Wapenda amani nchini kumtetea mahakamani Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Pinda

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,502
KAMATI ya Vijana Wapenda Amani Tanzania (VIWATA) keshokutwa itawasilisha maombi kwa Mwanasheria Mkuu, ya kupinga kesi aliyofunguliwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa kamati hiyo, Said Mwaipopo, alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa kesi hiyo imefunguliwa na wanaharakati hao kwa utashi wa kisiasa zaidi na haitowaletea Watanzania mapinduzi wanayoyataka.

“Sisi vijana wapenda amani na haki, tumeona kesi hii ni uzushi wa wazi au ajenda za kisiasa za kupanda mbegu za chuki kwa Waziri Mkuu na Mwanasheria wa Serikali,” alisema Mwaipopo.

Alisema kauli aliyoitoa Waziri Mkuu bungeni, kwamba watakaokaidi amri ya vyombo vya dola wapigwe, haikuwa na maana mbaya kama ambavyo imechukuliwa na watu wengi, kwani kabla ya hatua ya kupiga, vyombo hivyo vya dola hufuata kwanza utaratibu na kanuni zao walizojiwekea.

“Hii si kwa polisi nchini, vyombo vyote vya dola duniani, haviwezi kukuangalia pale unapotishia usalama wa mwananchi mwingine, lazima uchukuliwe hatua na ikibidi upigwe kwa ajili ya kutuliza amani na kuhakikisha usalama wa eneo husika,” alisisitiza.

Kamati hiyo pia imeelezea kusikitishwa na namna wanaharakati hao, walivyoichukulia vibaya kauli hiyo ya Pinda na kukimbilia mahakamani, wakati siku za nyuma kulitokea matamshi yenye dalili za kuvunja amani na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Alitaja matukio hao kuwa ni pamoja na baadhi ya wanasiasa kutamka wazi kuwa “nchi haitatawalika, mauaji ya Mwembechai, mauaji ya vikongwe Shinyanga, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, vurugu za Mtwara, vurugu za kisiasa na mabomu Arusha na Morogoro na wananchi kumwagiwa tindikali.

“Hivi karibuni kauawa hadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na vurugu za sasa za kidini na tukirejea nyuma kuna wanasiasa walikaririwa wakisema nchi haitotawalika, mbona watu hawa wa haki za binadamu hatuwaoni wakilalamika au kuchukua hatua kama hii…” alihoji.

Mjumbe wa Kamati hiyo, Andrew Mwila alisema kitendo cha wanaharakati hao kumshitaki Pinda, ni kinyume cha Katiba kwa kuwa inabainisha wazi kuwa mbunge yeyote ana kinga na yuko huru kuzungumza bungeni bila kushitakiwa.

“Kule (bungeni) wana taratibu zao, kama kweli mbunge kazungumza mambo mazito, kuna Kamati ya Maadili, anafikishwa huko lakini ana kinga ya kushitakiwa huku nje, na hilo tumeshuhudia kwani wapo wabunge wamezungumza mambo hatari na hawajashitakiwa, hii kesi ni danganya toto kuna mambo mengine nyuma yake,” alisema.

Kwa upande wake, Wakili kutoka kampuni ya Uwakili ya Austin Wilson, Sweetbert Nkubi, alisema kampuni yake inakamilisha utafiti wake juu ya suala hilo, na inatarajiwa kuwasilisha maombi ya kupinga kesi hiyo dhidi ya Pinda, keshokutwa.

“Tunachotaka ni kumuomba Mwanasheria Mkuu awaingize wateja wetu kwenye kesi hii ili watumie fursa hiyo kupinga mashitaka hayo dhidi ya Waziri Mkuu ambayo yamelenga kutaka ufafanuzi wa Katiba juu ya tamko hilo alilolitoa bungeni,” alisema.

Kwa hisani ya Habarileo.
 
Watu wanapigana vikumbo vya kisheria wakati mtoto wa mkulima yuko shambani kwake amechoka baada ya kutoa ushauri kwa polisi pale aliposema,
“Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.

“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.”

Watanzania tuko watu wa ajabu kweli. Kwanza kila siku tunasema hili likatiba la mwaka 1977 ni bovu na linatakiwa kurekebishwa au kufutiliwa mbali, halafu watu kama Waziri Mkuu wanapotumia likatiba hilo hilo bovu kutenda kazi zao, tunakimbia kwenda mahakamani tukidai Waziri Mkuu amevunja katiba. Hivi Waziri Mkuu atavunja vipi katiba ambayo ni mbovu. Yaani wewe umeharalisha wizi kisheria, na mtu akiitumia sheria hiyo kuiba, unapiga kelele na kwenda mahakamani kudai ametenda kosa!. Kosa lipi?.

