh Mungu ooh Yesu.. ooh Muhamad..SijakuelewaShughulikia tatizo lako kisayansi, jichange usome chochote hata mgambo mbele kwa mbeleFisadi wa elimu Mukandara yupo na anazidi kula bata, dua la kuku..
 
Ndugu Lusako leo nimekutana na baadhi ya vijana waliokubali kuandkika barua kuomba warudishwe chuo na kwa taarifa walizonipa na kunidhihirishia kwa kunionesha barua toka Baraza la chuo ni kwamba wamerudishwa chuo bila masharti yoyote. Narudia kukusihi wewe na wenzio mnaoteseka kwa kijiba maana nadhani nikisema kiburi kisicho na maana hutanielewa, andika barua ya kurudi nakuone huruma ndugu maana hali ya mtaani naifahamu hasa unapokua katika hali uliyo nayo. Wenzio kama aliyekuwa speaker amerudi na wengine takribani 16. Nimesikia kuwa yule dada alijiita mgumu mfupi hivi nae ameandika barua ya kuomba radhi sasa ujichunguze maana mwisho wa siku utabaki mwenyewe na faida kidogo.

Huo ni ushauri wangu tu si lazima waweza umeza au kuutema.
 
comrade,,we are probable arleady dead man.so i will never fear any man in this world till i will die.
emekha.

Mpaka leo hujui kwanin umefkuzwa,hujiamini kbsa dogo,pamoja na upuuzi ambao unasema bado unamwita muheshimiwa?
Unajua maana ya neno MH!?
Jipange sana,haki haiji inataftwa,sasa tafta haki yako na kama ni yako jua utaipata tu
 
WARAKA WA ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE KWAKO PROF. RWEKAZA MKANDALA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

NI VEMA UNGENIPIGA RISASI NIKAFA NIKAPOTEA DUNIANI KWA UDHALIMU ULIOSHINIKIZWA KUFANYA JUU YANGU NA WANAFUNZI WENZANGU NDANI YA TAIFA LANGU.KULIKO KUKUPIGIA MAGOTI NA KUDHARAU UTU WANGU KWA KUKUOMBA MSAMAHA USIOTOKANA NA DHAMIRA YA MOYO WANGU. HOW LONG FOR THESE INJUSTICES IN MY COUNTRY….? NOT LONG MR. PROFESSOR.

Pilato anamuhukumu yesu ingawa haoni kosa lake, anawaogopa wayaudi, anabembeleza urafiki wa kaysari. Ee Yesu usiye na kosa, hata mimi ningeweza kutenda mema mengi lakini naogopa macho ya wenzangu na maneno yao. Ee bwana uniimarishe utashi wangu nijitegemee katika kushika madaraka yangu.

"Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda". Ni maneno yako Prof. Rwekaza Mkandala uliyoyatoa tarehe 14/12/2012, katika ofisi yako tukiwa na kikao baina ya sisi wanafunzi nane {8}tuliokwisha fukuzwa UDSM kwa maandamano niliyoyaongoza tarehe 11/11/2011, ya kudai haki za watoto wa wavuja jasho walionyimwa mikopo ndani ya vyuo vikuu vya umma nchini, akiwepo Prof. Makenya Maboko na Prof. Yunus Mgaya.".nilisikitishwa sana na kauli yako ambayo mpaka leo naikumbuka "chuo hiki kinawenyewe na wenyewe wako mjini".

Mimi binafsi nafahamu kwa dhati ya moyo wangu kuwa chuo hiki ni cha watanzania na si cha mtu binafsi au genge la wahuni Fulani ambao wako mjini kama ulivyosema ambao wanaamua kufanya lolote baya wanalolitaka kulifanya sababu ya madaraka waliyonayo. Tumewapeni madaraka na mamlaka ya kutuongoza kwa mujibu wa katiba ya nchi yangu na hatujawapa madaraka hayo kama nyundo ya kuwapigia wavujajasho ndani ya taifa langu.

Mh. Profesa, nimeona nikusalimu kwa kumbukumbu iliyopo hapo juu na niendelee na maada iliyonisibu, lakini pia usisahau kuwahabarisha usalama wa taifa unaofanya nao kazi, maprofesa wengine hata wanaotoka vyuo vingine ambao walishiriki kufanya maamuzi ya kidikteta ya kuwafukuza wazalendo wa taifa hili ambao naamini ni maraisi wajao, mawaziri wajao, wabunge wajao, wakuu wa mikoa na wilaya.nk.. ndani ya vyuo vyao kwa kushinikizwa na wanasiasa walioko mjini kama ulivyokuwa ukijitetea machoni petu kinyume na kweli uliyokuwa unaifahamu.

Lakini pia ni vyema ukawataarifu hao binadamu wa mjini waliokuwa wanakushinikiza kufanya maamuzi ambayo moyo wako haukuridhia, wataarifu kuwa kijana Yule Yule niliyemtimua UDSM amesema kuwa "madaraka mliyo nayo sio ndoa ya milele hivyo waitendee haki nchi yangu, Nguvu ya pesa walizonazo hazina nafasi milele ya kupoteza haki ya binadamu yoyote Yule kwa sababu Mungu ni taa ya kila mwanadamu.

Kwa kitendo ulichonifanyia na ulichowafanyia wanafunzi wenzangu ambao mpaka sasa wamepoteza ndoto zao kielimu ndani ya Taifa lao hakita potea hivi hivi kama unavyofikiri, kwa sababu ni kinyume na katiba ya nchi yetu ibara ya 11[2,3] inayotoa fursa kwa kila mtanzania kupata haki yake ya msingi kielimu ndani yataifa lake.

Mh. Profesa, nakumbuka taarifa za upotoshwaji ulizozitoa mbele ya vyombo vya habari juu yangu na juu ya wanafunzi wenzangu zenye lengo la makusudi la kuchafua taswira zetu kwa jamii. Ni ukweli kwamba unamamlaka, unanguvu ya Pesa na unashirikiana na mfumo wa usalama wa taifa na uongozi uliopo madarakani kuyafanya uliyoyafanya na unayoendelea kuyafanya. ndio maana uliweza kutumia vyombo vya habari vibaya lakini utambue kuwa haki ya mtu inacheleweshwa tu haipotei, hata ningepigwa risasi kwa wakati huo naamini wapo wazalendo wangesimama kutetea haki yangu nikiwa kaburini.

Ni ukweli kwamba Umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na familia zetu, ndugu na jamaa, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuudanganya umma, umefanikiwa pia kwa kiasi kikubwa, kutoa taarifa za uongo ndani ya mfumo na nje ya mfumo. lakini hujafanikiwa kitu kimoja cha msingi kunitenga mimi au sisi na Mwenyezi Mungu.

Mh.profesa, nimeona umekuwa ni profesa mmoja hatari sana ndani ya nchi yangu uliyekubali kudharau utu na taaluma ya uprofesa ulionao, uliyekubali kuminya uwezo wako halisi wa kifikra kwa sababu ya shinikizo la wanasiasa unaodai wako mjini ambao kiuhalisia hawana hata uprofesa ulionao. Umekubali kuwaabudu mashetani wanaokushinikiza kufanya zambi za makusudi katika kupoteza ndoto za vijana watokao katika familia za wavujajasho. umekuwa ni pilato wa enzi za YESU.

