Wapinga nauli ya treni ya 700 na 800/=

Nh vizri wakaainisha umbali kwani ikiwa abiria wa Buguluni,vingunguti,Tabata watatozwa kiasi hicho cha nauli usafiri huo tayari umeshapata upizani na hautaendelea na bado msongamano utaendelea na kuzidi
 
Ccm kwanini wanawaza kuiba kwenye kili mradi kwa kuwanyonya wananchi?.....
 
Bila kuambiwa umbali ni ngumu kusema kama nauli ni kubwa ama la...naona tumeshakuwa wapinzani wa kila kitu...How can we judge fares without references to distances?

Mkuu, kwa waliopata bahati ya kwenda duniani watakushuhudia kwamba ili mradi unaitwa usafiri wa ndani ya mji, nauli huwa haitokani na umbali wa vituo. Nauli huwa ni moja tu.

Hata kwa TZ, hilo lilikuwepo enzi za UDA na baadaye enzi za Mhe. Mwaibula ambaye ndiye aliyeleta ustaarabu wa daladala kufuata njia walizopangiwa tu.

Kama lengo lao lilikuwa ni kuondoa foleni na kuongeza ufanisi na uzalishaji maeneo ya kazi kwa kuwapunguzia wa-Tz uchovu, usumbufu na muda mwingi wa kusafiri kwenda na kutoka kazini, basi nilitegemea nauli iwe hata chini ya Tshs. 300 ya sasa inayotozwa na daladala.

Lakini kama hilo halikuwa lengo lao, ila kufidia hela inayopotea kwa kushindwa kusafirisha mizigo na abiria mikoani basi kwa nauli hiyo ya Tsh. 700/800, hata hivyo haitoweza. Kwa sababu hawatapata abiria walalahoi maskini wa Dar ambao jioni utawahurumia wanavyokanyaga miguu umbali mrefu kurudi majumbani kwao.
 
bora tuendelee kubanana kwenye dala dala.hizo treni wapande vibopa wa wizarani ili tupunguze gharama za mafuta ya VX



Kimsingi hata hiyo 400/ hadi 500/= inayotangazwa na serikali bado ni kubwa. Kwa treni tunapaswa kulipa 200/= hadi 300/= vinginevyo haitakuwa na maana.
 
Bei pia ni muhimu iwe chini kwa ajili ya kuvutia watumiaji, ili wasikwee daladala. Na hakuna cha kusbsidise kwa kutumia kodi, ndo mwanya wa ufisadi. Lazma treni ijiendeshe!
 
Uendeshaji wa matreni yale sidhani kama yatategemea nauli yetu kujiendesha !!ina maana serikali haitaweka pesa zake kabisa??ili kusaidia nauli kuwa chini??kwa nauli ya 800 ni ngumu sana
 
Kama tunataka kurudi kwenye ujamaa wa ku-fix price hapo sawa lakini bado naamini bei ya usafiri kigezo kikubwa ni umbali na gharama.kama mtu anafanya biashara au ana jambo la muhimu la kufanya hata hii 800 ni nauli reasonable.Tupunguze movements zisizoongeza chochote kwenye uzalishaji.
 
tAFADHALI FAFANUA KUHUSU HII NAULI INAKUWAJE?? NIKUANZIA WAPI HADI WAPI?? KAMA HUWEZI FAFANUA NAHISI UMETUMWA ULETE MADA HII ILI WATU TUPIMWE TUMELICHUKILIAJE HILI SWALA....
 
Bei pia ni muhimu iwe chini kwa ajili ya kuvutia watumiaji, ili wasikwee daladala. Na hakuna cha kusbsidise kwa kutumia kodi, ndo mwanya wa ufisadi. Lazma treni ijiendeshe!

Je iwapo tukiambiwa ili treni ijiendeshe yenyewe nauli inatakiwa sh.1000 tutafanyaje, kama issue ya ruzuku unaipinga.
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Bei pia ni muhimu iwe chini kwa ajili ya kuvutia watumiaji, ili wasikwee daladala. Na hakuna cha kusbsidise kwa kutumia kodi, ndo mwanya wa ufisadi. Lazma treni ijiendeshe!

Ni HUDUMA ; MBONA UNAPANDA BODA BODA ? NI SHILLINGI NGAPI?
 
Tuchangie tuinue uchumi kwa kizazi kijacho;

Ukilipa fedha hiyo;
Tutapata vichwa vipya
mabehewa mapya
Mishaharaha na gharama za uendeshaji na utaalamu

Siwezi changia wkti najua ni wizi huo serikali gharama ya vitu vyake zinakuwaga cheap coz kuna fidia serikali inaweka kutoka kwenye kodi zetu,sasa wakinikamua namna hiyo sasa ni lini nitafaidika na kodi ninayokatwa kila mwezi?
 
Sitaki kuamini kuwa juhudi zote zilizofanywa na dr. mwakyembe matokeo yake ni kuwaumiza wakazi wa jiji la dsm.
 
Bila kuambiwa umbali ni ngumu kusema kama nauli ni kubwa ama la...naona tumeshakuwa wapinzani wa kila kitu...How can we judge fares without references to distances?

Yaani wewe ndo umefikiri. Inaweza kuwa 700 au 800 kwa siku nzima kwa maana ukishakata ticket
we unasafiri tu kwa sku nzima. Tusiwe tunapinga bila maelezo yanayojitosheleza. Uliyeleta mada hebu jaribu kueleza vizuri ueleweke.
 
Ni HUDUMA ; MBONA UNAPANDA BODA BODA ? NI SHILLINGI NGAPI?

Tatizo la wabongo hata wangeambiwa nauli 50 wangelalamika na kutaka iwe bure kabisa tumesahau ya pantoni? Mpaka Magufuli kawakomalia tunadhani maendeleo yanaletwa na malaika au ndo iandikwe ndani nauli kwa msaada wa watu wa mare...au jap... Sisi bwana!
 
waeleze sababu makini za gharama ya nauli kama hiyo rasivyo waache maana hali za wananchi wenyewe mbaya. kwa walivyosema hivyo hata watu wa daladala wataongeza nauli.

Nadhani alieleta uzi aliandika kabla ya kuangalia habari zilizojiri katika vyombo vya habari vya jana (jumamosi), ni kwamba kwa train ya Ubungo nauli ni 400 na wanafunzi au watoto 150 na ile ya TAZARA ni sh.500 na wanafunzi sh.150.
 
wangeanza na miatatu ili badae wapandishage,wakati watu wameshazoea..
 
Back
Top Bottom