Anaruditena
Member
- Apr 29, 2010
- 51
- 4
Wanachama wote wa CCM ambao ni wapenzi wa dhati kweli kweli - wa chama cha wakulima na wafanyakazi, cha misingi ya Azimio la Arusha, basi October 31, ni kuchagua Chadema ili tupate nafasi ya kurudisha chama chetu toka mikononi mwa mafisadi wachache- chama kimetekwa nyara na watu wachache wenye pesa.
Mwakani tuanze mchakato wa kupata Mwenyekiti na katibu safi na uongozi kwa jumla na sio uongozi wa familia mbili ( JK na Makamba) na tuanze kujenga chama chetu na ifikapo 2015 mafisadi wote nje ya chama.
Tukubali matoke kwa faida ya chama chetu CCM, ama sivyo hali yetu ya mbeleni itakuwa mbaya sana - kama KANU. Watanzania wengi wamekuwa waelewa ya hatima ya maisha yao; weekend hii nimeongea na ndugu walio kijijini sana na hata Dr. Slaa hajafika huko lakini wanasema watachagua Dr. Slaa kama raisi wao. Mimi nimeshakata tamaa kwa mwelekeo unavyokwenda.