Wanaume, tupeni majibu hapa...

Hivi kwanini wenzetu nyie si wepesi hata kidogo wa kukiri makosa yenu na kuomba msamaha? Kwanini mara nyingi huwa mnatafuta means ya kujusfty makosa kuliko kuomba msamaha? je ni ubabe ama ni aibu ama mnahisi kufanya hivyo ni kujishusha hadhi yani kutoka kuwa mwanaume na kuwa mtu mwingine?

je na kwa wale mnaokiri na kuwaangukia wake zenu kwa samahani, je wake zenu wamewahi kubadili heshima yenu ama hata kukudharau?

leo akina mama tukae tuwatupie maswali kwa kila hoja watakazo leta hadi tujue nini ni nini.

nawasilisha.

Ukiomba sana msamaha ugali utashindwa kuingia mezani
 
hivi nikikuomba msamaha utanufaika na nini hasa wakati kosa liliishatendeka? kwanza mkiombwa msamaha huwa mnavimba vichwa ni bora muombwe msamaha wa mangumi tu na manundu baaaaaasi mtatulia
 
aisee! you are lucky ila kuna wanaume ni wabish wasamahan na wengine wanadai eti kuish na mwanamke mgomvi ni bora uish kwenye paa. yaani men .................goja waje niwaskie hapa.

kitu kimoja nimegundua kwa wanaume, wana roho ndogo sana wao wagumu kusamehe ila wanataka kusamehewa mapema na kosa liishe, ila ukiwajulia unawakong'oli pale wanapokuboa au unag'ata huku unapuliza japo ukipata mwanaume anayejua kupenda na kucare.... walaaahi hutajuta kuzaliwa kwako na utamuenzi mama mzaa huyo mume kwa kukuzalia chema kikupacho raha maishani.....
wanaume jielezeeni hapa lol
 
do you think kwamba kuomba samahani ni kugalagaza p yako kwa mkeo? je unaamini hivyo? na je kupi kunakongeza p kukubali makosa kisha kuyarekebisha na kuomba samahan ama kutokubali kuomba samahani wakati iko wazi kabisa kwamba umekosea?

Binafsi siamini hivyo na ndo maana nimesema ni perception tu. Kwahiyo ushauri wangu kwa wanawake ni kwamba usilione hili kama shida sana kwani ni perception ya wanaume wengi tu (masculinity belief). Hata mimi nakumbuka before ilikuwa ngumu sana kutamka neno samahani kwa mke wangu, nilikuwa naona kama linakwama kwama vile kutoka kichwani mwangu, loh! Lakini natambua ilikuwa ni kwa sababu ya mtizamo huu wa wanaume wengi
 
so mbona nyie hata hiyo ya mjadala uishe hamna?
Kuna sababu mbili kubwa. Kwanza, we do realy care. You cant mend someone's broken heart kwa samahani ya juujuu tu, in fact you will end up breaking it more. Ndio maana, mwanamume anapoomba msamaha ujue kuwa it has come from the heart kwelikweli. Pili, always kuna njia nyingine za kuyamaliza hayo, hivyo si vema kutoa samahani ya bandia kwa sababu ina madhara makubwa huko mbele ya safari
 
wanaume wa jf mko wapi? tunawasubiri mtusaidie kwa nini samahani inakuwa ngumu kana jiwe?
ila mie naweza sema nina bahati naombwa msamaha pale anapokosea lol
wanaumee were r u?

Poor guy,umemkorogea la wapi makorora,kipatimo,mlingotini au la ujiji kwa kalumbanzira,au shuntama?
 
Binafsi siamini hivyo na ndo maana nimesema ni perception tu. Kwahiyo ushauri wangu kwa wanawake ni kwamba usilione hili kama shida sana kwani ni perception ya wanaume wengi tu (masculinity belief). Hata mimi nakumbuka before ilikuwa ngumu sana kutamka neno samahani kwa mke wangu, nilikuwa naona kama linakwama kwama vile kutoka kichwani mwangu, loh! Lakini natambua ilikuwa ni kwa sababu ya mtizamo huu wa wanaume wengi

aiasee! huu mtizamo huwa mnaupata wapi?
 
Back
Top Bottom