Wanaume Wa JF Tukutane Hapa

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,271
29,880
Mwanaume ni
binadamu wa jinsia ya kiume, kwa maana anafaa kuwa mume.

Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau ame balehe .

Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kiume tu au mvulana .

Baada ya kuzaa anaitwa kwa kawaida baba , jina lenye heshima kubwa katika utamaduni wa aina nyingi.

Akianza kupata wajukuu , anajulikana pia kama
babu.

Wanaume ni takriban nusu ya binadamu, wengine huwa wanawake .

Wanaume na
wanawake ni jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.
Mwanamume ana tabia zake za pekee upande wa mwili , nafsi na roho , na tofauti kati yao na wanawake hujitokeza kwa namna mbalimbali katika utendaji.

Katika maumbile ya mwili wanaume huwa na
viungo vya uzazi vya kiume ambavyo ni pekee kama vile mboo (uume, dhahakari) na mapumbu (korodani).

Wakati wa ku balehe homoni ya testosteroni inaongezeka mwilini mwa mwanaume na kusababisha tabia kama sauti ya chini, kongezeka ya nywele mwilini (kwa mfano
ndevu ), kuongezeka kwa upana wa mabega na
kiwango cha musuli mwilini kulingana na wanawake.

Msingi wa tofauti hizo ni hasa chembeuzi kinachoitwa "Y" yaani wanaume wana jozi la
chembeuzi "X" na "Y" ndani ya seli zao zote, lakini wanawake wana jozi la "X" mbili.

Chembeuzi Y inabeba habari zote zinazomfanya mwanadamu kukua kama mwanaume badala ya mwanamke.

Lakini si tofauti za mwilini pekee zinazosababisha wanaume kuwa tofauti na wanawake. Kuna pia tabia za ki akili na za ki roho za pekee zinazoonekana kati ya wanaume wengi.

Hata hivyo tofauti nyingi zinategemea pia
utamaduni kwa sababu mara nyingi watu wamepanga shughuli na pia namna ya maisha tofauti kwa wanaume na wanawake, hivyo watu wamezoea kuchukua matokeo ya mapatano haya kama jambo la kimaumbile hata kama ni la kiutamaduni tu.

Pamoja na hayo, kuna wanaume wasio wachache sana wenye tabia zinazotazamiwa kuwa za kike kwa sababu miili yao huwa na viwango vya homoni vilivyo tofauti na kawaida.

Kuna watu kadhaa wenye mwili wa kiume wanaojisikia kuwa wanawake, pengine kutokana na matukio ya utotoni au athari nyingine za
kisaikolojia..........

Wanaume Wenzangu Njoen Hapa Tupeane Mbinu Mbali Mbali Za Kufanikiwa Katika Maisha

Changamoto Za Kimaisha Na Ni Jinsi Gani Ya Kuziepukika Izo Changamoto

Najua Kuna Wanaume Wengi Sana Walio Fanikiwa Katika Nyanja Tofaut Tofaut

Ni Vzr Ukatoa Elim Iyo Taaluma Uliyo Nayo Kwa Wengine

##Nawasilisha
 
Nawakumbusheni tu.... Msisahau condom UKIMWI upo na unaua sana wanaume kuliko wanawake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom