Wapemba Waanza Kukamatwa

Marufuku kuwaona

2008-05-15 09:14:57
Na Dunstan Bahai

Jeshi la Polisi nchini, limesema halitawaruhusu ndugu wa watuhumiwa wa `uhaini` waliokamatwa kisiwani Pemba kwenda kuwajulia hali mahala wanakohifadhiwa.

Aidha, jeshi hilo limesema ndugu hao wasiwe na wasiwasi kwani ndugu zao wako salama na wakiumwa wanapatiwa huduma za kimatibabu kama binadamu wengine.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Bw. Khamis Mohammed Simba, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

Bw. Simba alikuwa ameombwa aeleze waliko watuhumiwa hao na kama ndugu wanaweza kwenda kuwajulia hali.

Alasiri!!!!!!
 
Mhh...

wamekuwa watuhumiwa wa uhaini?

Kikwete chonde chonde baba acha hii njia sio nzuri kwa usalama wa nchi yetu
 
Mhh...

wamekuwa watuhumiwa wa uhaini?

Kikwete chonde chonde baba acha hii njia sio nzuri kwa usalama wa nchi yetu

Mi niliuliza kwanini huyu jamaa hongelei swala hili wakati yeye ni bingwa msuluhisha maana kenya alienda, comorro alipeleka majeshi na pia ni kuongozi wa umoja wa africa, kwa cheo hico tuu anapaswa awe msatari wa mbele kushugulikia swala hili,

halafu kama hujagundua naona CCm kila mtu ni msemaji mkuu kuhusu swala la mlipuko wa znz. nafikiri hajui kama hili swala limesha kanza kuwa out of hand
 
Kumbuka pia kuwa alitoa ahadi ya kushughulikia mambo ya zanzibar!
 
Hii ndio Tanzania bwana yaani uonevu na uvunjwaji wa haki za binadamu unafanyika kila siku kwa kasi ya juu, MAFISADI ndio walistahili kubebeshwa tuhuma za uhaini lakini sio hawa raia masikini ambao wanaonewa tu kutokana na kutoa dukuduku lao la msingi. Wakati mafisadi wako kwenye viyoyozi wakiendelea kutafuna mabilioni yao ya wizi, Usalama wa Taifa la viongozi MAFISADI na Polisi wanatoka usiku wa manane kuwakamata raia wasio na hatia. Wameanzia Pemba sasa msishangae kesho wakija hapa JF na kusema nasi ni wahaini. Leo hii MAFISADI wanaonekana ni HEROES ndani ya ya CCM na hupokelewa na kupigiwa vigelegele. Heshima wanayoipata MAFISADI nchini Tanzania ni ya juu kuliko hata Mashujaa wetu waliofichua UFISADI.
 
Asalamu alaykum.

viongozi wanaona hilis uala kama ni la mchezo lakini kwa kweli linaweza kuifikisha tanzania pabaya na hasa kama leo mmesikiliza idhaa ya kiswahili ya BBC jioni wananchi wa pemba ambao wanatoa maoni yao kuhusu wenzao walivyokamatwa wamesema wazi wazi kumwambia Rais Kikwete kwamba wao hawaogopi na watu waliokamatwa 12 hawapo peke yao ni kisiwa kizima kwa hivyo kuna watu wapo tayari wanasema wakakamatwe huko na polisi waunganishwe na wenzao kwa kweli hali mbaya.

ndio yale aliyosema dk. salim ahmed salim asiyejua kufa aangalie kaburi.

stonetowner
 
Hivi kuna mtu yoyote ameshajiuliza kwa nini serikali yetu iliact swiftly kuwakamata hawa watu? what connects the dots....Anybody?
 
na ndo hapo ninapowakubali wazungu. coz wao huziba maji yanapotoka na si kujenga mtaro. serikali ilitakiwa ikae chini na kuzungumzia kwa kina hili swala la mgogoro wa pemba na hapo ndo wangekuwa wameziba mtaro.
lakini wanavyo wakamata jamaa na kuwapandikizia kesi za uhaini huko ni sawa na kujenga mtaro.
 
nyuma ya tukio hili kuna chama cha CUF, hivi ni sawa wengine waumie kwa maslahi ya wachache?
wanachafua hali ya hewa kwa manufaa binafsi? huwageuzA kila siku wenzao ni kafara

Mimi sioni tabu kama kuna uhusiano na chama cha CUF vilevile sishangai kama mtunzi ni CCM au MASTERMIND.
Ni lazima kuwepo na wenzao sasa ikiwa wamesema wamehusika watu 10000 ,hivi hapo au humo mtakosa CUF au CCM ,Mkapa alikuja na nuksi kwa kila mtanzania kuna waliokuwa wakizama na majahazi na kuna waliozama na meli kuna waliopinduka na treni kuna walioanguka na ndege ila Kikwete yeye naona amekuja na majungu !
Sidhani kama iliwahi kutokea Pemba kuzuka jambo hili ila naamini sasa na huu ni mwanzo wa mwamko wa hisia za kujikomboa.
 