Utambue kuwa Vilio vya vijana tuliofukuzwa vyuoni, vilio na manunguniko ya ndugu, jamaa na wazazi wetu, dua tulizoomba kwa Mwenyezi Mungu, hakika zimemfikia Mwenyezi Mungu na usubiri majibu yake wakati wowote tangia sasa. Ni heri vita inayotafuta haki kuliko kuendelea kuabudu shetani mwenye majina matatu "HOFU, WOGA NA SHAKA". Ni heri nipigwe risasi katika mapambano haya nikaweka historia ndani ya taifa langu kuliko nikaacha dhamira yako ya dhati ikanimaliza ndani ya taifa langu kimya kimya. Lakini pia NI BORA NIKAWA FORM SIX LEAVER MILELE, MWENYE FIKRA HURU KWA MASLAHI YA WATANZANIA KULIKO NIKAKUBALI KUUZA NA KUUDHARAU UTU WANGU KWA KUMUOMBA MSAMAHA PROFESA YOYOTE YULE ANAYEKANDAMIZA HAKI ZA WANYONGE NDANI YA NCHI YANGU.

Mh. Profesa, unalizika Taifa langu kwa kuzika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mwenendo hasi wa chuo kikuu chochote kile duniani ni muenendo hasi wa taifa husika. Umekuwa ni profesa kiongozi wa kulizika taifa langu na hii nikutokana na upeo wa mtazamo wangu. Umehusika kikamilifu katika harakati za kuzima fikra huru za wanafunzi ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam, unatumia madaraka yako vibaya kwa kuwafukuza wanafunzi waliojitambua, wenye uwezo wa kuhoji mambo, kukosoa mambo, na kushauri mambo kwa mustakabali mwema wa taifa lao.

Unamikakati ya makusudi ya kukiweka chuo kikuu cha Dar es Salaam kiwe genge la wahuni, genge la walanguzi na kisiwe kisima cha fikra huru "think tank of our nation" kama mwanzo kilivyokuwa, unamalengo ya dhati ya kutengeneza Taifa la Mambumbumbu ili watoto zenu na watoto wa viongozi wenzako walioko madarakani waendelee kulitawala taifa langu milele, unawafundisha wasomi nidhamu ya uoga, unashirikiana na usalama wa taifa kuwatisha wasomi wawe ni wasomi wa madesa na si kulisaidia taifa lao kwa kujadili mustakabali wa taifa lao.

Unaendelea kuwa chanzo cha kuzalisha viongozi mbumbumbu wataoligharimu taifa langu kama wengine walivyoligharimu taifa hili. Nikueleze ukweli kuwa Ukimya wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine nchini Unabomu zito litalolipuka mda wowote tangia sasa. Umewakandamiza kwa mda mrefu, wasomi wanamatatizo mengi ambayo yanahitaji kutatuliwa kidiplomasia, kwa sababu unatumia nguvu kubwa kuwanyamazisha hakika watatatua matatizo yao kwa nguvu. Huu ni unabii wangu ambao hakika siku za usoni utatimia. Umefika wakati wako wa kusoma alama za nyakati. Wasomi wamechoshwa kukandamizwa, wasomi wanataka walisaidie taifa lao ambalo kwa mda mrefu limekuwa shamba la bibi.

Wasomi wanataka kuwa na uhuru wa mawazo, uhuru wa kukusanyika na kujadili mabadiliko wayatakayo ndani ya taifa lao. Tusipopata mabadiliko kwa njia ya kidiplomasia tutayapata kwa njia ya nguvu.

Mh. Profesa, Napenda ufahamu kuwa duniani hakuna jipya, mtesa na mteswa wote hatima yao kifo yaani binadamu huishi mara moja tu na hufa. Hakuna mtu kutokana na madaraka yake, vyeo vyake, umaarufu wake, hadhi yake ya elimu atakufa atazikwa hewani. Sisi sote tutarudi vumbini. Jaribu kuitendea haki taaluma ya uprofesa kwa kulisaidia Taifa hili, kinyume na hilo utabakia na uprofesa wa jina usio na faida ndani ya taifa langu.

