Wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao, kweli?

Si ndo toto la kiume linapelekewa pilau na kachumbali kila j2 lipo UDSM hapo linapelekewa pilau na mama ake
Malezi ya design hii yamechangia sana vijana kuhamia upande wa Cameron mtoto wa mama anavaa heleni anasuka nywele dah inasikitisha sana wao wakinana mama wanaita malezi ya kisasa kumpelekea mtoto wa kiume pilau chuo dah inasikitisha sana.

Halaf pilau lenyewe linapelekewa na toothpick eti vinyama vikiganda kwenye meno lipekechue, mzembe nina ulimi wa ng'ombe kikiganda nafyonza. Kinamama wanaangamiza jinsia kamanda, leo lazima watubie kwenye hii sredi
 
Hata miye mwanzisha mada nimebaki nashangaa watu kuigeuza mada ikawa ya mapishi na kujua kupika wakati kuna mambo mengine kama heshima, upendo, kujali, na mengine niliyoyaorodhesha na yale ambayo sikuyaorodhesha!
Ndio JF ilivyo hahahah

Usikate tamaa Tausi,

Wewe nenda mdogo mdogo, tutafika kila pande....Ki ukweli hoja ya hao wadada uliowasikia si ya kweli wakati wote!

DC
 
Ukiwa kama mama unamfungashia mwanao wa jinsia ya kiume wa chuo kikuu pilau tena mwaka wa pili!!!! si unamdekeza
Siku usipo mpelekea anaanza kudeka mwishowe wanaume wanakusaidia kumnunulia chipsi mayai,kuku na pepsi juu

Fidel kama unamzungumzia mtu makhsus. Ulikutana nae chuo mwaka wa pili nini?
 
Binafsi nadhani mwanaume kujua kupika katika zama hizi is a PLUS!!
Mwanaume kama hujui kupika mbona unaweza kujikuta katika hali mbaya pale huyo mkeo hayupo.

Aaa wapi!! Hali mbaya itoke wapi wakati siku hizi kila kona kuna chakula? Nianzie brake point, hongera, miti mirefu,..... jackies....... hiyo hali mbaya nitaitoa wapi?
 
Halaf pilau lenyewe linapelekewa na toothpick eti vinyama vikiganda kwenye meno lipekechue, mzembe nina ulimi wa ng'ombe kikiganda nafyonza. Kinamama wanaangamiza jinsia kamanda, leo lazima watubie kwenye hii sredi

Mtaani kwetu kuna mama leo nampelekea uzi huu mtoto wa jinsia ya kiume anamvalisha nguo za kike anampiga na gauni eti la kushindia hawa akina mama kwakweli wanaangamiza jinsia ya kiume wanataka wanaume wafanya mambo ya wanawake lol.
 
Uzoefu unaonyesha wanaume waliolelewa na baba zao:

Wanapiga masanga kwa wingi
Wana ujasiri wa hali ya juu
Hawadekideki hovyo
Hawabagui misosi, wanaridhika na mapishi yoyote yale
Siyo mabishoo wala masharobaro
Ni wahangaikaji wa kusaka mikwanja
Hawawapelelezi wanawake hovyo hovyo, wanawaamini.
Siyo wambea.

Utafiti huo ukonyesha tena kuwa wanawake wengi hupenda wanaume wa namna hii.

CONCLUSION: Malezi ya baba na mama ni bora zaidi kuliko malezi ya mzazi mmoja bila kujalisha jinsia.
 
Huh! Fidel staki.....ana umri gani huyo mtoto?
 
Ukiwa kama mama unamfungashia mwanao wa jinsia ya kiume wa chuo kikuu pilau tena mwaka wa pili!!!! si unamdekeza
Siku usipo mpelekea anaanza kudeka mwishowe wanaume wanakusaidia kumnunulia chipsi mayai,kuku na pepsi juu
Inategemea na mtoto mwenyewe bana, inamana kumpa mtoto chakula ni kumdekeza? Unampa huku unamfundisha kuwa leo kipo bt kisipokuwepo pia akubaliane na hiyo hali... Nikimpelekea ugali je ni sawa?
 
Uzoefu unaonyesha wanaume waliolelewa na baba zao:

Wanapiga masanga kwa wingi
Wana ujasiri wa hali ya juu
Hawadekideki hovyo
Hawabagui misosi, wanaridhika na mapishi yoyote yale
Siyo mabishoo wala masharobaro
Ni wahangaikaji wa kusaka mikwanja
Hawawapelelezi wanawake hovyo hovyo, wanawaamini.
Siyo wambea.

Utafiti huo ukonyesha tena kuwa wanawake wengi hupenda wanaume wa namna hii.

CONCLUSION: Malezi ya baba na mama ni bora zaidi kuliko malezi ya mzazi mmoja bila kujalisha jinsia.
Kuna leo na kesho, kama baba katangulia mbele ya haki je? Tena katangulia wakati mtoto wa kiume ana 2years, hapo vipi?
 
mwanaume alielelewa na mwenye urafiki na mama yake ni sumu ,hana maamuzi ,anakuwa tu kama mtoto tena anakuwa na visa balaa
alielelewa na baba au dunia huyo ndo mwanaume

Na mwanaume anae soma chuo mwaka wa 3 anapelekewa ubwabwa na mama yake unazungumziaje hili Smile ndo malezi mazuri?
 
Back
Top Bottom