Waraka: Alphonce Lusako alias Emekha Ikhe kwako prof. Rwekaza Mkandala

mkuu pole sana,wewe ni kizazi cha akina nyerere,isiaka steven,mandela,gamal abel nasser,lumumba nk, ambao walijitolea kwa dhati dhidi ya africa lkn leo historia imewatupa,usiofu tupo pamoja songa mbele

mbele ndiyo huko kulikomfanya arudi nyuma.
 
Huu ndiyo wakati wa JF kuonyesha njia na kuwa sehemu ya mfano kwa masirahi ya wachache walioumizwa na wanaendelea kuumizwa na mfumo CCM, plz ndugu zangu ndani na nje ya JF tumsaidie mwezetu aweze timiza ndoto yake, moods plz anzisheni thread ya kumchangia ndugu yetu Alphonce.
 
Huu ndiyo wakati wa JF kuonyesha njia na kuwa sehemu ya mfano kwa masirahi ya wachache walioumizwa na wanaendelea kuumizwa na mfumo CCM, plz ndugu zangu ndani na nje ya JF tumsaidie mwezetu aweze timiza ndoto yake, moods plz anzisheni thread ya kumchangia ndugu yetu Alphonce.

Naunga mkono hoja kumchangia atimize ndoto yake. Pia namuombea Mabwepande impite mbali!
 
Ndugu mwakitobile nimependa ushauri wako. Namsihi kakaangu Alpphonce aache kulalama na kutafuta huruma kutoka kwa umma akidhania ataweza kushinda maisha. Aliokua anawapigania hata hawamjui wengi wameamua kujilipia wenyewe ada, wengine wameamua maisha mengine yaani mbadala wa Elimu ya chuo kikuu kwa sasa labda baadae akiwemo dada yangu aliyeamua kufanya diploma ya nursing kwanza baadae ataendelea juu zaidi. Kama kweli Alphonca anaamini katika MUNGU basi akumbuke yaliyomkuta Ayubu naye akafanya nini na mwisho wake ulikuaje, namaanisha unaweza kuptwa kilema leo kumbe unaepushiwa kifo kesho ukalalamika mwishowe unarudishwa kwenye hali yako ukafa kesho. Jipange upya kamanda. Baada ya kusema hayo namalizia kusikiliza tepu na kuangalia video ya tukio zima kama nilivyokua naripoti kwenye kituo changu cha habari kisha nitawaletea historia ya hili jambo na ushauri zaidi.
 
UPEMBUZI YAKINIFU WA HISTORIA NA UKWELI JUU YA WARAKA WA ALPHONCE LUSAKO alias EMEKHA IKHE

Hivi karibuni, Bwana Alphonce Lusako ameandika katika mtandao wa Wanabidii tuhuma kadhaa dhidi ya Profesa Rwekaza Mukandala ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo (VC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Katika tuhuma hizo, amejaribu kuonyesha ubaya na dhuluma aliyofanyiwa na huyo kiongozi wa UDSM. Kwa njia hiyo, Bw. Lusako ameeleza upande wake ya kile anachokiona yeye kuwa ni ukweli wa yaliyotokea. Kwa hiyo, na sisi wakereketwa wa ukweli wa historia ya UDSM tunapenda kueleza upande mwingine, ili wasomaji wapate fursa ya kuangalia upande mwingine wa taarifa na hatimaye kubaini ukweli.
Wenye kumbukumbu nzuri ya mambo, watakumbuka kuwa mnamo mwezi November 2011, lilianzishwa vuguvugu miongoni mwa wanafunzi wa hapo UDSM kwa lengo la kutaka wanafunzi wote wa Tanzania waliokuwa wamekosa mikopo toka Bodi ya Mikopo wapewe mikopo hiyo. Hii ilitokana na kubainika kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata udahili katika vyuo mbalimbali nchini lakini wakashindwa kupata mikopo. Kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo, wanafunzi hao hawakupata mikopo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya bajeti ya mfuko huo kuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi. Ilipofika Novemba 2011 vuguvugu hilo lilipamba moto zaidi, na ndipo Bw. Lusako akaamua kuchukua hatamu za uongozi wa harakati hizo, kama alivyokiri mwenyewe katika ujumbe wake tunaoujibu. Vuguvugu hilo lilibadilika sura na kugeuka kuwa mgomo, ujulikanao kwa jina maarufu chuoni kama KUNJI, na yeye akafanikiwa kuwapata wafuasi wake kwa mujibu wa malengo aliyoyabainisha wakati ule na kuyaeleza bayana kwenye ujumbe wake. Mgomo ule ulipoanza, ulikuwa na mwelekeo wa kuwa na sura ya kitaifa, kwa lengo la kuvihusisha vyuo vingi nchini, na kuna mengi yaliyojiri mwanzoni, kama wanahabari walivyokuwa wakiripoti kila siku. Mwanzoni, mgomo huo ulipata nguvu kwa kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa hawajapata malipo yao kwa kuwa yalichelewa. Baadaye wanafunzi wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) wakaongeza nguvu kwenye mgomo huo. Hata hivyo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza walipolipwa, wakaanza kujiengua kwenye mgomo; hawakuona sababu ya kuuendeleza baada ya kulipwa. Mgogoro huo ulizidi kubadilika sura, na baadhi yetu tutakumbuka jinsi ulivyohama toka kuwa wa nchi nzima na kuwa wa chuo kikuu kimoja tu cha Dar es Salaam (UDSM). Na hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa hata kwa UDSM haukuwa wa chuo chote, bali kundi dogo lililojitwisha jukumu la kudai haki ya waliokosa mkopo kwa kutumia njia ya kuushinikiza utawala wa chuo na hasa kuwashinikiza na kuwalazimisha wanafunzi wengine wote waunge mkono juhudi hizo. Mgogoro ulizidi kukua na siku moja kundi la vijana, wakiongozwa na Bw. Lusako, walijipanga, wakaingia barabarani wakiimba, na kuelekea jengo la Utawala, na hatimaye kutoka nnje ya mipaka ya chuo kuelekea Ikulu kupitia Ubungo. Baada ya kukataa kutii amri ya vikosi vya usalama, wanafunzi hao walikamatwa na polisi wa kutuliza ghasia. Katika kamatakamata hiyo, watu wengi walijikuta mikononi mwa polisi, akiwemo Bw. Lusako, wafuasi wake, na hata watu wengine wasiohusika na hata wasiokuwa wanafunzi. Baada ya mchujo, watu walioonekana kutokuwa na hatia waliachiwa huru. Ikumbukwe kuwa wakati wakiwa ndani ya chuo polisi hawakukamata wala kuhangaika nao hata walipovuruga madarasa na kufanya mikutano pale uwanja wa mabadiliko (Rev Square). Wafuasi wa Bw. Lusako waliosalimika kukamatwa hawakuridhika. Wakajipanga na kuanza maandamano upya ili kuwakomboa wenzao waliokamatwa. Kwa bahati mbaya, na kinyume na matarajio yao, wafuasi hao hawakuungwa mkono na wanafunzi wengi; kwa hiyo, wakajikusanya tena mbele ya jengo la Utawala wakishinikiza wenzao, akiwemo kiongozi wao Bw. Lusako, waachiwe huru bila masharti yoyote. Baada ya kukosa wafuasi wa kutosha, wakaamua kutumia njia ya mabavu, ya kuwafukuza wahadhiri na wanafunzi madarasani kwa njia ya vitisho, viboko na mawe. Katika tukio moja mhadhiri alimwagiwa maji akiwa akiwa anafundisha darasani! Wakapafanya Mlimani pasikalike kwa amani, huku wakishangilia kila walipofanikiwa kulivuruga darasa na kulitawanya. Waliokuwa Mlimani siku hizo, watakumbuka jinsi walimu na wanafunzi walivyokuwa wakikimbizwa kwa bakora wasiingie madarasani. Hapa tungependa kumuuliza Bw. Lusako atueleze uhalali wa mbinu za kundi lake za kuwacharaza viboko na kuwamwagia maji wanafunzi, maprofesa na wahadhiri waliothubutu kuingia madarasani kuendelea na masomo. Bw. Lusako atueleze kama hiyo ndiyo demokrasia, au kama huo ndio uzalendo wa kuwaadhibu wale wasiokubaliana na mawazo yake! Aweke wazi uhalali wa wanafunzi walio wengi (wenyeji na wageni), wenye mikopo na wasio na mikopo, waliotaka kuendelea na masomo lakini kundi lake likawazuia (kwa viboko, maji na mawe) kupata haki yao, wakiwa tayari wamelipa kazo zao. Je, huko ndiko kuipenda nchi "yake" (tukumbuke yeye hasemi nchi "yetu", bali ati ni nchi "yake"). Uongozi wa chuo ulijitahidi kurejesha amani chuoni. Moja ya njia zilizotumika ni pamoja na kuwezesha kuwapa dhamana wanafunzi waliokuwa mahabusu huko Segerea. Ikumbukwe kuwa, alikuwa ni VC huyo huyo anayetuhumiwa na Bw. Lusako alionesha huruma na kuamua kuruhusu Mshauri wa wanafunzi na DARUSO kuwawekea dhamana akina Lusako na wenzake. Bila huruma na ruhusa ya VC, Bw. Lusako angeendelea kusota Segerea. Baadaye, Bw. Lusako na wenzake walikutana na viongozi wa juu wa Chuo na kukubaliana mambo ya msingi ya kufanya. Vilevile walipewa taarifa kuwa utawala, ukishirikiana na DARUSO, ulishasaidia wanafunzi wengi kupata mikopo na waliokuwa wamepata kidogo walishaongezewa. Viongozi wa Chuo waliwaonesha wawakilishi hao ushahidi yakinifu wa mambo kadhaa pamoja na mikakati mingine, ambayo tunaamini Bw. Lusako anayajua na kukumbuka vyema. Bw. Lusako na wenzake walipoondoka kwenye kikao, wakabadili mawazo na kutoa taarifa tofauti kwa wenzao. Wakadai waliitwa kutulizwa tu bila kuwepo jambo la maana. Wakalaani uongozi wa chuo na wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo au kula chakula, wakati wao (akina Lusako) "wakihangaika kutafuta haki kwa watu wote". Wakafanikiwa kuwachochea zaidi wanaharakati wao na kuwapandisha jaziba wengine kadhaa. Saa moja na nusu usiku wa tarehe 12/11/2011, kundi la watu kama 200 wakajikusanya na kuelekea kafeteria wakiwa na zana za uharibifu. Njiani walikopita walivunja vioo vya magari yaliyosimama kuwapisha wapite, wakawashusha na kuwapiga abiria wa mabasi ya daladala yapitayo chuoni, bila kujali ni kina nani. Wenye magari yaliyoharibiwa na madereva wa mabasi husika ni mashahidi wa matukio hayo. Wakahitimisha walipofika kafeteria, wakamwaga mchanga kwenye chakula, wakavunja makabati ya kutunzia chipsi, wakavunja taa na meza, wakawachapa viboko wahudumu na waliokuwepo maeneo hayo, na mengine kadhaa. Hicho ndicho kikosi kazi cha kufundisha demokrasia na diplomasia, na kuleta amani na kutetea haki za wanyonge cha Mh. Bw. Lusako! Baada ya uongozi wa Chuo kupata taarifa, uliomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza la Chuo ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho kuhusu Chuo na hatima yake. Baada ya kupitia taarifa zote husika za matukio hayo, Baraza la Chuo, likatoa mwongozo kuwa wale wote walioshiriki katika sakata hilo wasimamishwe masomo, pamoja na uongozi mzima wa DARUSO wakiwemo wajumbe wa bunge la wanafunzi lililokaa kikao na kupitisha azimio la kupinga maamuzi ya Baraza la Chuo hapo awali baada ya akina Lusako na wenzake kadhaa kusimamishwa masomo. Baada ya mchakato wa kawaida wa kuchambua makosa ya waliosimamishwa masomo, wanafunzi wote waliobainika kutokuwa na hatia walirudishwa chuoni kuendelea na masomo yao. Hata wale waliokutwa na hatia, baadhi yao wakasamehewa na kuruhusiwa kurudi kuendelea na masomo (kwa masharti) kuanzia pale walipoachia, baada ya kuomba msamaha kwa Baraza la Chuo. Hata hivyo, baadhi ya wale waliokutwa na hatia, hawakuridhika na masharti waliyopewa na Chuo. Kwa hiyo, baadhi yao waliamua kufungua kesi mahakamani kudai haki zao, wakiongozwa na Mh. Bw. Lusako. Sasa inashangaza kuona mtu yuleyule aliyefungua kesi mahakamani, leo anafungua ‘kesi' nyingine kwenye ukumbi wa mitandao ya kijamii, kana kwamba haamini kama mahakama itamtendea haki! tena dhidi ya mtu na siyo taasisi. Yeye mwenyewe amekiri kuwa hataki na wala hawezi kuomba msamaha. Inaelekea ama anajichanganya kwa mambo kadhaa, au anaanza kuchanganyikiwa. Kwanza, kama ni kuomba msamaha, ataliomba kwa Baraza la Chuo, na wala siyo Makamu Mkuu wa Chuo anayemlaumu. Pili, anasahau kuwa yeye ndiye aliyepeleka kesi mahakamani, na kwa hiyo, hakustahili kuliibua suala hilo popote kabla ya mahakama kutoa hukumu. Inaelekea kuwa taratibu zote zinamchenga: za chuo na za mahakama. Ni vyema akaendelea kusubiri hukumu ya mahakama ambako amefungua kesi, hadi haki yake itakapopatikana. Katika kuonesha kuwa Prof. Mukandala ni muungwana, pamoja na mambo yote aliwakaribisha ofisini kwake kila wanapoomba iwe hivyo na kwamba ni mtu wa diplomasia Lusako anakiri alikutana na mkuu huyo tarehe 14/12/2014 akielewa kabisa walipewa barua ya kutokuonekana maeneo ya chuo. Cha kushangaza sana ni kwamba kila wanapokutana nae mkuu huyo alisema kwamba huko mjini wanamsumbua na hapendi kuonekana kama chuo kinamshinda nikinukuu "Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda" amaa! Katika hali ya kawaida wewe ukiwa kiongozi utasubiri viongozi wa juu wakuelekeze hata kuhakikisha chuo kina amani? Kikundi kidogo cha wahuni kinaleta fujo na kuhatarisha Amani ya Chuo alafu mkuu wa chuo akae kimya badala ya kukiondoa wengine wabaki katika utulivu? Eti chuo kina wenyewe nao wako mjini! Kwa mtazamo wangu haya ni maneno anayoyatumia ndugu Lusako ili apate kuonewa huruma. Hapa umetuongopea na niweke bayana tu kuwa ni uzushi mtupu. Zaidi ya hayo, Bw. Lusako ajifunze kutii sheria, kufuata kanuni na taratibu, na asiporidhika, ajifunze kupambana na mfumo au taasisi, badala ya kupambana na mtu binafsi. Ajifunze kutofautisha kati ya Prof. Mukandala, VC, Baraza la Chuo na UDSM. Bw. Lusako lazima ajifunze na kutambua kuwa mtu anapotafuta haki yake lazima ajali na kuheshimu haki za wenzake waliomzunguka. Kadhalika, kama Bw. Lusako angekuwa na uchungu wa kweli wa kuwajali watoto wa maskini waliokosa mikopo, na anaijua diplomasia kama anavyotaka ieleweke, basi angewakusanya hao hao waliokosa mikopo na wakashindwa kwenda vyuoni, na wanaokosa mlo wa kila siku, ili awasaidie kuwajengea uwezo wa kupambana na dhiki za maisha, badala ya kuwahamasisha wenzake kuleta kero na uharibifu wa mali za watu wasiokuwa na hatia. Bw. Lusako ajifunze kuheshimu haki za watu wasiokubaliana na mawazo yake. Busara alizo nazo zimuongoze kuwasheshimu hata wale wanaompinga au kwenda kinyume na matakwa yake, badala ya kuwakashfu na kuwaita mashetani. Ajue kuwa wanafunzi walioandika barua za kuomba msamaha walifanya hivyo kwa hiari na kwa maslahi yao wenyewe, baada ya kuzingatia malengo yao, kilichowaleta chuoni, na yote yaliyotokea. Je, hawana haki ya kufanya hivyo? Kwa kuwa Bw. Lusako amedokeza mengi ya kutuhumu, na sisi tumeeleza historia ya matukio, hatuoni haja ya kujibu kila hoja. Wasomaji wapime pande zote mbili na kuchambua mbichi, mbivu na hata mbovu. Pamoja na mambo mengine kadhaa, tunazo pia taarifa za baadhi ya watu kujitosa na kukiri kuwa walipewa fedha ili kuongoza mgomo huo na kuhamasisha vurugu, lakini tusingependa kuyaeleza hayo yote hapa. Inawezekana Bw. Lusako anazo sababu zake zilizomsukuma kufanya alivyofanya, na kuendelea kuandika anayoyaandika, lakini akumbuke kuwa historia ya maisha haili rushwa na wala haizikwi. Mara nyingi, kila mtu huvuna alichopanda. Ukipanda jamala utavuna heri; lakini ukipanda dhuluma utavuna uasi; ukipanda uchochezi utavuna kisasi, na ukipanda shari utavuna majuto. Kwa hiyo, Bw. Lusako atulie na kuikubali hali na ukweli wa kuvuna alichokipanda. Kama ataona mambo yamemzidia na akashindwa kujielewa, ni vyema akaomba msaada wa wataalam wa saikolojia na ushauri nasaha ili wampe mwanga wa kujitambua. Mwisho, tunapenda kuhitimisha kwa kuwakumbusha wasomaji misemo miwili ya wahenga isemayo kuwa "mfa maji haachi kutapatapa" na "penye ukweli, uwongo hujitenga". Ni sisi wakereketwa wa historia na ukweli. UDSM
 
Wakereketwa wa ukweli wa historia ya UDSM tunapenda kueleza upande mwingine, ili wasomaji wapate fursa ya kuangalia upande mwingine wa taarifa na hatimaye kubaini ukweli. Wenye kumbukumbu nzuri ya mambo, watakumbuka kuwa mnamo mwezi November 2011, lilianzishwa vuguvugu miongoni mwa wanafunzi wa hapo UDSM kwa lengo la kutaka wanafunzi wote wa Tanzania waliokuwa wamekosa mikopo toka Bodi ya Mikopo wapewe mikopo hiyo. Hii ilitokana na kubainika kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata udahili katika vyuo mbalimbali nchini lakini wakashindwa kupata mikopo. Kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo, wanafunzi hao hawakupata mikopo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya bajeti ya mfuko huo kuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi.

Ilipofika Novemba 2011 vuguvugu hilo lilipamba moto zaidi, na ndipo Bw. Lusako akaamua kuchukua hatamu za uongozi wa harakati hizo, kama alivyokiri mwenyewe katika ujumbe wake tunaoujibu. Vuguvugu hilo lilibadilika sura na kugeuka kuwa mgomo, ujulikanao kwa jina maarufu chuoni kama KUNJI, na yeye akafanikiwa kuwapata wafuasi wake kwa mujibu wa malengo aliyoyabainisha wakati ule na kuyaeleza bayana kwenye ujumbe wake.

Mgomo ule ulipoanza, ulikuwa na mwelekeo wa kuwa na sura ya kitaifa, kwa lengo la kuvihusisha vyuo vingi nchini, na kuna mengi yaliyojiri mwanzoni, kama wanahabari walivyokuwa wakiripoti kila siku. Mwanzoni, mgomo huo ulipata nguvu kwa kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa hawajapata malipo yao kwa kuwa yalichelewa. Baadaye wanafunzi wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) wakaongeza nguvu kwenye mgomo huo. Hata hivyo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza walipolipwa, wakaanza kujiengua kwenye mgomo; hawakuona sababu ya kuuendeleza baada ya kulipwa. Mgogoro huo ulizidi kubadilika sura, na baadhi yetu tutakumbuka jinsi ulivyohama toka kuwa wa nchi nzima na kuwa wa chuo kikuu kimoja tu cha Dar es Salaam (UDSM). Na hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa hata kwa UDSM haukuwa wa chuo chote, bali kundi dogo lililojitwisha jukumu la kudai haki ya waliokosa mkopo kwa kutumia njia ya kuushinikiza utawala wa chuo na hasa kuwashinikiza na kuwalazimisha wanafunzi wengine wote waunge mkono juhudi hizo.

Mgogoro ulizidi kukua na siku moja kundi la vijana, wakiongozwa na Bw. Lusako, walijipanga, wakaingia barabarani wakiimba, na kuelekea jengo la Utawala, na hatimaye kutoka nnje ya mipaka ya chuo kuelekea Ikulu kupitia Ubungo. Baada ya kukataa kutii amri ya vikosi vya usalama, wanafunzi hao walikamatwa na polisi wa kutuliza ghasia. Katika kamatakamata hiyo, watu wengi walijikuta mikononi mwa polisi, akiwemo Bw. Lusako, wafuasi wake, na hata watu wengine wasiohusika na hata wasiokuwa wanafunzi. Baada ya mchujo, watu walioonekana kutokuwa na hatia waliachiwa huru. Ikumbukwe kuwa wakati wakiwa ndani ya chuo polisi hawakukamata wala kuhangaika nao hata walipovuruga madarasa na kufanya mikutano pale uwanja wa mabadiliko (Rev Square).


Wafuasi wa Bw. Lusako waliosalimika kukamatwa hawakuridhika. Wakajipanga na kuanza maandamano upya ili kuwakomboa wenzao waliokamatwa. Kwa bahati mbaya, na kinyume na matarajio yao, wafuasi hao hawakuungwa mkono na wanafunzi wengi; kwa hiyo, wakajikusanya tena mbele ya jengo la Utawala wakishinikiza wenzao, akiwemo kiongozi wao Bw. Lusako, waachiwe huru bila masharti yoyote. Baada ya kukosa wafuasi wa kutosha, wakaamua kutumia njia ya mabavu, ya kuwafukuza wahadhiri na wanafunzi madarasani kwa njia ya vitisho, viboko na mawe. Katika tukio moja mhadhiri alimwagiwa maji akiwa akiwa anafundisha darasani! Wakapafanya Mlimani pasikalike kwa amani, huku wakishangilia kila walipofanikiwa kulivuruga darasa na kulitawanya. Waliokuwa Mlimani siku hizo, watakumbuka jinsi walimu na wanafunzi walivyokuwa wakikimbizwa kwa bakora wasiingie madarasani. Hapa tungependa kumuuliza Bw. Lusako atueleze uhalali wa mbinu za kundi lake za kuwacharaza viboko na kuwamwagia maji wanafunzi, maprofesa na wahadhiri waliothubutu kuingia madarasani kuendelea na masomo. Bw. Lusako atueleze kama hiyo ndiyo demokrasia, au kama huo ndio uzalendo wa kuwaadhibu wale wasiokubaliana na mawazo yake! Aweke wazi uhalali wa wanafunzi walio wengi (wenyeji na wageni), wenye mikopo na wasio na mikopo, waliotaka kuendelea na masomo lakini kundi lake likawazuia (kwa viboko, maji na mawe) kupata haki yao, wakiwa tayari wamelipa kazo zao. Je, huko ndiko kuipenda nchi "yake" (tukumbuke yeye hasemi nchi "yetu", bali ati ni nchi "yake").


Uongozi wa chuo ulijitahidi kurejesha amani chuoni. Moja ya njia zilizotumika ni pamoja na kuwezesha kuwapa dhamana wanafunzi waliokuwa mahabusu huko Segerea. Ikumbukwe kuwa, alikuwa ni VC huyo huyo anayetuhumiwa na Bw. Lusako alionesha huruma na kuamua kuruhusu Mshauri wa wanafunzi na DARUSO kuwawekea dhamana akina Lusako na wenzake. Bila huruma na ruhusa ya VC, Bw. Lusako angeendelea kusota Segerea.


Baadaye, Bw. Lusako na wenzake walikutana na viongozi wa juu wa Chuo na kukubaliana mambo ya msingi ya kufanya. Vilevile walipewa taarifa kuwa utawala, ukishirikiana na DARUSO, ulishasaidia wanafunzi wengi kupata mikopo na waliokuwa wamepata kidogo walishaongezewa. Viongozi wa Chuo waliwaonesha wawakilishi hao ushahidi yakinifu wa mambo kadhaa pamoja na mikakati mingine, ambayo tunaamini Bw. Lusako anayajua na kukumbuka vyema. Bw. Lusako na wenzake walipoondoka kwenye kikao, wakabadili mawazo na kutoa taarifa tofauti kwa wenzao. Wakadai waliitwa kutulizwa tu bila kuwepo jambo la maana. Wakalaani uongozi wa chuo na wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo au kula chakula, wakati wao (akina Lusako) "wakihangaika kutafuta haki kwa watu wote". Wakafanikiwa kuwachochea zaidi wanaharakati wao na kuwapandisha jaziba wengine kadhaa.

Saa moja na nusu usiku wa tarehe 12/11/2011, kundi la watu kama 200 wakajikusanya na kuelekea kafeteria wakiwa na zana za uharibifu. Njiani walikopita walivunja vioo vya magari yaliyosimama kuwapisha wapite, wakawashusha na kuwapiga abiria wa mabasi ya daladala yapitayo chuoni, bila kujali ni kina nani. Wenye magari yaliyoharibiwa na madereva wa mabasi husika ni mashahidi wa matukio hayo. Wakahitimisha walipofika kafeteria, wakamwaga mchanga kwenye chakula, wakavunja makabati ya kutunzia chipsi, wakavunja taa na meza, wakawachapa viboko wahudumu na waliokuwepo maeneo hayo, na mengine kadhaa. Hicho ndicho kikosi kazi cha kufundisha demokrasia na diplomasia, na kuleta amani na kutetea haki za wanyonge cha Mh. Bw. Lusako!

Baada ya uongozi wa Chuo kupata taarifa, uliomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza la Chuo ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho kuhusu Chuo na hatima yake. Baada ya kupitia taarifa zote husika za matukio hayo, Baraza la Chuo, likatoa mwongozo kuwa wale wote walioshiriki katika sakata hilo wasimamishwe masomo, pamoja na uongozi mzima wa DARUSO wakiwemo wajumbe wa bunge la wanafunzi lililokaa kikao na kupitisha azimio la kupinga maamuzi ya Baraza la Chuo hapo awali baada ya akina Lusako na wenzake kadhaa kusimamishwa masomo.

Baada ya mchakato wa kawaida wa kuchambua makosa ya waliosimamishwa masomo, wanafunzi wote waliobainika kutokuwa na hatia walirudishwa chuoni kuendelea na masomo yao. Hata wale waliokutwa na hatia, baadhi yao wakasamehewa na kuruhusiwa kurudi kuendelea na masomo (kwa masharti) kuanzia pale walipoachia, baada ya kuomba msamaha kwa Baraza la Chuo. Hata hivyo, baadhi ya wale waliokutwa na hatia, hawakuridhika na masharti waliyopewa na Chuo. Kwa hiyo, baadhi yao waliamua kufungua kesi mahakamani kudai haki zao, wakiongozwa na Mh. Bw. Lusako. Sasa inashangaza kuona mtu yuleyule aliyefungua kesi mahakamani, leo anafungua ‘kesi' nyingine kwenye ukumbi wa mitandao ya kijamii, kana kwamba haamini kama mahakama itamtendea haki! tena dhidi ya mtu na siyo taasisi. Yeye mwenyewe amekiri kuwa hataki na wala hawezi kuomba msamaha. Inaelekea ama anajichanganya kwa mambo kadhaa, au anaanza kuchanganyikiwa. Kwanza, kama ni kuomba msamaha, ataliomba kwa Baraza la Chuo, na wala siyo Makamu Mkuu wa Chuo anayemlaumu. Pili, anasahau kuwa yeye ndiye aliyepeleka kesi mahakamani, na kwa hiyo, hakustahili kuliibua suala hilo popote kabla ya mahakama kutoa hukumu. Inaelekea kuwa taratibu zote zinamchenga: za chuo na za mahakama. Ni vyema akaendelea kusubiri hukumu ya mahakama ambako amefungua kesi, hadi haki yake itakapopatikana.


Katika kuonesha kuwa Prof. Mukandala ni muungwana, pamoja na mambo yote aliwakaribisha ofisini kwake kila wanapoomba iwe hivyo na kwamba ni mtu wa diplomasia Lusako anakiri alikutana na mkuu huyo tarehe 14/12/2014 akielewa kabisa walipewa barua ya kutokuonekana maeneo ya chuo. Cha kushangaza sana ni kwamba kila wanapokutana nae mkuu huyo alisema kwamba huko mjini wanamsumbua na hapendi kuonekana kama chuo kinamshinda nikinukuu "Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda" amaa! Katika hali ya kawaida wewe ukiwa kiongozi utasubiri viongozi wa juu wakuelekeze hata kuhakikisha chuo kina amani? Kikundi kidogo cha wahuni kinaleta fujo na kuhatarisha Amani ya Chuo alafu mkuu wa chuo akae kimya badala ya kukiondoa wengine wabaki katika utulivu? Eti chuo kina wenyewe nao wako mjini! Kwa mtazamo wangu haya ni maneno anayoyatumia ndugu Lusako ili apate kuonewa huruma. Hapa umetuongopea na niweke bayana tu kuwa ni uzushi mtupu.

Zaidi ya hayo, Bw. Lusako ajifunze kutii sheria, kufuata kanuni na taratibu, na asiporidhika, ajifunze kupambana na mfumo au taasisi, badala ya kupambana na mtu binafsi. Ajifunze kutofautisha kati ya Prof. Mukandala, VC, Baraza la Chuo na UDSM. Bw. Lusako lazima ajifunze na kutambua kuwa mtu anapotafuta haki yake lazima ajali na kuheshimu haki za wenzake waliomzunguka. Kadhalika, kama Bw. Lusako angekuwa na uchungu wa kweli wa kuwajali watoto wa maskini waliokosa mikopo, na anaijua diplomasia kama anavyotaka ieleweke, basi angewakusanya hao hao waliokosa mikopo na wakashindwa kwenda vyuoni, na wanaokosa mlo wa kila siku, ili awasaidie kuwajengea uwezo wa kupambana na dhiki za maisha, badala ya kuwahamasisha wenzake kuleta kero na uharibifu wa mali za watu wasiokuwa na hatia. Bw. Lusako ajifunze kuheshimu haki za watu wasiokubaliana na mawazo yake. Busara alizo nazo zimuongoze kuwasheshimu hata wale wanaompinga au kwenda kinyume na matakwa yake, badala ya kuwakashfu na kuwaita mashetani. Ajue kuwa wanafunzi walioandika barua za kuomba msamaha walifanya hivyo kwa hiari na kwa maslahi yao wenyewe, baada ya kuzingatia malengo yao, kilichowaleta chuoni, na yote yaliyotokea. Je, hawana haki ya kufanya hivyo?

Kwa kuwa Bw. Lusako amedokeza mengi ya kutuhumu, na sisi tumeeleza historia ya matukio, hatuoni haja ya kujibu kila hoja. Wasomaji wapime pande zote mbili na kuchambua mbichi, mbivu na hata mbovu. Pamoja na mambo mengine kadhaa, tunazo pia taarifa za baadhi ya watu kujitosa na kukiri kuwa walipewa fedha ili kuongoza mgomo huo na kuhamasisha vurugu, lakini tusingependa kuyaeleza hayo yote hapa.


Inawezekana Bw. Lusako anazo sababu zake zilizomsukuma kufanya alivyofanya, na kuendelea kuandika anayoyaandika, lakini akumbuke kuwa historia ya maisha haili rushwa na wala haizikwi. Mara nyingi, kila mtu huvuna alichopanda. Ukipanda jamala utavuna heri; lakini ukipanda dhuluma utavuna uasi; ukipanda uchochezi utavuna kisasi, na ukipanda shari utavuna majuto. Kwa hiyo, Bw. Lusako atulie na kuikubali hali na ukweli wa kuvuna alichokipanda. Kama ataona mambo yamemzidia na akashindwa kujielewa, ni vyema akaomba msaada wa wataalam wa saikolojia na ushauri nasaha ili wampe mwanga wa kujitambua. Mwisho, tunapenda kuhitimisha kwa kuwakumbusha wasomaji misemo miwili ya wahenga isemayo kuwa "mfa maji haachi kutapatapa" na "penye ukweli, uwongo hujitenga".

Ni sisi wakereketwa wa historia na ukweli.
UDSM
 
Wakereketwa wa ukweli wa historia ya UDSM tunapenda kueleza upande mwingine, ili wasomaji wapate fursa ya kuangalia upande mwingine wa taarifa na hatimaye kubaini ukweli. Wenye kumbukumbu nzuri ya mambo, watakumbuka kuwa mnamo mwezi November 2011, lilianzishwa vuguvugu miongoni mwa wanafunzi wa hapo UDSM kwa lengo la kutaka wanafunzi wote wa Tanzania waliokuwa wamekosa mikopo toka Bodi ya Mikopo wapewe mikopo hiyo. Hii ilitokana na kubainika kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata udahili katika vyuo mbalimbali nchini lakini wakashindwa kupata mikopo. Kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo, wanafunzi hao hawakupata mikopo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya bajeti ya mfuko huo kuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi. Ilipofika Novemba 2011 vuguvugu hilo lilipamba moto zaidi, na ndipo Bw. Lusako akaamua kuchukua hatamu za uongozi wa harakati hizo, kama alivyokiri mwenyewe katika ujumbe wake tunaoujibu. Vuguvugu hilo lilibadilika sura na kugeuka kuwa mgomo, ujulikanao kwa jina maarufu chuoni kama KUNJI, na yeye akafanikiwa kuwapata wafuasi wake kwa mujibu wa malengo aliyoyabainisha wakati ule na kuyaeleza bayana kwenye ujumbe wake. Mgomo ule ulipoanza, ulikuwa na mwelekeo wa kuwa na sura ya kitaifa, kwa lengo la kuvihusisha vyuo vingi nchini, na kuna mengi yaliyojiri mwanzoni, kama wanahabari walivyokuwa wakiripoti kila siku. Mwanzoni, mgomo huo ulipata nguvu kwa kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa hawajapata malipo yao kwa kuwa yalichelewa. Baadaye wanafunzi wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) wakaongeza nguvu kwenye mgomo huo. Hata hivyo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza walipolipwa, wakaanza kujiengua kwenye mgomo; hawakuona sababu ya kuuendeleza baada ya kulipwa. Mgogoro huo ulizidi kubadilika sura, na baadhi yetu tutakumbuka jinsi ulivyohama toka kuwa wa nchi nzima na kuwa wa chuo kikuu kimoja tu cha Dar es Salaam (UDSM). Na hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa hata kwa UDSM haukuwa wa chuo chote, bali kundi dogo lililojitwisha jukumu la kudai haki ya waliokosa mkopo kwa kutumia njia ya kuushinikiza utawala wa chuo na hasa kuwashinikiza na kuwalazimisha wanafunzi wengine wote waunge mkono juhudi hizo. Mgogoro ulizidi kukua na siku moja kundi la vijana, wakiongozwa na Bw. Lusako, walijipanga, wakaingia barabarani wakiimba, na kuelekea jengo la Utawala, na hatimaye kutoka nnje ya mipaka ya chuo kuelekea Ikulu kupitia Ubungo. Baada ya kukataa kutii amri ya vikosi vya usalama, wanafunzi hao walikamatwa na polisi wa kutuliza ghasia. Katika kamatakamata hiyo, watu wengi walijikuta mikononi mwa polisi, akiwemo Bw. Lusako, wafuasi wake, na hata watu wengine wasiohusika na hata wasiokuwa wanafunzi. Baada ya mchujo, watu walioonekana kutokuwa na hatia waliachiwa huru. Ikumbukwe kuwa wakati wakiwa ndani ya chuo polisi hawakukamata wala kuhangaika nao hata walipovuruga madarasa na kufanya mikutano pale uwanja wa mabadiliko (Rev Square). Wafuasi wa Bw. Lusako waliosalimika kukamatwa hawakuridhika. Wakajipanga na kuanza maandamano upya ili kuwakomboa wenzao waliokamatwa. Kwa bahati mbaya, na kinyume na matarajio yao, wafuasi hao hawakuungwa mkono na wanafunzi wengi; kwa hiyo, wakajikusanya tena mbele ya jengo la Utawala wakishinikiza wenzao, akiwemo kiongozi wao Bw. Lusako, waachiwe huru bila masharti yoyote. Baada ya kukosa wafuasi wa kutosha, wakaamua kutumia njia ya mabavu, ya kuwafukuza wahadhiri na wanafunzi madarasani kwa njia ya vitisho, viboko na mawe. Katika tukio moja mhadhiri alimwagiwa maji akiwa akiwa anafundisha darasani! Wakapafanya Mlimani pasikalike kwa amani, huku wakishangilia kila walipofanikiwa kulivuruga darasa na kulitawanya. Waliokuwa Mlimani siku hizo, watakumbuka jinsi walimu na wanafunzi walivyokuwa wakikimbizwa kwa bakora wasiingie madarasani. Hapa tungependa kumuuliza Bw. Lusako atueleze uhalali wa mbinu za kundi lake za kuwacharaza viboko na kuwamwagia maji wanafunzi, maprofesa na wahadhiri waliothubutu kuingia madarasani kuendelea na masomo. Bw. Lusako atueleze kama hiyo ndiyo demokrasia, au kama huo ndio uzalendo wa kuwaadhibu wale wasiokubaliana na mawazo yake! Aweke wazi uhalali wa wanafunzi walio wengi (wenyeji na wageni), wenye mikopo na wasio na mikopo, waliotaka kuendelea na masomo lakini kundi lake likawazuia (kwa viboko, maji na mawe) kupata haki yao, wakiwa tayari wamelipa kazo zao. Je, huko ndiko kuipenda nchi “yake” (tukumbuke yeye hasemi nchi “yetu”, bali ati ni nchi “yake”). Uongozi wa chuo ulijitahidi kurejesha amani chuoni. Moja ya njia zilizotumika ni pamoja na kuwezesha kuwapa dhamana wanafunzi waliokuwa mahabusu huko Segerea. Ikumbukwe kuwa, alikuwa ni VC huyo huyo anayetuhumiwa na Bw. Lusako alionesha huruma na kuamua kuruhusu Mshauri wa wanafunzi na DARUSO kuwawekea dhamana akina Lusako na wenzake. Bila huruma na ruhusa ya VC, Bw. Lusako angeendelea kusota Segerea. Baadaye, Bw. Lusako na wenzake walikutana na viongozi wa juu wa Chuo na kukubaliana mambo ya msingi ya kufanya. Vilevile walipewa taarifa kuwa utawala, ukishirikiana na DARUSO, ulishasaidia wanafunzi wengi kupata mikopo na waliokuwa wamepata kidogo walishaongezewa. Viongozi wa Chuo waliwaonesha wawakilishi hao ushahidi yakinifu wa mambo kadhaa pamoja na mikakati mingine, ambayo tunaamini Bw. Lusako anayajua na kukumbuka vyema. Bw. Lusako na wenzake walipoondoka kwenye kikao, wakabadili mawazo na kutoa taarifa tofauti kwa wenzao. Wakadai waliitwa kutulizwa tu bila kuwepo jambo la maana. Wakalaani uongozi wa chuo na wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo au kula chakula, wakati wao (akina Lusako) “wakihangaika kutafuta haki kwa watu wote”. Wakafanikiwa kuwachochea zaidi wanaharakati wao na kuwapandisha jaziba wengine kadhaa. Saa moja na nusu usiku wa tarehe 12/11/2011, kundi la watu kama 200 wakajikusanya na kuelekea kafeteria wakiwa na zana za uharibifu. Njiani walikopita walivunja vioo vya magari yaliyosimama kuwapisha wapite, wakawashusha na kuwapiga abiria wa mabasi ya daladala yapitayo chuoni, bila kujali ni kina nani. Wenye magari yaliyoharibiwa na madereva wa mabasi husika ni mashahidi wa matukio hayo. Wakahitimisha walipofika kafeteria, wakamwaga mchanga kwenye chakula, wakavunja makabati ya kutunzia chipsi, wakavunja taa na meza, wakawachapa viboko wahudumu na waliokuwepo maeneo hayo, na mengine kadhaa. Hicho ndicho kikosi kazi cha kufundisha demokrasia na diplomasia, na kuleta amani na kutetea haki za wanyonge cha Mh. Bw. Lusako! Baada ya uongozi wa Chuo kupata taarifa, uliomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza la Chuo ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho kuhusu Chuo na hatima yake. Baada ya kupitia taarifa zote husika za matukio hayo, Baraza la Chuo, likatoa mwongozo kuwa wale wote walioshiriki katika sakata hilo wasimamishwe masomo, pamoja na uongozi mzima wa DARUSO wakiwemo wajumbe wa bunge la wanafunzi lililokaa kikao na kupitisha azimio la kupinga maamuzi ya Baraza la Chuo hapo awali baada ya akina Lusako na wenzake kadhaa kusimamishwa masomo. Baada ya mchakato wa kawaida wa kuchambua makosa ya waliosimamishwa masomo, wanafunzi wote waliobainika kutokuwa na hatia walirudishwa chuoni kuendelea na masomo yao. Hata wale waliokutwa na hatia, baadhi yao wakasamehewa na kuruhusiwa kurudi kuendelea na masomo (kwa masharti) kuanzia pale walipoachia, baada ya kuomba msamaha kwa Baraza la Chuo. Hata hivyo, baadhi ya wale waliokutwa na hatia, hawakuridhika na masharti waliyopewa na Chuo. Kwa hiyo, baadhi yao waliamua kufungua kesi mahakamani kudai haki zao, wakiongozwa na Mh. Bw. Lusako. Sasa inashangaza kuona mtu yuleyule aliyefungua kesi mahakamani, leo anafungua ‘kesi’ nyingine kwenye ukumbi wa mitandao ya kijamii, kana kwamba haamini kama mahakama itamtendea haki! tena dhidi ya mtu na siyo taasisi. Yeye mwenyewe amekiri kuwa hataki na wala hawezi kuomba msamaha. Inaelekea ama anajichanganya kwa mambo kadhaa, au anaanza kuchanganyikiwa. Kwanza, kama ni kuomba msamaha, ataliomba kwa Baraza la Chuo, na wala siyo Makamu Mkuu wa Chuo anayemlaumu. Pili, anasahau kuwa yeye ndiye aliyepeleka kesi mahakamani, na kwa hiyo, hakustahili kuliibua suala hilo popote kabla ya mahakama kutoa hukumu. Inaelekea kuwa taratibu zote zinamchenga: za chuo na za mahakama. Ni vyema akaendelea kusubiri hukumu ya mahakama ambako amefungua kesi, hadi haki yake itakapopatikana. Katika kuonesha kuwa Prof. Mukandala ni muungwana, pamoja na mambo yote aliwakaribisha ofisini kwake kila wanapoomba iwe hivyo na kwamba ni mtu wa diplomasia Lusako anakiri alikutana na mkuu huyo tarehe 14/12/2014 akielewa kabisa walipewa barua ya kutokuonekana maeneo ya chuo. Cha kushangaza sana ni kwamba kila wanapokutana nae mkuu huyo alisema kwamba huko mjini wanamsumbua na hapendi kuonekana kama chuo kinamshinda nikinukuu “Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda” amaa! Katika hali ya kawaida wewe ukiwa kiongozi utasubiri viongozi wa juu wakuelekeze hata kuhakikisha chuo kina amani? Kikundi kidogo cha wahuni kinaleta fujo na kuhatarisha Amani ya Chuo alafu mkuu wa chuo akae kimya badala ya kukiondoa wengine wabaki katika utulivu? Eti chuo kina wenyewe nao wako mjini! Kwa mtazamo wangu haya ni maneno anayoyatumia ndugu Lusako ili apate kuonewa huruma. Hapa umetuongopea na niweke bayana tu kuwa ni uzushi mtupu. Zaidi ya hayo, Bw. Lusako ajifunze kutii sheria, kufuata kanuni na taratibu, na asiporidhika, ajifunze kupambana na mfumo au taasisi, badala ya kupambana na mtu binafsi. Ajifunze kutofautisha kati ya Prof. Mukandala, VC, Baraza la Chuo na UDSM. Bw. Lusako lazima ajifunze na kutambua kuwa mtu anapotafuta haki yake lazima ajali na kuheshimu haki za wenzake waliomzunguka. Kadhalika, kama Bw. Lusako angekuwa na uchungu wa kweli wa kuwajali watoto wa maskini waliokosa mikopo, na anaijua diplomasia kama anavyotaka ieleweke, basi angewakusanya hao hao waliokosa mikopo na wakashindwa kwenda vyuoni, na wanaokosa mlo wa kila siku, ili awasaidie kuwajengea uwezo wa kupambana na dhiki za maisha, badala ya kuwahamasisha wenzake kuleta kero na uharibifu wa mali za watu wasiokuwa na hatia. Bw. Lusako ajifunze kuheshimu haki za watu wasiokubaliana na mawazo yake. Busara alizo nazo zimuongoze kuwasheshimu hata wale wanaompinga au kwenda kinyume na matakwa yake, badala ya kuwakashfu na kuwaita mashetani. Ajue kuwa wanafunzi walioandika barua za kuomba msamaha walifanya hivyo kwa hiari na kwa maslahi yao wenyewe, baada ya kuzingatia malengo yao, kilichowaleta chuoni, na yote yaliyotokea. Je, hawana haki ya kufanya hivyo? Kwa kuwa Bw. Lusako amedokeza mengi ya kutuhumu, na sisi tumeeleza historia ya matukio, hatuoni haja ya kujibu kila hoja. Wasomaji wapime pande zote mbili na kuchambua mbichi, mbivu na hata mbovu. Pamoja na mambo mengine kadhaa, tunazo pia taarifa za baadhi ya watu kujitosa na kukiri kuwa walipewa fedha ili kuongoza mgomo huo na kuhamasisha vurugu, lakini tusingependa kuyaeleza hayo yote hapa. Inawezekana Bw. Lusako anazo sababu zake zilizomsukuma kufanya alivyofanya, na kuendelea kuandika anayoyaandika, lakini akumbuke kuwa historia ya maisha haili rushwa na wala haizikwi. Mara nyingi, kila mtu huvuna alichopanda. Ukipanda jamala utavuna heri; lakini ukipanda dhuluma utavuna uasi; ukipanda uchochezi utavuna kisasi, na ukipanda shari utavuna majuto. Kwa hiyo, Bw. Lusako atulie na kuikubali hali na ukweli wa kuvuna alichokipanda. Kama ataona mambo yamemzidia na akashindwa kujielewa, ni vyema akaomba msaada wa wataalam wa saikolojia na ushauri nasaha ili wampe mwanga wa kujitambua. Mwisho, tunapenda kuhitimisha kwa kuwakumbusha wasomaji misemo miwili ya wahenga isemayo kuwa “mfa maji haachi kutapatapa” na “penye ukweli, uwongo hujitenga”. Ni sisi wakereketwa wa historia na ukweli. UDSM
 
kwa nyie mnaosema akarudi chuo chochote tz, walifungwa kwenda kusoma chuo chochote cha tz,
 
2ko pamoja ndugu yangu..ni kweli udsm imebadilitka., uhuru na fikra za wasomi wa chuo kikongwe nchin upo ndan ya mifuko ya watu wachache... Mpaka leo kuna 1st year hawaelewi unaposema REVO SQUARE unamaanisha nini
 
Prof madesa hao hawajitambui,haina misimamo,bendera fuata upepo. Aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.
 