Nimefikia sehemu ninahoji uhalali wa uprofesa wako kwa sababu, mambo unayoyafanya ndani ya Taifa langu yananipa wasiwasi kwani hayaendani na taaluma uliyonayo. Mh.Profesa naomba litendee haki taifa langu, wewe ni mzee kwa umri sasa tuachie vijana tutaoishi na taifa hili kwa mda mrefu. Kiac

Kwa hili kamanda usikatishwe tamaa hata Mnyika aliishia mwaka wa pili lakini angalia representation zake ni zaidi ya huyo professor but remmember if not in this way there is other way so keep it up the struggle
 
Ndugu zangu wana JF nimeona kwenye gazeti la Mwananchi leo taarifa kuhusu kukwama kwa rufaa ya waliofukuzwa UDSM. Taarifa hiyo inasema wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa haina uwezo wa kukiamuru chuo hicho kuwarejesha chuoni baada ya kushinda kesi.

Nadhani tutakumbuka hapo awali nilishamshauri ndugu Lusako kuhusu haya mambo. Kesi wanazoziendesha kimsingi ndizo zinazozuia Baraza la Chuo UDSM lililo chini ya Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba kutothubutu hata kutaja majina yao kwenye vikao vya baraza. Hivi karibuni nitoa habari ya baadhi ya waliofukuzwa wamerudishwa bila hata amri ya mahakama bali ni wao kufuata ushauri wa kuomba msamaha kila mmoja kwa namna yake kuna mmoja ameniambia aliandika barua ikapita kwa diwani, mbunge (tena mbunge kupitia CHADEMA) na kwa mkuu wa wilaya ikaenda kwa Mwenyekiti wa baraza kupitia kwa Makamu Mkuu wa Chuo huyo huyo Mukandala anayemkebehi na kumdhihaki humu.

Nataka kuwashauri hawa ndugu pia kuwa katika hali ya kawaida baraza la chuo limepewa mamlaka kisheria na mahakama hiyo ya kisutu haina mamlaka ya kuliamuru baraza hilo. Kufukuzwa chuo kulifanywa na baraza siyo Mukandala lazima tukubaliane na hilo na baraza hilo siyo lililokupeleka mahakamani bali ni polisi ambayo mlikataa kutii amri halali ya kutokuandamana nnje ya mipaka ya chuo lakini tukataka kutoka kwenda mjini kupitia Ubungo ikala kwetu. Kwahiyo nadhani kuna umuhimu wa kuconsult kina Mabere Marando au Tundu Lisu au mwanasheria mnayemuamini awashauri zaidi kuhusu swala hili. tutapoteza muda na hela bila mafanikio yoyote.

Ni ushauri tu unaweza kumeza au kutema
 
Bw Lusako,jikusanye ,wewe na family ukamalizie degree yako nje.UDSM ni political institution,sio tena kitovu cha wasomi wenye akili independent ,ni wachache sana.

Sijui ulikuwa unachukua digrii gani,i assume wewe nado ni kijana,unaweza kwenda India,au Sauz eleimu bado sio ghali sana.
Kuomba msamaha ni against your principle.Wameshaku black list huwezi kupata ajira nzuri tena serikalini.Labda uwe kama msaliti wa maadili,Bw James Mbatia,hakumaliza degree baadae magamba na UWT wamemnunua!Angalia anachofanya.

Usije likakukuta hili.Serikali hii ni ya visasi,huwezi ukaone serikali yoyote duniani inamtesa medical doctor eti sababu ya migomo ya madactari(Dr Ulimboka).Kuna uozo mkubwa sana ,itachukua muda kuuondoa .

UDSM tangu Luhanga then Mukandara inafanya kazi kwa maagizo ys serikali na UWT.Hakuna independence.kama wewe ni mtoto wa kilaza wa CCM/serikali huwezi kufeli hata siku moja.Phd nazo za kupeana!Refer to Hosea,Magufuli na Feleshi.

Hivyo Bw Lusako naamini ukiandika barua nyingi kwa taasisi zinazopenda free thinking,,ukaeleza matatizo yako utapata sponsor kumalizia degree yako nje ya nchi.Waachie design ya kina prince wapate degree zao pale.

Pale walipomwashisha Prof Mwaregu eti amezeeka it is begar belief

Usije wa ku-Mbatia,maana ulaji ni weakness ya mwanadamu hasa mwafrika.
 
NI VEMA UNGENIPIGA RISASI NIKAFA NIKAPOTEA DUNIANI KWA UDHALIMU ULIOSHINIKIZWA KUFANYA JUU YANGU NA WANAFUNZI WENZANGU NDANI YA TAIFA LANGU.KULIKO KUKUPIGIA MAGOTI NA KUDHARAU UTU WANGU KWA KUKUOMBA MSAMAHA USIOTOKANA NA DHAMIRA YA MOYO WANGU. HOW LONG FOR THESE INJUSTICES IN MY COUNTRY….? NOT LONG MR. PROFESSOR.

hakika kijana hata kama una msimamo huo ulionao lakini kumbuka ungeweza kujishusha chini na kukubali kuomba msamaha ili uweze kupata elimu amabayo unasema ni haki yako,ukiwa na msimamo huo utaendelea kulilia humu mitandaoni bila tija yoyote,wale uliowapigania sasa wengine wameshamaliza na wapo makazini we bado una hangaika tu.

. Kwa wale wote walioandika barua za msamaha kwenu hawakujua walitendalo,walivamiwa na shetani mwenye majina matatu “HOFU, SHAKA NA WOGA”.
kwangu mimi hao hata kama ni hofu,shaka na woga ndio vilivyowafanya waombe msamaha kama unavyosema wewe:naona ni watu waliochukua maamuzi ya busara ili tu waweze kupata kile wanachokihitaji kwani kama ni mapambano wanaweza kuyafanya hata baada ya kupata kile wanachokihitaji.

ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE. ?

NB:pOLE KWA YALIYOKUKUTA ILA USHAURI WANGU NI KWAMBA BORA UFANYE YALE WANAYOYATAKA KWA MUDA HUU ILI UWEZE KUTIMILIZA NDOTO YAKO YA KUPATA ELIMU VINGINEVYO NDUGU YANGU MALALAMIKO YAKO HAYATAISHA MAJUKWAANI.NI BORA UJIFANYE MJINGA ILI UPATE UNACHOKITAKA.FIKIRIA WALE ULIOKUWA UKIWAPIGINIA HIYO HAKI WAKIO WAPI?JE HATA SIKU MOJA WAMEAHI KUKUMBUKA?YOU STAND ALONE
Ulimjibu vizuri
 
Poleh,umehshajaribu kufanya application chuo Kingine kijana?..huwezi jua Mungu kakuandalia nini, ukute anataka uache hili sakata na UDSM akutumie sehemu nyingine, tafakari upya
Sometimes js let it go and start over...
Changamoto ya Ada ikiwepo unaweza share watu wakakuchangia
 
(a)Masuala ya risasi na kufa yanatoka wapi?
Upo tayari kufa,kwa ajili ya nini hasa?Siasa za Chuo?Kufa ni sifa?
Utaondoka ukiwa umejiandaa?Utakuwa na uhusiano mzuri na Kristo Yesu?
Maana ukiondoka kijasiri,lakini ukiwa humjui Masiha,utakuwa umepata hasara kubwa.Sijakuelewa;jitafakari upya.
(b) Kwa uandishi wa hovyo namna hiyo,ninapata shida kuelewa ikiwa ulikwenda kujifunza.
(c) Andika kwa heshima hoja zako bila kushambulia Viongozi wa Chuo.
 
WARAKA WA ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE KWAKO PROF. RWEKAZA MKANDALA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

NI VEMA UNGENIPIGA RISASI NIKAFA NIKAPOTEA DUNIANI KWA UDHALIMU ULIOSHINIKIZWA KUFANYA JUU YANGU NA WANAFUNZI WENZANGU NDANI YA TAIFA LANGU.KULIKO KUKUPIGIA MAGOTI NA KUDHARAU UTU WANGU KWA KUKUOMBA MSAMAHA USIOTOKANA NA DHAMIRA YA MOYO WANGU. HOW LONG FOR THESE INJUSTICES IN MY COUNTRY - NOT LONG MR. PROFESSOR.

