Wapi Shukrani Zangu Ziende?

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,515
6,489
House girl ndie anaepika chakula changu, ndie anafua nguo zangu na kupasi, kwa kifupi anafanya karibu kila kitu hata iwe weekend(isipokuwa tendo la ndoa). Watu huku nje wananipongeza kuwa baada ya kuoa napendeza/mtanashati na ninanawili(ila hali inakoenda inabidi nifanye mazoezi). Sasa jamani hongera za haya mabadiliko mazuri nimshukuru nani kati ya mke na house girl (hata kama nitashukuru kimoyomoyo vile)
 
Hata zamani za mfalme suleman walikuwa wanaoa
mke na mtumwa wake,
inaonyesha haya mambo yalikuwepo,
but, weka mazingira mazuri kwanza.
 
Jipe mwenyewe...
Pesa ya chakula unatoa wewe...ya kumlipa dada wa kazi unatoa wewe...nguo unanunua wewe...so sifa zote jipe mwenyewe!!
Ungejua ungeajiri dada wa kazi kitambo!!
 
Huo mtazamo sio mzuri kabisa... For iko too Conclusive... Msichana wa kazi anapokuwepo nyumbani ni kweli aweza fanya kazi zoote But anaemsimamia huyo binti ni Mkeo. Yeye ndo atamfundisha kupika vizuri, jinsi ya kufua na kunyosha na shughuli nyingi hapo ndani... Mke anawajibu mkubwa saana kwa mumewe BUT kumbuka kua sio mtumwa wako, na mara nyingi akina dada/mama wengi wamekua wakiishughulisha hivo inakua ngumu kufanya hayo majukumu mwenyewe... Hivo basi kupost ulopost unamvunjia heshima Mkeo na ni dalili ya kusema wataka kulala na House girl... Unless otherwise Mkeo ndo mmoja ya wale watu wavivu wakutupwa ....
 
Ushauri wa bure: mkeo mtengenezee mazingira ya kuwa mbali na nyumbani kama miezi 3 hivi. Ubaki na wanao na hgeli. Afu uone kama utathubutu kumtamani huyo hgeli. Ndio utagundua hata ambavyo mkeo unamuona mkali na msemaji sana ana umuhimu wake! Mtalishwa hadi inzi!
 
Mkeo tu, usitafute loopholes za kijinga!
Kwajni mkeo ni mtumwa wako au mwenza wako?
Ndio maana mumeweka msaidizi ili mkifika kitandani mcheze mkiwa na nguvu sawa!
 
shukrani ya nn???we jishukuru tu mwenyewe kwa kua na bahati ya kuhudumiwa na wa2 2!
 
Hata tendo la ndoa anza kumpa yeye

Ahsante

Hahahahahah lol! amlipe kwa vitendo...Haya G lakini hili linaweza kuleta mpasuko mkubwa sana kwenye ndoa maana jamaa anaweza kunogewa akachonga mzinga :):) (EOM)
 
Mpe mwenyezi mungu kwa kukujalia uwezo wakuweza kubadilisha mboga mpaka ukawa na shavu kama dodo,pili mpe mzazi wako tatu mkeo mfanya kazi unampa shukrani kila anapokupa kitu....
 
Huo mtazamo sio mzuri kabisa... For iko too Conclusive... Msichana wa kazi anapokuwepo nyumbani ni kweli aweza fanya kazi zoote But anaemsimamia huyo binti ni Mkeo. Yeye ndo atamfundisha kupika vizuri, jinsi ya kufua na kunyosha na shughuli nyingi hapo ndani... Mke anawajibu mkubwa saana kwa mumewe BUT kumbuka kua sio mtumwa wako, na mara nyingi akina dada/mama wengi wamekua wakiishughulisha hivo inakua ngumu kufanya hayo majukumu mwenyewe... Hivo basi kupost ulopost unamvunjia heshima Mkeo na ni dalili ya kusema wataka kulala na House girl... Unless otherwise Mkeo ndo mmoja ya wale watu wavivu wakutupwa ....
Malengo ya hii post na matarajio si mazuri jamaa anatafuta support ili afanye ushenzi fulani!!!!!!!!!!!!!!! Mhs mkeo ndiye mwalimu wa house girl wako, bila yeye hakuna zuri litafanyika unless na house girl ana malengo yake pia!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mungu wangu!!, kwa kiasi kikubwa nimeishia kusengenywa, hata hivyo napokea msimamo wa kila mmoja halafu nachanganya na zangu. Mke wangu atabakia kuwa mke na heshima tele, ila tusiwe wanafiki house girl wanafanya kazi na wanastahili kupongezwa hata kimoyomoyo.
 
Huo mtazamo sio mzuri kabisa... For iko too Conclusive... Msichana wa kazi anapokuwepo nyumbani ni kweli aweza fanya kazi zoote But anaemsimamia huyo binti ni Mkeo. Yeye ndo atamfundisha kupika vizuri, jinsi ya kufua na kunyosha na shughuli nyingi hapo ndani... Mke anawajibu mkubwa saana kwa mumewe BUT kumbuka kua sio mtumwa wako, na mara nyingi akina dada/mama wengi wamekua wakiishughulisha hivo inakua ngumu kufanya hayo majukumu mwenyewe... Hivo basi kupost ulopost unamvunjia heshima Mkeo na ni dalili ya kusema wataka kulala na House girl... Unless otherwise Mkeo ndo mmoja ya wale watu wavivu wakutupwa ....

Hapo kwenye red; hapana sio hivyo ndugu
 
Mpe tu huyo housegal wako mana umemsifia sana lol.....

Penye ukweli tusilete unafiki, chukua hatua tafadhali. Tunajua nanyi mna kazi, lakini angalau siku moja moja unaonyesha kuwa hujasahau. Uasili usife. Hiki nilichokiandika nimekiona hata kwa watu wengine, hakitokea kwa mtu mmoja tu kama mimi.
 
Ushauri wa bure: mkeo mtengenezee mazingira ya kuwa mbali na nyumbani kama miezi 3 hivi. Ubaki na wanao na hgeli. Afu uone kama utathubutu kumtamani huyo hgeli. Ndio utagundua hata ambavyo mkeo unamuona mkali na msemaji sana ana umuhimu wake! Mtalishwa hadi inzi!
Mnakuwa wagumu sana kuelewa hili somo,...yaaani kila kitu afanye housegirl halafu bado mnajifanya nyie ndio muhimu sana kiasi kwamba mkitoka kutaonekana ombwe,...anyway mimi somo nililojifunza ni kwamba tukoelekea mahausigel wengi watawachukulia wanaume wenu kwa mtindo huu
 
Penye ukweli tusilete unafiki, chukua hatua tafadhali. Tunajua nanyi mna kazi, lakini angalau siku moja moja unaonyesha kuwa hujasahau. Uasili usife. Hiki nilichokiandika nimekiona hata kwa watu wengine, hakitokea kwa mtu mmoja tu kama mimi.
Well said mkuu,......hapo h/girl ni wa kupongezwa hata kama watarusha mawe kwa hasira.
 
Back
Top Bottom