Wakereketwa wa ukweli wa historia ya UDSM tunapenda kueleza upande mwingine, ili wasomaji wapate fursa ya kuangalia upande mwingine wa taarifa na hatimaye kubaini ukweli. Wenye kumbukumbu nzuri ya mambo, watakumbuka kuwa mnamo mwezi November 2011, lilianzishwa vuguvugu miongoni mwa wanafunzi wa hapo UDSM kwa lengo la kutaka wanafunzi wote wa Tanzania waliokuwa wamekosa mikopo toka Bodi ya Mikopo wapewe mikopo hiyo. Hii ilitokana na kubainika kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata udahili katika vyuo mbalimbali nchini lakini wakashindwa kupata mikopo. Kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo, wanafunzi hao hawakupata mikopo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya bajeti ya mfuko huo kuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi. Ilipofika Novemba 2011 vuguvugu hilo lilipamba moto zaidi, na ndipo Bw. Lusako akaamua kuchukua hatamu za uongozi wa harakati hizo, kama alivyokiri mwenyewe katika ujumbe wake tunaoujibu. Vuguvugu hilo lilibadilika sura na kugeuka kuwa mgomo, ujulikanao kwa jina maarufu chuoni kama KUNJI, na yeye akafanikiwa kuwapata wafuasi wake kwa mujibu wa malengo aliyoyabainisha wakati ule na kuyaeleza bayana kwenye ujumbe wake. Mgomo ule ulipoanza, ulikuwa na mwelekeo wa kuwa na sura ya kitaifa, kwa lengo la kuvihusisha vyuo vingi nchini, na kuna mengi yaliyojiri mwanzoni, kama wanahabari walivyokuwa wakiripoti kila siku. Mwanzoni, mgomo huo ulipata nguvu kwa kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa hawajapata malipo yao kwa kuwa yalichelewa. Baadaye wanafunzi wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) wakaongeza nguvu kwenye mgomo huo. Hata hivyo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza walipolipwa, wakaanza kujiengua kwenye mgomo; hawakuona sababu ya kuuendeleza baada ya kulipwa. Mgogoro huo ulizidi kubadilika sura, na baadhi yetu tutakumbuka jinsi ulivyohama toka kuwa wa nchi nzima na kuwa wa chuo kikuu kimoja tu cha Dar es Salaam (UDSM). Na hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa hata kwa UDSM haukuwa wa chuo chote, bali kundi dogo lililojitwisha jukumu la kudai haki ya waliokosa mkopo kwa kutumia njia ya kuushinikiza utawala wa chuo na hasa kuwashinikiza na kuwalazimisha wanafunzi wengine wote waunge mkono juhudi hizo. Mgogoro ulizidi kukua na siku moja kundi la vijana, wakiongozwa na Bw. Lusako, walijipanga, wakaingia barabarani wakiimba, na kuelekea jengo la Utawala, na hatimaye kutoka nnje ya mipaka ya chuo kuelekea Ikulu kupitia Ubungo. Baada ya kukataa kutii amri ya vikosi vya usalama, wanafunzi hao walikamatwa na polisi wa kutuliza ghasia. Katika kamatakamata hiyo, watu wengi walijikuta mikononi mwa polisi, akiwemo Bw. Lusako, wafuasi wake, na hata watu wengine wasiohusika na hata wasiokuwa wanafunzi. Baada ya mchujo, watu walioonekana kutokuwa na hatia waliachiwa huru. Ikumbukwe kuwa wakati wakiwa ndani ya chuo polisi hawakukamata wala kuhangaika nao hata walipovuruga madarasa na kufanya mikutano pale uwanja wa mabadiliko (Rev Square). Wafuasi wa Bw. Lusako waliosalimika kukamatwa hawakuridhika. Wakajipanga na kuanza maandamano upya ili kuwakomboa wenzao waliokamatwa. Kwa bahati mbaya, na kinyume na matarajio yao, wafuasi hao hawakuungwa mkono na wanafunzi wengi; kwa hiyo, wakajikusanya tena mbele ya jengo la Utawala wakishinikiza wenzao, akiwemo kiongozi wao Bw. Lusako, waachiwe huru bila masharti yoyote. Baada ya kukosa wafuasi wa kutosha, wakaamua kutumia njia ya mabavu, ya kuwafukuza wahadhiri na wanafunzi madarasani kwa njia ya vitisho, viboko na mawe. Katika tukio moja mhadhiri alimwagiwa maji akiwa akiwa anafundisha darasani! Wakapafanya Mlimani pasikalike kwa amani, huku wakishangilia kila walipofanikiwa kulivuruga darasa na kulitawanya. Waliokuwa Mlimani siku hizo, watakumbuka jinsi walimu na wanafunzi walivyokuwa wakikimbizwa kwa bakora wasiingie madarasani. Hapa tungependa kumuuliza Bw. Lusako atueleze uhalali wa mbinu za kundi lake za kuwacharaza viboko na kuwamwagia maji wanafunzi, maprofesa na wahadhiri waliothubutu kuingia madarasani kuendelea na masomo. Bw. Lusako atueleze kama hiyo ndiyo demokrasia, au kama huo ndio uzalendo wa kuwaadhibu wale wasiokubaliana na mawazo yake! Aweke wazi uhalali wa wanafunzi walio wengi (wenyeji na wageni), wenye mikopo na wasio na mikopo, waliotaka kuendelea na masomo lakini kundi lake likawazuia (kwa viboko, maji na mawe) kupata haki yao, wakiwa tayari wamelipa kazo zao. Je, huko ndiko kuipenda nchi "yake" (tukumbuke yeye hasemi nchi "yetu", bali ati ni nchi "yake"). Uongozi wa chuo ulijitahidi kurejesha amani chuoni. Moja ya njia zilizotumika ni pamoja na kuwezesha kuwapa dhamana wanafunzi waliokuwa mahabusu huko Segerea. Ikumbukwe kuwa, alikuwa ni VC huyo huyo anayetuhumiwa na Bw. Lusako alionesha huruma na kuamua kuruhusu Mshauri wa wanafunzi na DARUSO kuwawekea dhamana akina Lusako na wenzake. Bila huruma na ruhusa ya VC, Bw. Lusako angeendelea kusota Segerea. Baadaye, Bw. Lusako na wenzake walikutana na viongozi wa juu wa Chuo na kukubaliana mambo ya msingi ya kufanya. Vilevile walipewa taarifa kuwa utawala, ukishirikiana na DARUSO, ulishasaidia wanafunzi wengi kupata mikopo na waliokuwa wamepata kidogo walishaongezewa. Viongozi wa Chuo waliwaonesha wawakilishi hao ushahidi yakinifu wa mambo kadhaa pamoja na mikakati mingine, ambayo tunaamini Bw. Lusako anayajua na kukumbuka vyema. Bw. Lusako na wenzake walipoondoka kwenye kikao, wakabadili mawazo na kutoa taarifa tofauti kwa wenzao. Wakadai waliitwa kutulizwa tu bila kuwepo jambo la maana. Wakalaani uongozi wa chuo na wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo au kula chakula, wakati wao (akina Lusako) "wakihangaika kutafuta haki kwa watu wote". Wakafanikiwa kuwachochea zaidi wanaharakati wao na kuwapandisha jaziba wengine kadhaa. Saa moja na nusu usiku wa tarehe 12/11/2011, kundi la watu kama 200 wakajikusanya na kuelekea kafeteria wakiwa na zana za uharibifu. Njiani walikopita walivunja vioo vya magari yaliyosimama kuwapisha wapite, wakawashusha na kuwapiga abiria wa mabasi ya daladala yapitayo chuoni, bila kujali ni kina nani. Wenye magari yaliyoharibiwa na madereva wa mabasi husika ni mashahidi wa matukio hayo. Wakahitimisha walipofika kafeteria, wakamwaga mchanga kwenye chakula, wakavunja makabati ya kutunzia chipsi, wakavunja taa na meza, wakawachapa viboko wahudumu na waliokuwepo maeneo hayo, na mengine kadhaa. Hicho ndicho kikosi kazi cha kufundisha demokrasia na diplomasia, na kuleta amani na kutetea haki za wanyonge cha Mh. Bw. Lusako! Baada ya uongozi wa Chuo kupata taarifa, uliomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza la Chuo ambalo ndilo lenye maamuzi ya mwisho kuhusu Chuo na hatima yake. Baada ya kupitia taarifa zote husika za matukio hayo, Baraza la Chuo, likatoa mwongozo kuwa wale wote walioshiriki katika sakata hilo wasimamishwe masomo, pamoja na uongozi mzima wa DARUSO wakiwemo wajumbe wa bunge la wanafunzi lililokaa kikao na kupitisha azimio la kupinga maamuzi ya Baraza la Chuo hapo awali baada ya akina Lusako na wenzake kadhaa kusimamishwa masomo. Baada ya mchakato wa kawaida wa kuchambua makosa ya waliosimamishwa masomo, wanafunzi wote waliobainika kutokuwa na hatia walirudishwa chuoni kuendelea na masomo yao. Hata wale waliokutwa na hatia, baadhi yao wakasamehewa na kuruhusiwa kurudi kuendelea na masomo (kwa masharti) kuanzia pale walipoachia, baada ya kuomba msamaha kwa Baraza la Chuo. Hata hivyo, baadhi ya wale waliokutwa na hatia, hawakuridhika na masharti waliyopewa na Chuo. Kwa hiyo, baadhi yao waliamua kufungua kesi mahakamani kudai haki zao, wakiongozwa na Mh. Bw. Lusako. Sasa inashangaza kuona mtu yuleyule aliyefungua kesi mahakamani, leo anafungua ‘kesi' nyingine kwenye ukumbi wa mitandao ya kijamii, kana kwamba haamini kama mahakama itamtendea haki! tena dhidi ya mtu na siyo taasisi. Yeye mwenyewe amekiri kuwa hataki na wala hawezi kuomba msamaha. Inaelekea ama anajichanganya kwa mambo kadhaa, au anaanza kuchanganyikiwa. Kwanza, kama ni kuomba msamaha, ataliomba kwa Baraza la Chuo, na wala siyo Makamu Mkuu wa Chuo anayemlaumu. Pili, anasahau kuwa yeye ndiye aliyepeleka kesi mahakamani, na kwa hiyo, hakustahili kuliibua suala hilo popote kabla ya mahakama kutoa hukumu. Inaelekea kuwa taratibu zote zinamchenga: za chuo na za mahakama. Ni vyema akaendelea kusubiri hukumu ya mahakama ambako amefungua kesi, hadi haki yake itakapopatikana. Katika kuonesha kuwa Prof. Mukandala ni muungwana, pamoja na mambo yote aliwakaribisha ofisini kwake kila wanapoomba iwe hivyo na kwamba ni mtu wa diplomasia Lusako anakiri alikutana na mkuu huyo tarehe 14/12/2014 akielewa kabisa walipewa barua ya kutokuonekana maeneo ya chuo. Cha kushangaza sana ni kwamba kila wanapokutana nae mkuu huyo alisema kwamba huko mjini wanamsumbua na hapendi kuonekana kama chuo kinamshinda nikinukuu "Nafahamu mnapigania haki zenu za msingi lakini mjini wananisumbua, hiki chuo si chuo changu, chuo hiki kina wenyewe na wenyewe wako mjini, wananiambia kuwa nimeshindwa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam na mimi siwezi kukubali kuwa chuo kimenishinda" amaa! Katika hali ya kawaida wewe ukiwa kiongozi utasubiri viongozi wa juu wakuelekeze hata kuhakikisha chuo kina amani? Kikundi kidogo cha wahuni kinaleta fujo na kuhatarisha Amani ya Chuo alafu mkuu wa chuo akae kimya badala ya kukiondoa wengine wabaki katika utulivu? Eti chuo kina wenyewe nao wako mjini! Kwa mtazamo wangu haya ni maneno anayoyatumia ndugu Lusako ili apate kuonewa huruma. Hapa umetuongopea na niweke bayana tu kuwa ni uzushi mtupu. Zaidi ya hayo, Bw. Lusako ajifunze kutii sheria, kufuata kanuni na taratibu, na asiporidhika, ajifunze kupambana na mfumo au taasisi, badala ya kupambana na mtu binafsi. Ajifunze kutofautisha kati ya Prof. Mukandala, VC, Baraza la Chuo na UDSM. Bw. Lusako lazima ajifunze na kutambua kuwa mtu anapotafuta haki yake lazima ajali na kuheshimu haki za wenzake waliomzunguka. Kadhalika, kama Bw. Lusako angekuwa na uchungu wa kweli wa kuwajali watoto wa maskini waliokosa mikopo, na anaijua diplomasia kama anavyotaka ieleweke, basi angewakusanya hao hao waliokosa mikopo na wakashindwa kwenda vyuoni, na wanaokosa mlo wa kila siku, ili awasaidie kuwajengea uwezo wa kupambana na dhiki za maisha, badala ya kuwahamasisha wenzake kuleta kero na uharibifu wa mali za watu wasiokuwa na hatia. Bw. Lusako ajifunze kuheshimu haki za watu wasiokubaliana na mawazo yake. Busara alizo nazo zimuongoze kuwasheshimu hata wale wanaompinga au kwenda kinyume na matakwa yake, badala ya kuwakashfu na kuwaita mashetani. Ajue kuwa wanafunzi walioandika barua za kuomba msamaha walifanya hivyo kwa hiari na kwa maslahi yao wenyewe, baada ya kuzingatia malengo yao, kilichowaleta chuoni, na yote yaliyotokea. Je, hawana haki ya kufanya hivyo? Kwa kuwa Bw. Lusako amedokeza mengi ya kutuhumu, na sisi tumeeleza historia ya matukio, hatuoni haja ya kujibu kila hoja. Wasomaji wapime pande zote mbili na kuchambua mbichi, mbivu na hata mbovu. Pamoja na mambo mengine kadhaa, tunazo pia taarifa za baadhi ya watu kujitosa na kukiri kuwa walipewa fedha ili kuongoza mgomo huo na kuhamasisha vurugu, lakini tusingependa kuyaeleza hayo yote hapa. Inawezekana Bw. Lusako anazo sababu zake zilizomsukuma kufanya alivyofanya, na kuendelea kuandika anayoyaandika, lakini akumbuke kuwa historia ya maisha haili rushwa na wala haizikwi. Mara nyingi, kila mtu huvuna alichopanda. Ukipanda jamala utavuna heri; lakini ukipanda dhuluma utavuna uasi; ukipanda uchochezi utavuna kisasi, na ukipanda shari utavuna majuto. Kwa hiyo, Bw. Lusako atulie na kuikubali hali na ukweli wa kuvuna alichokipanda. Kama ataona mambo yamemzidia na akashindwa kujielewa, ni vyema akaomba msaada wa wataalam wa saikolojia na ushauri nasaha ili wampe mwanga wa kujitambua. Mwisho, tunapenda kuhitimisha kwa kuwakumbusha wasomaji misemo miwili ya wahenga isemayo kuwa "mfa maji haachi kutapatapa" na "penye ukweli, uwongo hujitenga". Ni sisi wakereketwa wa historia na ukweli. UDSM

Hii aina ya uandishi inaitwa Kanyaga Twende!
 
Ushauri wa mwisho kwa Ndugu Alphonce na wenzie waliofukuzwa vyuoni.

1. Kwa kuwa nimona unatumia sana vifungu vya vitabu vitakatifu (BIBILIA) basi kumbuka hadithi ya mwana mpotevu. Nadhani kuna umuhimu wa kujifikiria upya hasa namna ya kuomba kurudi chuoni. Maswala ya kutumia social media au kuita press conference ni kupoteza muda na pesa au kuhangaika pasipo manufaa. Baada ya kutoka kwenye press conference yenu jana niliomba mtoa taarifa wangu pale Muhimbili anipatie copy ya University Charter niliipitia kwa umakini nikimshirikisha mtaalamu wa sheria ambae niliamini yuko balance, nikagundua kuwa baada ya baraza la chuo kutoa maamuzi wa kupinga ni mahakama tu na si mamlaka nyingine.

2. Kuna kitu kinitwa kuhofia kuonekana una hofu. Kuomba msamaha mnataka (in indirect ways) lakini kwenye mtandao mnatukana hauwezi kuomba msamaha sasa huyo rais atasaidia nini? Kisingizio cha kwamba nyie ni watanzania mnaotamani elimu mnadhani nani atawasikiliza wakati mmeshamwaga matusi mengi humu JF? Pia unadhani nyie ni wengi kuliko 4m 4 wa mwaka jana waliopata 0? Nyie mnonekana kama tone tu ndani ya Bahari! hasa mnapotumia siasa kuomba msamaha. Mara nyingi mmekua mkisema humu na kwingineko kuwa si lazima usome chuo kikuu ndiyo upate maisha hasa pale rev square na utawala mnapowatukana wanachuo na wale wasiowaunga mkono, jana mnasema mnataabika mtaani na hakuna chuo kinachowakubali, hata private? Je nnje ya nchi mlipokuwa mkiwaambia wenzenu na wengine mkipata promise za kupata ajira au kupewa jimbo mwaka ujao wa uchaguzi? Jamani tusijidanganye au kudanganya wengine, Ulikuja mwenyewe na begi lako utarudi na begi lako ukiwa na disco au gamba/cheti/degree. Acheni uoga wa kuonesha kuwa mmesononeka sana kwa kufukuzwa kwenu kaeni chi mpange mikakati hata ya kuwatumia wazazi wenu wawaombe msamaha yaishe. Elimu nzuri jama hasa ya chuo kikuu
 
Ushauri wa mwisho kwa Ndugu Alphonce na wenzie waliofukuzwa vyuoni.

1. Kwa kuwa nimona unatumia sana vifungu vya vitabu vitakatifu (BIBILIA) basi kumbuka hadithi ya mwana mpotevu. Nadhani kuna umuhimu wa kujifikiria upya hasa namna ya kuomba kurudi chuoni. Maswala ya kutumia social media au kuita press conference ni kupoteza muda na pesa au kuhangaika pasipo manufaa. Baada ya kutoka kwenye press conference yenu jana niliomba mtoa taarifa wangu pale Muhimbili anipatie copy ya University Charter niliipitia kwa umakini nikimshirikisha mtaalamu wa sheria ambae niliamini yuko balance, nikagundua kuwa baada ya baraza la chuo kutoa maamuzi wa kupinga ni mahakama tu na si mamlaka nyingine.

2. Kuna kitu kinitwa kuhofia kuonekana una hofu. Kuomba msamaha mnataka (in indirect ways) lakini kwenye mtandao mnatukana hauwezi kuomba msamaha sasa huyo rais atasaidia nini? Kisingizio cha kwamba nyie ni watanzania mnaotamani elimu mnadhani nani atawasikiliza wakati mmeshamwaga matusi mengi humu JF? Pia unadhani nyie ni wengi kuliko 4m 4 wa mwaka jana waliopata 0? Nyie mnonekana kama tone tu ndani ya Bahari! hasa mnapotumia siasa kuomba msamaha. Mara nyingi mmekua mkisema humu na kwingineko kuwa si lazima usome chuo kikuu ndiyo upate maisha hasa pale rev square na utawala mnapowatukana wanachuo na wale wasiowaunga mkono, jana mnasema mnataabika mtaani na hakuna chuo kinachowakubali, hata private? Je nnje ya nchi mlipokuwa mkiwaambia wenzenu na wengine mkipata promise za kupata ajira au kupewa jimbo mwaka ujao wa uchaguzi? Jamani tusijidanganye au kudanganya wengine, Ulikuja mwenyewe na begi lako utarudi na begi lako ukiwa na disco au gamba/cheti/degree. Acheni uoga wa kuonesha kuwa mmesononeka sana kwa kufukuzwa kwenu kaeni chi mpange mikakati hata ya kuwatumia wazazi wenu wawaombe msamaha yaishe. Elimu nzuri jama hasa ya chuo kikuu
 
Sijui nahuyu ataongezwa kwenye list ya Wanyakyusa wa kuondolewa? ..............Kibona,Mwaikambo,Mwaikusa,Mwakyembe, Mwangosi, Mwandosya, Kibanda....and now Lusako......wataweza kweli kuwamaliza?
 
mmmh sasa bwana lusako mbona unaonekana kama mpenda sifa na anaetaka awe shujaa muda wowote anapoonekana mbele za watu,sasa kulikua na haja gani ya wewe kuendelea na malumbano mara baada ya kutoka segerea??je we ukuona wanafunzi uliokua ukiwatetea walikusaliti? Sasa ivi uko wap?ila ucjari maisha ni zaidi ya udsm na chuo kikuu kiujumla!
 
Ushauri wa mwisho kwa Ndugu Alphonce na wenzie waliofukuzwa vyuoni.

1. Kwa kuwa nimona unatumia sana vifungu vya vitabu vitakatifu (BIBILIA) basi kumbuka hadithi ya mwana mpotevu. Nadhani kuna umuhimu wa kujifikiria upya hasa namna ya kuomba kurudi chuoni. Maswala ya kutumia social media au kuita press conference ni kupoteza muda na pesa au kuhangaika pasipo manufaa. Baada ya kutoka kwenye press conference yenu jana niliomba mtoa taarifa wangu pale Muhimbili anipatie copy ya University Charter niliipitia kwa umakini nikimshirikisha mtaalamu wa sheria ambae niliamini yuko balance, nikagundua kuwa baada ya baraza la chuo kutoa maamuzi wa kupinga ni mahakama tu na si mamlaka nyingine.

2. Kuna kitu kinitwa kuhofia kuonekana una hofu. Kuomba msamaha mnataka (in indirect ways) lakini kwenye mtandao mnatukana hauwezi kuomba msamaha sasa huyo rais atasaidia nini? Kisingizio cha kwamba nyie ni watanzania mnaotamani elimu mnadhani nani atawasikiliza wakati mmeshamwaga matusi mengi humu JF? Pia unadhani nyie ni wengi kuliko 4m 4 wa mwaka jana waliopata 0? Nyie mnonekana kama tone tu ndani ya Bahari! hasa mnapotumia siasa kuomba msamaha. Mara nyingi mmekua mkisema humu na kwingineko kuwa si lazima usome chuo kikuu ndiyo upate maisha hasa pale rev square na utawala mnapowatukana wanachuo na wale wasiowaunga mkono, jana mnasema mnataabika mtaani na hakuna chuo kinachowakubali, hata private? Je nnje ya nchi mlipokuwa mkiwaambia wenzenu na wengine mkipata promise za kupata ajira au kupewa jimbo mwaka ujao wa uchaguzi? Jamani tusijidanganye au kudanganya wengine, Ulikuja mwenyewe na begi lako utarudi na begi lako ukiwa na disco au gamba/cheti/degree. Acheni uoga wa kuonesha kuwa mmesononeka sana kwa kufukuzwa kwenu kaeni chi mpange mikakati hata ya kuwatumia wazazi wenu wawaombe msamaha yaishe. Elimu nzuri jama hasa ya chuo kikuu

amwombe msamaha nani? Yaani kupaza sauti na kukemea UJINGA ndo dhambi? We gamba kweli damu.
 
Pole sana mkuu ila kilio chenu ni kilio cha watanznia wote na mungu atajitu kilio cha wanyonge
 
NIWAKUMBUSHE TU KUWA VITA BAINA YA DHULUMA NA HAKI, MARA ZOTE HAKI HUSIMAMA.
Kwenu mjiitao wakereketwa wa UDSM.
Taarifa potofu si njema sana ndugu zangu.
Niseme tu, mda wenu wa kuwalaghai watanzania umekwisha. Kwa mda mrefu watawala wa vyuo vikuu mumekuwa watetezi wa dhuluma kinyume na haki mnayoiongea midomoni mwenu, mnayo iandika kwenye vitabu vyenu lakini hamuiishi mioyoni mwenu.
Watawala wa UDSM hawakwepi lawama ya kuwa ni Kiini cha matatizo yaliyotokea udsm. Kwani wao ndio waliohusika kupeleka taarifa potofu katika baraza la chuo na baraza la chuo lilisimamia taarifa potofu walozozitoa watawala kuhukumu wanafunzi..
wanafunzi wote walikamatwa ndani ya chuo"UDSM"na wengine kukamatwa wakiwa wamekuja kutuwekea mdhamana kituo cha polisi OSTERBAY. Wanafunzi wote 51, hawakurudishwa na watawala ila walirudishwa baada ya haki kushinda dhuluma katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mnamo tar. 30 Augost 2012. Ambapo wanafunzi wa udsm, tuliposhinda kesi zidi ya jamhuri.
Sasa kuwadanganya watanzania kuwa wanafunzi wakiwa ndani ya chuo, polisi hawakukamata wala kuhangaika nao hata walipovuruga madarasa na kufanya mikutano pale uwanja wa mabadiliko (Rev Square). Ni uongo Na kama umetumwa kawaambie wawe wakweli wanapotuma taarifa hizi.
Kawaambieni watawala waliowatuma kwamba tunaposema "mgomo au maandamano ya wanafunzi"hatumaanishi wengine wasome na wengine wagome. Tunamaanisha wanafunzi wote waungane ili kudai madai ya msingi. Suala hapa ni madai aina gani?, kama ni madai ya msingi wanafunzi wote hawana budi kuunga mkono. Atayeonekana haungi mkono suala la msingi na lenye maslahi mema na watanzania walioonewa, ni wajibu wa msomi yeyote anayejitambua kumkumbusha msomi mwenzake kwa njia za kidiplomasia, zikishindikana njia za kidiplomasia, binafsi naunga mkono njia za kutumia nguvu yani kuwalazimisha wasiogoma au wasioandamana kugoma au kuandamana kwa maslahi ya walioonewa ndani ya nchi yetu. Nadhani ndio kitu kilichotokea UDSM, baadhi ya wanafunzi walikerwa na wanafunzi wanaojifanya hawajui uonezi wanaofanyiowa wenzao ndio maana ikafika sehemu wakaanza kutishiana wao kwa wao. Lakini waeleze watawala wa UDSM kuwa VYUO VIKUU NI SEHEMU PEKEE YA KUUAUBINAFSI, NA KUFUNDISHANA MIOYO YA KUPIGANIA HAKI ZA WALIOONEWA HATA KAMA WEWE HUJAONEWA.
Halafu tuliosimama kuongoza maandamano yenye maslahi na wavujajasho wa taifa hili hatukuwahi kupiga mtu, kushawishi mtu au kumtuma mtu apige mwanafunzi mwenzake. Na nafikiri ni upuuzi kumshawishi mwanafunzi mwenzio kwa viboko na kwanini na yeye akubali kushawishiwa kwa viboko, eti kwa kum-mwagia maji mhadhiri wetu na kwa nini mhadhiri wetu amwagiwe maji. Jibu ninalopata hapa ni kwamba huenda mliwatuma vibaraka wenu wafanye vurugu ili kuharibu nia yetu ya dhati na kukamilisha mliyoyafanya.
Lakini pia kama mlishindwa kuithibitishia mahakama juu ya uharifu mliotusingizia, mnataka muwathibitishie watu kwa maandishi kama mlivyotoa taarifa potofu mbele ya vyombo vya habari tarehe 13/12/2014?
Lakini pia kama kunawafuasi wangu ambao mnasema walipiga vioo magari, wakamwaga mchanga kwenye chakula, wakavunja makabati ya kutunzia chipsi, wakavunja taa na meza, wakawachapa viboko wahudumu na waliokuwepo maeneo hayo,waliwapiga wanafunzi wenzao, na mnasema mashahidi mnao.
mnataka mnihakikishie kuwa ndani ya chuo hakuna usalama, hakuna polisi maana mpaka leo sijaona mfuasi wangu ambaye alikamatwa kwa tuhuma mlizotoa. Na ndio maana naamini kuwa mliwatuma watu wenu kufanya vurugu ili muvuruge nia yetu ya dhati. Na hii ni michezo ambayo hata wahuni wachache wa hii nchi wanaifanya zidi ya vyama pinzani.
Ivi kweli wadau inawaingia akilini, yani Lusako na wafuasi wake ni watukutu, wamefukuzwa chuo halafu jopo la Uongozi wa DARUSO zaidi ya 97% ya wabunge waidhinishe mgomo wa kututaka turudi. Inamaana na wao ni vichaa, wavutabangi, hawajui walifanyalo?. mumekosa hoja. Ukweli utasimama tu nendeni kwa watoto wa shule ya msingi mnaweza mkawadanganya na nahisi na wao wanaweza kuwahoji na kushtukia dhuluma mlizokwisha fanya.
Niseme tu dawa yenu ipo jikoni, inachemka. Kogo za maneno ya hapa na pale na misemo mbali mbali,havina tija. Ila mufahamu nanyi mtavuna mlicho panda. Mtalipwa kwa kiasi mlichotenda.
NI WAKATI AMBAO TUTALIKOMBOA TAIFA KUPITIA MATESO NA UONEZI MLIOTUFANYIA, MNAOENDELEA KUTUFANYIA. HATUNA SHIDA SANA NA NINYI KWA SABABU NI WATU WACHACHE SANA NA WEPESI SANA MBELE YA HAKI. UWEPO WENU NI UWEPOTOSHA WA MABADILIKO NDANI YA NCHI HII.
NADHANI HAMUAMINI KWAMBA MABADILIKO YANAKUJA, HAMUAMINIKWAMBA MMETUTESA VYA KUTOSHA, HAMUAMINI KWAMBA KIHAMA CHENU KIMEWADIA. SUBIRINI TU.
HATUPAMBANI KWA NYAMA TU, TUNAPAMBANA KWA MAOMBI,AKILI NYINGI NA KUSAMBAZA SUMU ZA MABADILIKO YA KIFIKRA KWA WATANZANIA.
Naamini

 
katika mapambano yoyote nilazima utambue kuwa kuna sacrifce. hakuna mapambano for justice ambayo hayana kafara. nimejitoa kwa watu nahitaji kuwa sadaka ya watu. hivyo i don mind. sikusimama kwa ajili ya watu fulani wanichangie. nilisimama kwa kua nilitambua kilio cha wavujajasho wa Taifa langu.
 
comrade; education is not about graduating. life is perfomance. education is abt mind liberation. i will never acuse my self for what i did. and it is better for me to face expulsion than to knil down before injustice people. na unaposema kuna haja gani ya malumbano, nikuulize kitu kulikuwa na haja gani ya watawala wa udsm, kuendeleza malumbano kwenye vyombo vya habari na kutoa taarifa za uongo kwenye media?
 
Back
Top Bottom