Pilato anamuhukumu yesu ingawa haoni kosa lake, anawaogopa wayaudi, anabembeleza urafiki wa kaysari. Ee Yesu usiye na kosa, hata mimi ningeweza kutenda mema mengi lakini naogopa macho ya wenzangu na maneno yao. Ee bwana uniimarishe utashi wangu nijitegemee katika kushika madaraka yangu.

"Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda".

Ni maneno yako Prof. Rwekaza Mkandala uliyoyatoa tarehe 14/12/2012, katika ofisi yako tukiwa na kikao baina ya sisi wanafunzi nane {8}tuliokwisha fukuzwa UDSM kwa maandamano niliyoyaongoza tarehe 11/11/2011, ya kudai haki za watoto wa wavuja jasho walionyimwa mikopo ndani ya vyuo vikuu vya umma nchini, akiwepo Prof. Makenya Maboko na Prof. Yunus Mgaya.".nilisikitishwa sana na kauli yako ambayo mpaka leo naikumbuka "chuo hiki kinawenyewe na wenyewe wako mjini".

Mimi binafsi nafahamu kwa dhati ya moyo wangu kuwa chuo hiki ni cha watanzania na si cha mtu binafsi au genge la wahuni Fulani ambao wako mjini kama ulivyosema ambao wanaamua kufanya lolote baya wanalolitaka kulifanya sababu ya madaraka waliyonayo. Tumewapeni madaraka na mamlaka ya kutuongoza kwa mujibu wa katiba ya nchi yangu na hatujawapa madaraka hayo kama nyundo ya kuwapigia wavujajasho ndani ya taifa langu.

Mh. Profesa, nimeona nikusalimu kwa kumbukumbu iliyopo hapo juu na niendelee na maada iliyonisibu, lakini pia usisahau kuwahabarisha usalama wa taifa unaofanya nao kazi, maprofesa wengine hata wanaotoka vyuo vingine ambao walishiriki kufanya maamuzi ya kidikteta ya kuwafukuza wazalendo wa taifa hili ambao naamini ni maraisi wajao, mawaziri wajao, wabunge wajao, wakuu wa mikoa na wilaya.nk.. ndani ya vyuo vyao kwa kushinikizwa na wanasiasa walioko mjini kama ulivyokuwa ukijitetea machoni petu kinyume na kweli uliyokuwa unaifahamu.

Lakini pia ni vyema ukawataarifu hao binadamu wa mjini waliokuwa wanakushinikiza kufanya maamuzi ambayo moyo wako haukuridhia, wataarifu kuwa kijana Yule Yule niliyemtimua UDSM amesema kuwa "madaraka mliyo nayo sio ndoa ya milele hivyo waitendee haki nchi yangu, Nguvu ya pesa walizonazo hazina nafasi milele ya kupoteza haki ya binadamu yoyote Yule kwa sababu Mungu ni taa ya kila mwanadamu.

Kwa kitendo ulichonifanyia na ulichowafanyia wanafunzi wenzangu ambao mpaka sasa wamepoteza ndoto zao kielimu ndani ya Taifa lao hakita potea hivi hivi kama unavyofikiri, kwa sababu ni kinyume na katiba ya nchi yetu ibara ya 11[2,3] inayotoa fursa kwa kila mtanzania kupata haki yake ya msingi kielimu ndani yataifa lake.

Mh. Profesa, nakumbuka taarifa za upotoshwaji ulizozitoa mbele ya vyombo vya habari juu yangu na juu ya wanafunzi wenzangu zenye lengo la makusudi la kuchafua taswira zetu kwa jamii. Ni ukweli kwamba unamamlaka, unanguvu ya Pesa na unashirikiana na mfumo wa usalama wa taifa na uongozi uliopo madarakani kuyafanya uliyoyafanya na unayoendelea kuyafanya. ndio maana uliweza kutumia vyombo vya habari vibaya lakini utambue kuwa haki ya mtu inacheleweshwa tu haipotei, hata ningepigwa risasi kwa wakati huo naamini wapo wazalendo wangesimama kutetea haki yangu nikiwa kaburini.

