Wanaume wenye experience na jambo hili naomba ndio wanijibu

Ndege Tausi

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
992
472
kama mume mkewe hajabahatika kumzalia mtoto. lakini mume anaye mwanamke nje ya ndoa anamzalia watoto halafu mwanaume huyo anaendelea kumwambia mkewe eti bado anampenda sana, je ni kweli anampenda mkewe? Naomba wajibu wanaume ambao hili jambo limewatokea tafadhali.
 
Sijui ni uzoefu wa aina gani unauhitaji kwenye hili lakini mi naona hili linaweza kujibiwa na yoyote yule anaethamini ubinadamu

Kimsingi hakuna anaeweza kuwa na mapenzi na watu wawili tofauti
Mapenzi huenda na kuheshimiana pia
Huwezu kudai una mapenzi na mtu halafu una mwanamke mwingine huo ni uongo

Suala la kupata mtoto ni majaaliwa na mtu yoyote anaefikiri kidogo tu anaweza kuliona hilo
Kama mmekwenda hospital na kuangalia na mkaambiwa hakuna mwenye matatizo ni kwanini unamuadhibu mwenzako kwa adhabu ya kibazazi kama hii?
Kwanini usimuache tu akajua moja?

Kama wewe mtoa mada ni mwanamke tambua hapo huyo jamaa hakuwa anajua hata upendo ni kitu gani wakati anakuona na hajui upendo ni kitu gani

Wakati anakuoa alikuwa anakuona kama mashine ya kufyatua watoto na sio kweli kuwa alikupenda kama alivyokuwa anakuambia

Kama anakupenda ni kwanini afanye jambo la hovyo kama hilo?

Mtoto ni kitu gani hadi uamue kumfanyia mwenzako unyama wa aina hii?

Huwa sipendi sana hii .......!!!!!!
 
Ubarikiwe sana ndugu yangu. Uzoefu ninaouzungumzia ni kama huo wa huyo mume wa kuwa na mke ambaye hakuzaa na hawara ambaye kamzalia. Nilihitaji wanipe ule ukweli ulioko ndani ya mioyo yao kama bado wana mapenzi na wake zao au ni fix tu.
 
Mi ni msichana japo umeomba ushauri kwa wanaume. Upendo wa kweli huvumilia yote, na kama huwezi kubeba mizigo ya mpendwa wako basi wewe huna upendo wa dhati. Hivi kuna mtu anayependa asizae kwa muda ambao yupo tayari kuanzisha familia. Do you know how it hurts kuona wenzako wanaitwa baba au mama afu wewe huna hata dalili ya kushika mimba? Yote tisa, uje ujue mumeo kazaa nje ya ndoa coz wewe huwezi kuzaa for the meantime (hatujui utazaa lini au ndo hutozaa milele)

Men should stop taking things lightly. Hivi itakuwaje wewe uwe na matatizo ya uzazi afu ukagundua mkeo kapewa mimba na mwanaume mwingine, hivi utataka kweli ht kumuona huyo mwanamke? Na vipi utamlea kwa moyo huyo mtoto kama ambavyo nyinyi mnatuleteaga watoto wenu mliozaa nje tuwalee? Jamani na sisi wake zenu tuna mioyo ya nyama, mtuvumilie tu kwani hakuna anayependa asizae watoto. Tujifunze kubebeana mizigo (matatizo)

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kama mume mkewe hajabahatika kumzalia mtoto. lakini mume anaye mwanamke nje ya ndoa anamzalia watoto halafu mwanaume huyo anaendelea kumwambia mkewe eti bado anampenda sana, je ni kweli anampenda mkewe? Naomba wajibu wanaume ambao hili jambo limewatokea tafadhali.

Inawezekana sana kuwa anakupenda sana kwani asipokupenda atakuacha. Sote tu binaadamu na tunaongozwa na mazingira na hamu ya jambo au kitu ni moja ya mazingira hayo.
Hata hivyo ili kuondowa kuonekana udanganyifu ndipo mungu ameweka ndowa za zaidi ya mke mmoja (waislamu). kukosekana kwa uwazi ndio kunasababisha kutofahamiana na matatizo mengi ya kuzaa watoto nje ya ndowa!
 
Huko ughaibuni (hasa nchi za magharibi) kuna kitu kinaitwa kuasili watoto(adoption) hivyo kwa wanandoa ambao kwao inashindikana kuwa na biological children huwa wanaasili. Tatizo kwetu hilo jambo bado halijazoeleka/kukubalika hivyo kwa wanaume wengi ambao wanatamani kuwa baba lakini wake zao ndo wanamatatizo jamii iliyozunguka mara nyingi huwashawishi kuacha alama kwa kupitia vimada so unakuta mwanaume anakupenda lakini kuna presha za ndugu wazazi n.k sasa ili kupambana nazo na kuwa na win win situation hufanya hivyo. Ila mimi hayajanifika lakini naifaham presha kutoka kwa ndugu na jamaa.
 
Sijui ni uzoefu wa aina gani unauhitaji kwenye hili lakini mi naona hili linaweza kujibiwa na yoyote yule anaethamini ubinadamu

Kimsingi hakuna anaeweza kuwa na mapenzi na watu wawili tofauti
Mapenzi huenda na kuheshimiana pia
Huwezu kudai una mapenzi na mtu halafu una mwanamke mwingine huo ni uongo

Suala la kupata mtoto ni majaaliwa na mtu yoyote anaefikiri kidogo tu anaweza kuliona hilo
Kama mmekwenda hospital na kuangalia na mkaambiwa hakuna mwenye matatizo ni kwanini unamuadhibu mwenzako kwa adhabu ya kibazazi kama hii?
Kwanini usimuache tu akajua moja?

Kama wewe mtoa mada ni mwanamke tambua hapo huyo jamaa hakuwa anajua hata upendo ni kitu gani wakati anakuona na hajui upendo ni kitu gani

Wakati anakuoa alikuwa anakuona kama mashine ya kufyatua watoto na sio kweli kuwa alikupenda kama alivyokuwa anakuambia

Kama anakupenda ni kwanini afanye jambo la hovyo kama hilo?

Mtoto ni kitu gani hadi uamue kumfanyia mwenzako unyama wa aina hii?

Huwa sipendi sana hii .......!!!!!!

Huwa najiuliza sana kama cheating na upendo vinamahusiano!

Pia siamini kuwa anaemcheat mke/mme anamaanisha hampendi mwenzi wake

Mimi naamini hivi:
Mtu anae cheat upendo ( mapenzi) ninaposema mapenzi namaanisha zile hisia za kufeel you love somebody,huyu kweli ni kwamba hampendi mkewe/mke lkn kunawatu wanacheat sex na sio upendo. You may have sex with a person you don,t love sijui kama walijua hilo mkuu
 
Huko ughaibuni (hasa nchi za magharibi) kuna kitu kinaitwa kuasili watoto(adoption) hivyo kwa wanandoa ambao kwao inashindikana kuwa na biological children huwa wanaasili. Tatizo kwetu hilo jambo bado halijazoeleka/kukubalika hivyo kwa wanaume wengi ambao wanatamani kuwa baba lakini wake zao ndo wanamatatizo jamii iliyozunguka mara nyingi huwashawishi kuacha alama kwa kupitia vimada so unakuta mwanaume anakupenda lakini kuna presha za ndugu wazazi n.k sasa ili kupambana nazo na kuwa na win win situation hufanya hivyo. Ila mimi hayajanifika lakini naifaham presha kutoka kwa ndugu na jamaa.

Kuasili watoto mume alikataa kwa madai eti tabia zao zinaweza kutusumbua. Kuhusu pressure ya ndugu zake mume, nahisi kama kawaida ya miafrika mume anazipata.
 
Binafsi naona anakupenda ,tena sana tu.angekuwa hakupendi angekuacha.kasome biblia uone jinsi sarah alivyomshawishi abraham alale na kijakazi ili apate uzao,lkn pia soma uone kizazi cha lutu kiliendelea vp,we si rahisi kihivyo mwanaume rijali kizazi chake kiishie hewani,mapenzi ni kitu kingine na watoto wana umuhimu wao kwa kila kizazi.hv unajua mwanamke na mwanaume nani huendeleza kizazi ?
 
easier said than done, yaani kwa uzoefu wangu hili jambo ni zito sana sio la kuchukulia kirahisi rahisi tu kwamba kama unampenda utavumilia, utamheshimu, and the like (kwa pande zote mbili)

Kinacholeta ugumu zaidi ni pale mwenza mmojawapo anapogundua kwamba alikuaw cheated kwenye hiyo hali...kwamba mtu anajua kabisa ana tatizo hilo ila anaaamua aingie kwenye ndoa huku akijua matarajio makubwa hasa kwa sisi familia a kiafrika ni watoto.
Tatizo linakuzwa zaidi na hali ya utoaji mimba iliyokithiri kwa baadhi ya kinadada, yaani anataka afaidi 'usichana' na anataka akishamaliza ndo atafute 'boya' limuoe na yeye awe na P.O.Box mjini hapa....sasa mwenza akijua alidanganywa ni rahisi sana kutafuta 'uzao' nje

