[FONT=century
gothic]KAMATI ya Vijana Wapenda Amani Tanzania (VIWATA) keshokutwa
itawasilisha maombi kwa Mwanasheria Mkuu, ya kupinga kesi aliyofunguliwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).[/FONT]
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, Katibu wa kamati hiyo, Said Mwaipopo, alisema wamechukua
uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa kesi hiyo imefunguliwa na
wanaharakati hao kwa utashi wa kisiasa zaidi na haitowaletea Watanzania
mapinduzi wanayoyataka.
Sisi vijana wapenda amani na haki, tumeona
kesi hii ni uzushi wa wazi au ajenda za kisiasa za kupanda mbegu za
chuki kwa Waziri Mkuu na Mwanasheria wa Serikali, alisema
Mwaipopo.
Alisema kauli aliyoitoa Waziri Mkuu
bungeni, kwamba watakaokaidi amri ya vyombo vya dola wapigwe, haikuwa na
maana mbaya kama ambavyo imechukuliwa na watu wengi, kwani kabla ya
hatua ya kupiga, vyombo hivyo vya dola hufuata kwanza utaratibu na
kanuni zao walizojiwekea.
Hii si kwa polisi nchini, vyombo vyote vya
dola duniani, haviwezi kukuangalia pale unapotishia usalama wa
mwananchi mwingine, lazima uchukuliwe hatua na ikibidi upigwe kwa ajili
ya kutuliza amani na kuhakikisha usalama wa eneo husika,
alisisitiza.
Kamati hiyo pia imeelezea kusikitishwa na
namna wanaharakati hao, walivyoichukulia vibaya kauli hiyo ya Pinda na
kukimbilia mahakamani, wakati siku za nyuma kulitokea matamshi yenye
dalili za kuvunja amani na hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa.
Alitaja matukio hao kuwa ni pamoja na
baadhi ya wanasiasa kutamka wazi kuwa nchi haitatawalika, mauaji ya
Mwembechai, mauaji ya vikongwe Shinyanga, mauaji ya watu wenye ulemavu
wa ngozi, vurugu za Mtwara, vurugu za kisiasa na mabomu Arusha na
Morogoro na wananchi kumwagiwa tindikali.
Hivi karibuni kauawa hadi Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza na vurugu za sasa za kidini na tukirejea nyuma
kuna wanasiasa walikaririwa wakisema nchi haitotawalika, mbona watu hawa
wa haki za binadamu hatuwaoni wakilalamika au kuchukua hatua kama hii
alihoji.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Andrew Mwila alisema
kitendo cha wanaharakati hao kumshitaki Pinda, ni kinyume cha Katiba
kwa kuwa inabainisha wazi kuwa mbunge yeyote ana kinga na yuko huru
kuzungumza bungeni bila kushitakiwa.
Kule (bungeni) wana taratibu zao, kama
kweli mbunge kazungumza mambo mazito, kuna Kamati ya Maadili,
anafikishwa huko lakini ana kinga ya kushitakiwa huku nje, na hilo
tumeshuhudia kwani wapo wabunge wamezungumza mambo hatari na
hawajashitakiwa, hii kesi ni danganya toto kuna mambo mengine nyuma
yake, alisema.
Kwa upande wake, Wakili kutoka kampuni ya
Uwakili ya Austin Wilson, Sweetbert Nkubi, alisema kampuni yake
inakamilisha utafiti wake juu ya suala hilo, na inatarajiwa kuwasilisha
maombi ya kupinga kesi hiyo dhidi ya Pinda, keshokutwa.
Tunachotaka ni kumuomba Mwanasheria Mkuu
awaingize wateja wetu kwenye kesi hii ili watumie fursa hiyo kupinga
mashitaka hayo dhidi ya Waziri Mkuu ambayo yamelenga kutaka ufafanuzi wa
Katiba juu ya tamko hilo alilolitoa bungeni, alisema.
Kwa hisani ya Habarileo.
Toa kichefuchefu chako na uma------ wako.