Sheria zinaharalisha kupitia likatiba hili bovu kwa mwananchi kupata kipigo sawasawa kutoka polisi, na pale Waziri Mkuu alipowakumbusha polisi kutumia sheria zilizopo kupitia katiba, tunakimbia kwenda mahakamani kudai amevunja katiba. Katiba ipi?.

The Deputy Minister for Home Affairs, Mr Pereira Silima, listed several circumstances where the police can be forced to use guns, tear-gas and other weapons in arresting criminals.

The law allows the police to use minimum possible force in restoration of peace in events like unlawful assembly, dangerous riots and similar incidents..

21.​Use of force in making arrest
​(1) A police officer or other person shall not, in the course of arresting a person, use more force or subject the person to greater indignity than is necessary to make the arrest or to prevent the escape of the person after he has been arrested.
​(2) Without limiting the application of subsection (1), a police officer shall not, in the course of arresting a person, do an act likely to cause the death of that person, unless the police officer believes on reasonable grounds that the doing of that act is necessary to protect life or to prevent serious injury to some other person.

Watanzania kwa usanii hatujambo.
 
Waumini.jpg

Mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa kwenye mkutano katika viwanja vya Mwembeyanga,Temeke Jijini Dar es Salaam jana.
 
Ngoja zamu yao nao ifike ya kupigwa ndio watamjua Pinda ninani. Kiongozi kama Pinda hafai kutetewa kwani amekua akitoa kauli tata sana zenye madhara ndani yake hata kupelekea vifo kwa watanzania.
 
Hao sio wapenda amani, ni waua amani, do they know the rule of law? Vijana wa siku hizi kila kitu wanaweka maslahi yao mbele tuu, tunalipeleka taifa hili wapi? Wanatazamia kupata kitu!

The next day wakipigwa wao, wanaanza maandamano! Hebu vijana akili zenu zifanye kazi, nchi inaendeshwa ka sheria sio utashi wa kiongozi!
 
Wale vijana, eti wapenda amani. Wapenda amani wanaotetea wanawake wajawazito na watoto wanaopigwa risasi Mtwara. Wanawake wanaobakwa Mtwara. Wanaume waliotendewa mambo kinyume na haki za binadamu huko Mtwara.

Wapenda amani wanaojipendekeza na kutumiwa na watawala kushangilia mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, wakiwemo wanahabari, wakulima, wafugaji, n.k.
 
Maneno "Sisi", "Vijana" na "Wasomi" yamenajisiwa na siasa uchwara za machokoraa wenye njaa za kupitiliza. Yaani natamani hizi Pre-fix zingeondolewa kabisa na BAKITA katika misamiati ya Kiswahili na tutafute maneno mengine
 
KAMATI ya Vijana Wapenda Amani Tanzania (VIWATA) keshokutwa itawasilisha maombi kwa Mwanasheria Mkuu, ya kupinga kesi aliyofunguliwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa kamati hiyo, Said Mwaipopo, alisema wamechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa kesi hiyo imefunguliwa na wanaharakati hao kwa utashi wa kisiasa zaidi na haitowaletea Watanzania mapinduzi wanayoyataka.

“Sisi vijana wapenda amani na haki, tumeona kesi hii ni uzushi wa wazi au ajenda za kisiasa za kupanda mbegu za chuki kwa Waziri Mkuu na Mwanasheria wa Serikali,” alisema Mwaipopo.

Alisema kauli aliyoitoa Waziri Mkuu bungeni, kwamba watakaokaidi amri ya vyombo vya dola wapigwe, haikuwa na maana mbaya kama ambavyo imechukuliwa na watu wengi, kwani kabla ya hatua ya kupiga, vyombo hivyo vya dola hufuata kwanza utaratibu na kanuni zao walizojiwekea.

“Hii si kwa polisi nchini, vyombo vyote vya dola duniani, haviwezi kukuangalia pale unapotishia usalama wa mwananchi mwingine, lazima uchukuliwe hatua na ikibidi upigwe kwa ajili ya kutuliza amani na kuhakikisha usalama wa eneo husika,” alisisitiza.

Kamati hiyo pia imeelezea kusikitishwa na namna wanaharakati hao, walivyoichukulia vibaya kauli hiyo ya Pinda na kukimbilia mahakamani, wakati siku za nyuma kulitokea matamshi yenye dalili za kuvunja amani na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Alitaja matukio hao kuwa ni pamoja na baadhi ya wanasiasa kutamka wazi kuwa “nchi haitatawalika, mauaji ya Mwembechai, mauaji ya vikongwe Shinyanga, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, vurugu za Mtwara, vurugu za kisiasa na mabomu Arusha na Morogoro na wananchi kumwagiwa tindikali.

“Hivi karibuni kauawa hadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na vurugu za sasa za kidini na tukirejea nyuma kuna wanasiasa walikaririwa wakisema nchi haitotawalika, mbona watu hawa wa haki za binadamu hatuwaoni wakilalamika au kuchukua hatua kama hii…” alihoji.

Mjumbe wa Kamati hiyo, Andrew Mwila alisema kitendo cha wanaharakati hao kumshitaki Pinda, ni kinyume cha Katiba kwa kuwa inabainisha wazi kuwa mbunge yeyote ana kinga na yuko huru kuzungumza bungeni bila kushitakiwa.

“Kule (bungeni) wana taratibu zao, kama kweli mbunge kazungumza mambo mazito, kuna Kamati ya Maadili, anafikishwa huko lakini ana kinga ya kushitakiwa huku nje, na hilo tumeshuhudia kwani wapo wabunge wamezungumza mambo hatari na hawajashitakiwa, hii kesi ni danganya toto kuna mambo mengine nyuma yake,” alisema.

Kwa upande wake, Wakili kutoka kampuni ya Uwakili ya Austin Wilson, Sweetbert Nkubi, alisema kampuni yake inakamilisha utafiti wake juu ya suala hilo, na inatarajiwa kuwasilisha maombi ya kupinga kesi hiyo dhidi ya Pinda, keshokutwa.

“Tunachotaka ni kumuomba Mwanasheria Mkuu awaingize wateja wetu kwenye kesi hii ili watumie fursa hiyo kupinga mashitaka hayo dhidi ya Waziri Mkuu ambayo yamelenga kutaka ufafanuzi wa Katiba juu ya tamko hilo alilolitoa bungeni,” alisema.

Kwa hisani ya Habarileo.
sasa iyo kamati ya wapenda amani mbona hieleweki kwa sababu matendo yake hayaendani na jina la kamati yao.LHRC naTanganyika Law Society wanachotaka ni ufafanuzi na tafsiri ya kikatiba Ibara ya 100 na sheria ya kinga,Haki na madaraka ya Bunge ya mwaka 2002 kama vinatumika ikiwa kiongozi kama waziri mkuu ambaye anapaswa kuzilinda sheria anahamasisha watu kupigwa kitu ambacho ni kinyume na ibara ya 13 ya katiba hiyohiyo ambayo inakataza watu kuteswa au kupigwa.Je,waziri mkuu mnaemtetea hajui sheria na Ibara hii?na anapo sema wananchi wapigwe tu.Je,na sisi wananchi tukiamua kujibu mapigo kutakuwa na amani kweli mnayoitetea?nawauliza vijana wapenda amani isiyo na haki ndani yake.KIGUMU CHAMA CHA WAPENDA AMANI,ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA KAMATI YA WAPENDA AMANI?????????....
 
Njaa ni kitu kibaya sana,
Hiyo haitawasaidia hata kidgo,
Mfumo wa elimu unazalisha vijana hopless waliokosa vission katika maisha yao,waliokosa uzalendo na kukata tamaa kimaisha,
Inatia simanzi na kuleta kichefu chefu hata kuwaona,sembuse tuh kuwaskiliza..!
 
Hakuna chuki ya kupandikizwa wala nini kama kweli wanapenda amani waandae kongamano wawasikie wananchi machungu yao halafu wapeleke kunakohusika!!!!!!

Yaaani mpaka unaweza ona aibu kuwa niaba ya watu wengine kwa jinsi akili zao zinavyofanya kazi!!!!

Mtakutana mahakamani huko na wenye shughuli zao
 
“Tunachotaka ni kumuomba Mwanasheria Mkuu awaingize wateja wetu kwenye kesi hii ili watumie fursa hiyo kupinga mashitaka hayo dhidi ya Waziri Mkuu ambayo yamelenga kutaka ufafanuzi wa Katiba juu ya tamko hilo alilolitoa bungeni,” alisema.

Hii ilivyokaa ni kuomba kazi kwa Mwanasheria Mkuu, vijana hawana kazi, wako benchi so wanaomba kazi ya kuwekwa kwenye orodha ya wanasheria wa serikali kupinga hiyo kesi ili wapate posho. Tanzania bhana kwa posho?!!!!
 
Nawapongeza vijana sasa wanatupa matumaini ya mwelekeo mzuri wamegundua vurugu hazina maana.
 
Hii inaitwa opportunism, wachumia tumbo, ni wahuni tu kama wahuni wengine eti wapenda amani huku wanashabikia kiongozi anayevunja amani kwa kukiuka katiba wajinga kweli.

Nilitegemea instead kamati hii imkemee Pinda kwa kauli za uchochezi badala yake wanamtetea, shit.
 
Maneno
"Sisi", "Vijana" na "Wasomi"
yamenajisiwa na siasa uchwara za machokoraa wenye njaa za kupitiliza.
Yaani natamani hizi Pre-fix zingeondolewa kabisa na BAKITA katika
misamiati ya Kiswahili na tutafute maneno mengine

waacheni vijana waonyeshe uzalendo wao na si hawa vibibi vizee akina kijo bisimba ambao wanakabiliwa na njaa kali
 
Back
Top Bottom