Jambo jengine ni wazazi pande zote mbili kuwa wanaulizia wajukuu kila mara, kwamba ndoa ina miaka miwili bila mtoto tayari kelele zinakuwa zimeshaanza kwamba "mnasubiri tufe bila kuona wajukuu' ....hili naona pia lianchangia kushawishi kuchepuka nje....marafiki pia wanachangia..unajisikiaje kukaa na marafiki zako wanaongelea mambo ya shule, ada, kliniki nk wakati wewe hola

Nirudie kusema kwamba tusimhukumu yeyote anayechepuka kwa sababu hatujui hasa ni nini. kama alivosema mchangiaji mmoja hapo juu, love is not equal to sex....., na wakati mwingine kama akipatikana mtoto inasaidia kustabilise mahusiano maana wazee wanajua kuna mtoto 'mahali', na malalamiko yanapungua ndani kama waliioona na waelewa..LAKINI kama ndio wale wa strictly hakuna kuchepuka na wanaamini hivyo no matter what,hili litakuwa jakamoyo!

Ngoja niishie hapa kwanza, wakubwa wenzangu watakuwa wamenielewa

CC Asprin, snowhite Nicas Mtei
 
Last edited by a moderator:
je ikiwa mwanaume hana uwezo wa kuzaa,

mke akazaa na mwanaume mwengine, na akamwambia mumewe anampenda...

je unadhani ni kweli anampenda mumewe?
 
Kuasili watoto mume alikataa kwa madai eti tabia zao zinaweza kutusumbua. Kuhusu pressure ya ndugu zake mume, nahisi kama kawaida ya miafrika mume anazipata.

Hilo neno hilo, bado upo utumwani mwa watu weupe?
 
je ikiwa mwanaume hana uwezo wa kuzaa,

mke akazaa na mwanaume mwengine, na akamwambia mumewe anampenda...

je unadhani ni kweli anampenda mumewe?

hivi shemeji BADILI TABIA, unadhani ni kwanini utafiti unaonyesha kuwa 48% ya wanandoa walioenda kucheki DNA zao walikuta kwamba watoto sio wa kwao (wababa)?

Ninachojua wanawake ni wajanja sana, akishajua kwamba mambo nehi anachepuka descreetly anakuwa mjamzito mtoto ni wa kwako baaas,,,,aibu haipo tena hapo na heshima ya mume inaendelea kuwapo...wapo wengi tu wa namna hii hahitaji kumwambia.....kwa mwanaume ndo kasheshe
 
Last edited by a moderator:
kama mume mkewe hajabahatika kumzalia mtoto. lakini mume anaye mwanamke nje ya ndoa anamzalia watoto halafu mwanaume huyo anaendelea kumwambia mkewe eti bado anampenda sana, je ni kweli anampenda mkewe? Naomba wajibu wanaume ambao hili jambo limewatokea tafadhali.

uzoefu sina coz waifu kazaa na sina dem nje
 
Sijui ni uzoefu wa aina gani unauhitaji kwenye hili lakini mi naona hili linaweza kujibiwa na yoyote yule anaethamini ubinadamu

Kimsingi hakuna anaeweza kuwa na mapenzi na watu wawili tofauti
Mapenzi huenda na kuheshimiana pia
Huwezu kudai una mapenzi na mtu halafu una mwanamke mwingine huo ni uongo

Suala la kupata mtoto ni majaaliwa na mtu yoyote anaefikiri kidogo tu anaweza kuliona hilo
Kama mmekwenda hospital na kuangalia na mkaambiwa hakuna mwenye matatizo ni kwanini unamuadhibu mwenzako kwa adhabu ya kibazazi kama hii?
Kwanini usimuache tu akajua moja?

Kama wewe mtoa mada ni mwanamke tambua hapo huyo jamaa hakuwa anajua hata upendo ni kitu gani wakati anakuona na hajui upendo ni kitu gani

Wakati anakuoa alikuwa anakuona kama mashine ya kufyatua watoto na sio kweli kuwa alikupenda kama alivyokuwa anakuambia

Kama anakupenda ni kwanini afanye jambo la hovyo kama hilo?

Mtoto ni kitu gani hadi uamue kumfanyia mwenzako unyama wa aina hii?

Huwa sipendi sana hii .......!!!!!!

Ukimkosa mtoto ndo utajua thamani ya mtoto;
Unauliza mtoto kitu gani?????
 
je ikiwa mwanaume hana uwezo wa kuzaa,

mke akazaa na mwanaume mwengine, na akamwambia mumewe anampenda...

je unadhani ni kweli anampenda mumewe?

Ningependa ufahamu kuwa kuzaa na mtu si kwamba wampenda huyo mtu.

Love is not chidren,
Love is not sex,
Love is all about feelings. Pia love ni roho na ndiomaana huweza kufa.

Kunawatu ambao roho ya upendo ilikufa, hawa watu hawawezi kupenda lkn wanafanya sex ili kutimiza matamanio ya mwili
 
Back
Top Bottom