Wapendwa wetu wahanga.....

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
455
Mbagala yalilipuka,likasemwa ile mbaya,
Bahati yamekumbuka,waseme tena ubaya,
kila lake kuibuka,wamwite baba ubaya,
Wapendwa wetu wahanga,subira si yetu haki,

Waziri naye raisi,zao hoja kama toto,
eti kwao si rahisi,kuliona kama moto,
chunguzi zao rahisi,vichwa kutowaka moto,
Wapendwa wetu wahanga,subira si yetu haki,

misri wameyaona,libia ya jana pia,
ageria kumenyana,yalianza tunisia,
kwetu tutakuja pona,wapo tutaililia,
Wapendwa wetu wahanga,subira si yetu haki,

Pole zangu marehemu,lopoteza zao nyumba,
Haki yake marehemu,kamwe haitajayumba,
Hata wetu mwalimu,likiacha kimeyumba,
Wapendwa wetu wahanga,subira si yetu haki,

Machozi sasa yatoka,jasho nalo li usoni,
Uchungu haujatoka,nazidi kuwa maskini,
Nyumba nayo imetoka,chama kisicho makini,
Wapendwa wetu wahanga,subira si yetu haki,

Mbagala walinyonywa,wajanja wote wakala,
tume nyingi zikaundwa,muafaka umelala,
gongo mboto zitaundwa,wale kuku ha kulala,
wapendwa wetu wahanga,subira si yetu haki,
 
kama huna lako hoja,hapa sio taarabu,
kuleta vyako vioja,sisiemu ni tarabu,
hata wao ni vioja, wao si wastarabu,
Siku yao ikifika,wote tutaandamana,
 
ooh! Shairi zuri sana la kufariji na kuelekeza nini cha kufanya wakati huu wa msiba. Lakini limekaa kisiasa zaidi, kwa nini usilipeleke kule?
 
ooh! Shairi zuri sana la kufariji na kuelekeza nini cha kufanya wakati huu wa msiba. Lakini limekaa kisiasa zaidi, kwa nini usilipeleke kule?

Mkuu na machungu sana na nchi yangu sema hamna jinsi.....Let them sleep in peace....
 
Ahsante Mkuu,
Utunzi mzuri, Ujumbe Murua, unatia moyo......Marhabaa!

Ningeshauri upeleke kule kwenye ukumbi wa Lugha
 
Ahsante Mkuu,
Utunzi mzuri, Ujumbe Murua, unatia moyo......Marhabaa!

Ningeshauri upeleke kule kwenye ukumbi wa Lugha

Ni kwa ajili ya wapendwa wetu wahanga ndugu yangu, tun awapenda na wametutoka...nadhani hapa itasomwa na watu wengi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom