Wanawake msikengeuke kisa eti mmefika chuoni ama una Degree

mi naona tabia haihusiani nakiwango cha elimu au kiasi cha pesa ulicho nacho. YAWEZEKANA MTU ANA TABIA FULANI LAKIN HAJAPATA NAFASI YAKUONYESHA TABIA ukiona mwanamke/mwanaume kaenda kusoma/kapata pesa akabadilika ujue hiyo ndio tabia yake halisi sema alikuwa hajapata nafasi wala usijidanganye amekengeuka. kuna watu wengi wameoa la saba C (namaanisha failed coz enzi zetu angepataAnaB) angefaulu lakini haheshimiwi hadhaminiwi majukumu mengi bado yamemlemea utajuta. kuna wanawake/wanaume ndoa zao zina amani mwenzie akiwa hana hata hamsin. najaribu tu kumwambia mtoa mada ukiona kapata chuo kamwacha mtu ujue alikuwa naye tu kwakuwa hajapata anayemtafuta. NENDA SHULE/PATA HELA TUJUE JE UNAMPENDA MPENZI WAKO
 
Duh! We jamaa mbona una wivu sanaa mwache mpenzi wako ampende mtu wa level yake na usijipe moyo kwa story ya shigongo.mwanaume pambana na sio kulala mika.usilete mauzo muda wa kazi financial success is the only freedom in life.Afu watanzania wengi nawashangaa sana jinsi mnavyo fananisha Elimu na kisomo eti vyote sawa.mamaee mwanaume fanya kazi kwanza.Hawa wanawake wapo tuu.unataka upendwe hela huna na isitoshe hata kitabu ulikimbia unataka umpate nan sasa.sugua kichwa bwana
 
kumbe ukilaza ni unapimwa kwa kutafuta hela?ama darasani kwa kipimo chepesi na kilichozoeleka

Bongo waliosoma hawana tofauti sana na wasiosoma ambao wanahela..... kwani waliosoma wanatafuta vyeti kwaajili ya kuajiriwa wapate hela baasi. Hatuna ubunifu na wala hatuwezi kuvumbua.
 
aaaaaaaaaaaaaah wapi, tunapenda sana muendeleeeeeeeeeeeeeeee, ila tabu yenu mukishaendele munakengeuka muno wakati mshapendana toka mwanzo

Mabadiliko yanapotokea huna budi kukubaliana nayo ndugu.... hata nyie hamkawii kutupiga chini wanawake ambao hatujasoma kwa kudai kuwa hatuna msaada kwenu sababu ya elimu ndogo tulonayo... sasa hapo ndio shida .....
 
Jipe moyo usisome ukitegemea utapendwa na maisha ya sasa yalivyo.....Ukiona wanaorudi darasa ukubwani usifikiri wajinga na wanaenjoy....yamewakutaaaa




Wale wadada wasioisha kudharau wanaume wasio na elimu ama wao hawawataki ama wanashangaa na kuwacheka rafiki zao wenye wapenzi wasioenda kidato wanapaswa kupata somo kutokakwa mwandishi nguli wa vitabu Eric James Shigongo.


ERIC JAMES SHIGONGO ANA MKE MWENYE ELIMU YA MSTERS LAKINI YEYE ALIKOMEA DARASA LA SABA TU. ALIKUWA AKIONGEA VOICE OF AMERICA KWENYE STRAIGHT TALK TO AFRICA ON AFRICAN WRITERS.

KAMA HAITOSHI HATA DARASANI ALIKUWA NDIO KILAZA WA DARASA KWAKUSHIKA MKIA NA HATA KUPATA SIFURI KIASI MPAKA AKAWA AMEPEWA JINA LA MADASO( hili ni neno la kisukuma likimaanisha nguo iliyoisha na kuchakaa ambayo haifai tena kuvaliwa, kwa kiswahili rahisi ni sawa na tambala, na jina hilo kwa haraka haraka katika kisukuma linamtambulisha shigongo kama mtu asiye na faida yoyote).


Mabinti wapendeni wapenzi wenu bila kujali hali yao kama mlishakubaliana toka mwanzo, just fight for life.

Hizi habari za kukengeuka kila kila mnapofika chuo na kujiona mmesoma sana na kuwatupilia mbali wapenzi wenu kisa wao hawakupenya kufika chuo ama hawakusoma si suluhisho la mapenzi wala maisha.

Stori nyingine ni inspiration kwa vijana na hapa si mahala pake.
 
Jipe moyo usisome ukitegemea utapendwa na maisha ya sasa yalivyo.....Ukiona wanaorudi darasa ukubwani usifikiri wajinga na wanaenjoy....yamewakutaaaa
ninaowashauri wenyewe ndio kama hawa, kazi ipo. kwa hiyo kila ukipanda ngazi kielimu unampiga chini mpenzi wako?
 
Duh! We jamaa mbona una wivu sanaa mwache mpenzi wako ampende mtu wa level yake na usijipe moyo kwa story ya shigongo.mwanaume pambana na sio kulala mika.usilete mauzo muda wa kazi financial success is the only freedom in life.Afu watanzania wengi nawashangaa sana jinsi mnavyo fananisha Elimu na kisomo eti vyote sawa.mamaee mwanaume fanya kazi kwanza.Hawa wanawake wapo tuu.unataka upendwe hela huna na isitoshe hata kitabu ulikimbia unataka umpate nan sasa.sugua kichwa bwana
ukisema wa level yake unamaanisha nini? ushajua hii mada inanihusu mimi? ukiwa na fikira fupi ndio madhara yake haya.
 
tatizo wanaume wengine wanajistukia tu kama hawajaenda kidato, ukifanya kitu kidogo tu anaona kama unamdharau kumbe mtu hata huna wazo hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom