Geeque
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 936
- 316
Hakuna asiejua serikali ya CCM ni genge la Majambazi na Mafisadi ambao hawajui demokrasia ni nini na wala hawaheshimu haki za binadamu, kwa kifupi ni madikteta wakubwa. CCM wanachojua zaidi ni kujitajirisha binafsi, kuiba rasilimali za nchi, kupokea rushwa kubwa ambazo zinadhoofisha uchumi wa nchi na kufanya ufisadi kwa kasi mpya na ari ya kinyonyaji. GOD DAMN CCM.Haki ya kujitenga (right of secession) ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu, mradi iwe imedaiwa kwa msingi wa amani na uamuzi kufikiwa kwa njia za kidemokrasia (mfano referrendum). Hawa wapemba mpaka hapo walipodai haki hiyo hawajakosea chochote, hakuna hata chembe ya uhaini. Ingekuwa uhaini kama wangechukua silaha na kujitangazia jamhuri yao kwa nguvu, au wangeeleza nia ya kutwaa serikali kwa nguvu. Lakini hawa wameandika tu barua na kupeleka katika mamlaka ambayo jambo kama hilo linaweza kujadiliwa, na ambako haki hiyo imetamkwa, ambako ni Umoja wa Mataifa. Kuwaita hawa wahaini na kuanza kuwatisha kwa kuwasomba kwenye madege ya kijeshi kwenda kuwahoji Unguja ni udikteta wa hali ya juu, ni kuwazuia kueleza mawazo yao, jambo ambalo ni kinyume kabisa cha haki za binadamu. Serikali ya CCM inapaswa kuacha kutenda udikteta wakati inahubiri demokrasia.