Ni ukweli kwamba Umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na familia zetu, ndugu na jamaa, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuudanganya umma, umefanikiwa pia kwa kiasi kikubwa, kutoa taarifa za uongo ndani ya mfumo na nje ya mfumo. lakini hujafanikiwa kitu kimoja cha msingi kunitenga mimi au sisi na Mwenyezi Mungu.

Mh. Profesa, nimeona umekuwa ni profesa mmoja hatari sana ndani ya nchi yangu uliyekubali kudharau utu na taaluma ya uprofesa ulionao, uliyekubali kuminya uwezo wako halisi wa kifikra kwa sababu ya shinikizo la wanasiasa unaodai wako mjini ambao kiuhalisia hawana hata uprofesa ulionao. Umekubali kuwaabudu mashetani wanaokushinikiza kufanya zambi za makusudi katika kupoteza ndoto za vijana watokao katika familia za wavujajasho. umekuwa ni pilato wa enzi za YESU.

Utambue kuwa Vilio vya vijana tuliofukuzwa vyuoni, vilio na manunguniko ya ndugu, jamaa na wazazi wetu, dua tulizoomba kwa Mwenyezi Mungu, hakika zimemfikia Mwenyezi Mungu na usubiri majibu yake wakati wowote tangia sasa. Ni heri vita inayotafuta haki kuliko kuendelea kuabudu shetani mwenye majina matatu "HOFU, WOGA NA SHAKA". Ni heri nipigwe risasi katika mapambano haya nikaweka historia ndani ya taifa langu kuliko nikaacha dhamira yako ya dhati ikanimaliza ndani ya taifa langu kimya kimya. Lakini pia NI BORA NIKAWA FORM SIX LEAVER MILELE, MWENYE FIKRA HURU KWA MASLAHI YA WATANZANIA KULIKO NIKAKUBALI KUUZA NA KUUDHARAU UTU WANGU KWA KUMUOMBA MSAMAHA PROFESA YOYOTE YULE ANAYEKANDAMIZA HAKI ZA WANYONGE NDANI YA NCHI YANGU.

Mh. Profesa, unalizika Taifa langu kwa kuzika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mwenendo hasi wa chuo kikuu chochote kile duniani ni muenendo hasi wa taifa husika. Umekuwa ni profesa kiongozi wa kulizika taifa langu na hii nikutokana na upeo wa mtazamo wangu. Umehusika kikamilifu katika harakati za kuzima fikra huru za wanafunzi ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam, unatumia madaraka yako vibaya kwa kuwafukuza wanafunzi waliojitambua, wenye uwezo wa kuhoji mambo, kukosoa mambo, na kushauri mambo kwa mustakabali mwema wa taifa lao.

Unamikakati ya makusudi ya kukiweka chuo kikuu cha Dar es Salaam kiwe genge la wahuni, genge la walanguzi na kisiwe kisima cha fikra huru "think tank of our nation" kama mwanzo kilivyokuwa, unamalengo ya dhati ya kutengeneza Taifa la Mambumbumbu ili watoto zenu na watoto wa viongozi wenzako walioko madarakani waendelee kulitawala taifa langu milele, unawafundisha wasomi nidhamu ya uoga, unashirikiana na usalama wa taifa kuwatisha wasomi wawe ni wasomi wa madesa na si kulisaidia taifa lao kwa kujadili mustakabali wa taifa lao.

Unaendelea kuwa chanzo cha kuzalisha viongozi mbumbumbu wataoligharimu taifa langu kama wengine walivyoligharimu taifa hili. Nikueleze ukweli kuwa Ukimya wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine nchini Unabomu zito litalolipuka mda wowote tangia sasa. Umewakandamiza kwa mda mrefu, wasomi wanamatatizo mengi ambayo yanahitaji kutatuliwa kidiplomasia, kwa sababu unatumia nguvu kubwa kuwanyamazisha hakika watatatua matatizo yao kwa nguvu. Huu ni unabii wangu ambao hakika siku za usoni utatimia. Umefika wakati wako wa kusoma alama za nyakati. Wasomi wamechoshwa kukandamizwa, wasomi wanataka walisaidie taifa lao ambalo kwa mda mrefu limekuwa shamba la bibi.

Wasomi wanataka kuwa na uhuru wa mawazo, uhuru wa kukusanyika na kujadili mabadiliko wayatakayo ndani ya taifa lao. Tusipopata mabadiliko kwa njia ya kidiplomasia tutayapata kwa njia ya nguvu.

Mh. Profesa, Napenda ufahamu kuwa duniani hakuna jipya, mtesa na mteswa wote hatima yao kifo yaani binadamu huishi mara moja tu na hufa. Hakuna mtu kutokana na madaraka yake, vyeo vyake, umaarufu wake, hadhi yake ya elimu atakufa atazikwa hewani. Sisi sote tutarudi vumbini. Jaribu kuitendea haki taaluma ya uprofesa kwa kulisaidia Taifa hili, kinyume na hilo utabakia na uprofesa wa jina usio na faida ndani ya taifa langu.

Nimefikia sehemu ninahoji uhalali wa uprofesa wako kwa sababu, mambo unayoyafanya ndani ya Taifa langu yananipa wasiwasi kwani hayaendani na taaluma uliyonayo. Mh.Profesa naomba litendee haki taifa langu, wewe ni mzee kwa umri sasa tuachie vijana tutaoishi na taifa hili kwa mda mrefu. Kiache chuo kikuu cha Dar es salaam kiwe huru. Usiendeleza udhalimu uliokwisha tufanyia sisi, kinyume na hayo dhambi hii itakutafuna leo na mpaka kaburini kwako.

Namalizia kwa kumnukuu Hayati Mwalim. J.K. Nyerere aliyesema kuwa kazi kubwa ya vyuo vikuu ni kutafuta ukweli, kusema ukweli na kuuishi ukweli huo kwa gharama yoyote ile bila kujali madhara yatakayokutokea kutokana na kweli uliyoisimamia. Nitasema ukweli daima fitina kwangu mwiko. Kwa wale wote walioandika barua za msamaha kwenu hawakujua walitendalo,walivamiwa na shetani mwenye majina matatu "HOFU, SHAKA NA WOGA".

Kwa sasa wanajuta, wamekubali kushusha utu wao kwa sababu ya ukatili wenu. Niliwahi jiuliza swali moja kwa nini waasi wanatokea katika mataifa mengine, nimepata jibu kutokana na mazingira niliyopo tusifikie huko lakini najua unakifahamu ulichokifanya, najua unafahamu upotoshwaji ulioufanya ndani ya mfumo wa uongozi wa nchi hii na nje ya mfumo, najua unafahamu umepoteza nafsi ngapi za vijana kwa kupoteza ndoto zao kielimu. Yote haya uyapime katika mizani ya haki na ujiulize kutokana na uliyo yafanya unastahili nini hapa duniani.

Mh. Profesa. Nakutakia tafakari njema. Muombe Mungu Hekima na Busara zenye utashi wa kujitegemea katika madaraka yako. Kinyume na hapo unarithi ya pilato, sauti za walala hoi, wavujajasho wa taifa hili zitakulilia hata kaburini kwako.

ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA

TRUTH IS POWER, CHANGES IS MY MISSION AND GOD IS MY LEADER.
Dogo kwanini unapenda kujiita ''mwanaharakati huru'' wakati wewe ni kada wa Chadema?Juzi Mbowe ''kakuchinjilia'' mbali uchaguzi bavicha, hakuna mtu yeyote unayempigania zaidi ya kutaka ''political mileage'' kwa tumbo lako binafsi. Jijenge kwanza kimaisha siasa zipo tu.
 
Back
Top Bottom