Wapi anapatikana Daktari Mzuri wa Watoto?

ikigijo

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
1,821
1,874
Wadau wa afya habari? Poleni na Majukumu.

Nimekuwa namuuguza mtoto wangu Takriba wiki 3 sasa juzi tuu kamaliza Matibabu akisumbuliwa na Kifua,

Mtoto ana Miezi 6.
Anapumua kwa shida yaani Anakoroma akiwa amelala na unaona anavyohangaika Kupumua Mbavu zake.

Wiki ya 3 Sasa,
Amekuwa akitumia dawa ila Improvement ni kidogo na dozi amemaliza tangu juzi,

Nilimpeleka Furaha Hospital Mbweni Teta.

Natafakari wapi nitapata Daktari Mzuri wa watoto?

Unaweza Kuta haiitaji madawa tena labda ni ushauri na Vitu vingine vya Kumfanyia i just imagine tu.

Natanguliza Shukrani wadau
 
Unaweza kunicheki nikuulize maswali kidogo ? Mimi sio daktari wala sina nia ya kufanya biashara yoyote tu nia nikutaka kukupa muongozo
 
Ana homa z mara kwa mara!? Kama ndio weka tatu.

Kwenye shingo ukimshika unaona kuna kama tonses zisizomuumiza!? Kam ndio weka 3

Anakohoa!? Ana muda gani!? Kama zaid ya wiki 3 weka tatu!

Anapungua uzito!? Kama anapungua weka 3 kama haongezeki wala hapungui weka 1.

Andika jumla hapa uliyopat hapa nkwambie kama sio nimonia itakuwa nn
 
Ana homa z mara kwa mara!? Kama ndio weka tatu.
Kwenye shingo ukimshika unaona kuna kama tonses zisizomuumiza!? Kam ndio weka 3
Anakohoa!? Ana muda gani!? Kama zaid ya wiki 3 weka tatu!
Anapungua uzito!? Kama anapungua weka 3 kama haongezeki wala hapungui weka 1.
Andika jumla hapa uliyopat hapa nkwambie kama sio nimonia itakuwa nn
😂😂😂😂😂😂😂😂
Taaluma ya afya siku hizi imekuwa rahisi sana-
Madaktari siku hizi hamfanyi tena phycical examination.. No inspection, no palpation, no purcussion, no auscultation..
Ni mwendo wa lab diagnosis na antibiotics tu!
 
Nenda kwa Dr Kundi ana dili na watoto tu mimi mwangu alikuwa na Athuma ya ngozi upumuaji wake ulikuwa wa shida sana amemsaidia ushari aliotupa na matibabu yupo Tabata Mangumi uliza tu Dr Kundi utapelekwa
 
Nenda Aghakan kama mfuko unaruhusu. Nilipata shida ya mtoto kama hiyo bahati nzuri alikuwa na miaka 1 na miezi 2.

Walikuta ni kilimi(sikumbuki kitaalamu) ila alikuwa anapata shida ya kupumua usku hasa akilala na homa za mara kwa mara. Walimfanyia operation ndogo akapona.

Tatizo ulikuwa ukimpa dawa ya kikohozi na kifua anapata nafuu baada ya mda tatizo linarudi.

Baada ya kukiondoa ,shida ikaisha.

Nenda utapata ufumbuzi wa haraka.
 
Nendeni Muhimbili au Agakhan mtoto apate chest X-ray.

Nashukuru kwa Ushauri.

Naomba Majina ya Madaktari wanaopatikana Muhimbili au Aga Khan wa watoto?

Je hawapatikani hospital nyingine?

Naona Kama Muhimbili Beuracracy sana mpaka upate matibabu!

Cha Muhimu jina la daktari wa watoto
 
Nenda Aghakan kama mfuko unaruhusu. Nilipata shida ya mtoto kama hiyo bahati nzuri alikuwa na miaka 1 na miezi 2. Walikuta ni kilimi(sikumbuki kitaalamu)...
Natumia NHIF.

Naomba jina la Daktari naweza kumtafuta hospital nyingine
 
Nenda kwa Dr Kundi ana dili na watoto tu mimi mwangu alikuwa na Athuma ya ngozi upumuaji wake ulikuwa wa shida sana amemsaidia ushari aliotupa na matibabu yupo Tabata Mangumi uliza tu Dr Kundi utapelekwa

Je Ilikuwa lini?
Mtoto alipona au imetulia hiyo Athma ya ngozi?
Baridi ikianza je?
 
Ana homa z mara kwa mara!? Kama ndio weka tatu.
Kwenye shingo ukimshika unaona kuna kama tonses zisizomuumiza!? Kam ndio weka 3...
Tonsils alikuwa nazo amepata matibabu nadhani amepona sina hakika sababu alipewa antibiotics....but tonsils zinawezasababisha kupata shida ya Kupumua?

Hakohoi, wiki 3, hapungui uzito ameongezeka.
 
Nenda Aghakan kama mfuko unaruhusu. Nilipata shida ya mtoto kama hiyo bahati nzuri alikuwa na miaka 1 na miezi 2. Walikuta ni kilimi(sikumbuki kitaalamu) ila alikuwa anapata shida ya kupumua usku hasa akilala na homa za mara kwa mara. Walimfanyia operation ndogo akapona.
Tatizo ulikuwa ukimpa dawa ya kikohozi na kifua anapata nafuu baada ya mda tatizo linarudi.
Baada ya kukiondoa ,shida ikaisha.
Nenda utapata ufumbuzi wa haraka.
Ulitumia Gharama kiasi gani mkuu?
 
Mkuu, nakushauri nenda hospitali ya rufaa ya serikali(MNH,Mloganzila), ikishindikana huko ndio uanze kuhangaika na sehemu zingine.

Otherwise huko kwingine watu wanachojali ni wameingiza chao first, then mgonjwa second.

Unforgettable
 
Mkuu ni Siri sana Huwezi Sema hapa kwa faida ya wengine pia?
Mi niko Open
Sio siri ila naona kuna mtu kama amenisaidia ila nilichokuwa nataka kukuambia mtu amenisaidia hapo chini kuelezea ...
Muhimu kujaribu kuelezea dalili zote alizokuwa nazo huyo mtoto pale unapokwenda hospitali ili apate matibabu sahihi
 
Back
Top Bottom