Acheni kuongea pumba. kwa akili zenu kweli mnakubali Pemba ijitenge? mmelogwa nini. ijitenge kwasababu gani? kwasababu wamegundua mafuta pale wafaidi peke yao?au kwasababu ya tatizo dogo tu la muafaka huu ambao unaweza kumalizwa kidiplomasia tu natukaendelea kuishi kwa amani zote. nyie msiwe kama watoto wadogo. sasa huu mziki walioanzisha mi nakwambia wataucheza wenyewe. ni kitu mbaya sana kutaka kujitenga.siku hizi dunia nzima watu wanatafuta kujiunga, wao wanatafuta kujitenga. akili gani hiyo?, badae,watu wa kusini wataamua wajitenge makao yao makuu ya nchi yao yawe mbeya. wakaskazini nao itafika kipindi wataamua yawe mwanza. wachaga nao itafikia kipindi watasema yaleyale ya Chifu Maleale, wawe na nchi yao ya kilimanjaro. badae wapwani watasema,sisi tunataka nchi inayoitwa dsm. huu upuuzi ni aibu kwa watu wenye akili kama watz. hata kama kuna matatizo,tushughulikie kuwa pressurise viongozi wamalize tofauti zao, na sio kuomba kujitenga. yasinge patikana mafuta huko pemba mngekuwa na wazo kama hilo?, na je,kama mna roho chafu kama hiyo nyie wapemba wachache,basi siku nyingi mlikuwa na mawazo hayo moyoni na mlikuwa mnatafuta sababu. sasa mmeipata na mnataka kutimiza azma yenu. kwataarifa yenu, naomba muende polepole na tuheshimiane. KAMWULIZENI MUHAMAD BACAR kule anjourn. atawapa ushauri mzuri sana. hata wao walikuwa na matatizo kama hayohayo ya kwenu. solution waliyoichukua,ilikuwa wrong way. na nyinyi fikirini kwanza kabla yakuamua kufanya huu upuuzi. period.
 
Mkuu Kidzogalae vipi? kwanini usifikirie kwa upande wako huenda unayoyaongea wewe ndiyo pumba (SIJAKUBALIANA NA KIMEO LAKO KWAMBA TUNAONGEA PUMBA).

Ukisoma vizuri maoni ya watu wengi hapo yanalenga katika mabo yafuatayo
1) kupinga ubaguzi na unyanyasaji wanofanyiwa wa Pemba
2) kupinga kukamatwa kwa Wazee waliowasilisha maoni/mapendekezo yao UN na kukubaliwa ingekuwa ni uhaini UN wasinge kubali kwani policy ya Un ni UMOJA.
3) Kuzuiliwa kwa waliokamata kwa zaidi ya masaa yanayotakiwa kisheria tena kuwazuia ndugu kwenda kuwatembelea, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
4) Jambo lolote linaloashiria mabavu hasa ya kijeshi linazidisha chuki ya Wapemba hivyo linapaswa kuepukwa.

Nikirudi kwako Kidzogalae wewe umefurahia kwa watu hao kukamatwa na kwamba wameanzisha muziki na wataucheza wenyewe. Unaonekani ni mnyanyasaji mkubwa wewe. I hate oppressors.

Tulenge kutoa maoni ya namna ya kusuluhisha tatizo siyo kuchochea chuki miongoni mwa jamii yetu.
 
wewe ulitaka selikali ifanye nini sana kama watu wanaonyesha element za kuligawa taifa kiasi hicho?ulitaka wakae kimya waasubirie? unafikiri mwisho wake ungekuwa nini? unaposema waliokamatwa ni wazee, unafikiri wazee wetu wakifanya makosa tuwaache kwasababu wao wameenda age? wewe unafikiri mwisho wa huu muziki ninini? frankly speaking nambie wewe unasapoti hii issue ya wapemba au sio. kama kweli wewe sio mmoja wa hao, nambie hapahapa public kama unasapoti wapemba wajitenge. kama hautasema basi utajulikana wewe ni mpemba mbinafsi na unatakiwa ukamatwe hata wewe. bado niko palepale, mnaosapoti wapemba kujitenga,mnaongea pumba.period.
 
Kidzogalae, mimi siyo Mpemba tena sijawahi hata kufika Pemba wala Unguja, mimi ni Mtanzania. Msimamo wangu ni UMOJA ndiyo maana naunga mkono hata shirikisha la Afrika Mashariki (hata kwenye ile thread yako ya Mradi wa magadi, nimekushangaa unavyo wachukia wakenya).

Sababu nilizo zitoa hapo juu ndiyo zinazonifanya nitofautiane na wewe. Zisome tena sababu ya 1 mpaka 4. I hate oppressors and racists.
 
Nziku, niko nyuma yako, hususan sababu ya tatu. Hiyo inanisumbua vibaya mno.
 
hahaha, wewe bwana mdogo, acha kutupiga mchanga wa macho hapa. nenda kale chakula ulale kwanza lunch imefika.
 
Back
Top Bottom