Wanaume tuacheni 'ubinafsi wa mapenzi'

Kwenye maandiko tunaambiwa "Mpingeni shetani naye atawakimbia", lakini kwenye uzinzi issue inakuwa tofauti sana, hatuambiwi "Ipingeni zinaa", tunaambiwa kabisa "IKIMBIENI ZINAA", na pia tunaambiwa " Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu"...ukianza kuleta swagga za kukemea uzinzi utajikuta imeshakucost.

Kila mtu anajijua jinsi anavyostruggle kwenye eneo hili, kazi si haba. Lakini pamoja na ugumu wote tunaouona, still hakuna justification ya cheating. Tena ukiwa Mcha Mungu ndo majaribu yanakufataje ili yakukomaze vizuri ( Tumesamehewa Dhambi na si Majaribu), na sio kama wapendwa hawaanguki, watu wanaanguka lakini wanatubu kwa kumaanisha na mwa neema ya Mungu wananyanyuka tena.

Tunachokikataa hapa ni ile mtu anazini afu anatafuta cheap justification eti " wanaume kucheat ni nature yetu" au mtu anakwambia eti bora wanaume tukicheat tunaleta tu maradhi, wanawake mtatuletea watoto haramu khaa. Hivi mnadhani wanawake hatupendi "varieties? Kumletea mwenzako maradhi ni kitu kidogo?
Mtu anafanya cheating as if ni haki yake ya msingi, kwamba by any means lazima atacheat. Dhambi tunafanya lakini tusijustify. Afu mbaya zaidi ni pale mtu anapoona ni sawa kwake yeye kufanya kitu fulani, ila akifanya mwingine ni dhambi isiyosameheka.

Afu tunapenda kweli kuwaonea walokole, mtu akisema/kukemea kitu fulani ambacho possibly hatupendi kukisikia.... utatusikia tu "huyu naye kujifanya mlokole/ huyu naye anatafuta tu sifa". In reality tunawaonea sana, kwa sababu wanachokiongea sio kwamba wamejitungia wao ili kutukomeshea sisi, nope... wanachokiongea ndicho exactly kilichopo kwenye Maandiko Matakatifu. Hata wakisema wanyamaze au sisi tuhalalalishe kitu fulani, haitobadili ukweli kuwa tutakuwa kinyume na maandiko. Mpendwa tuombe tu neema ya Mungu, bila hivyo hatuwezi chochote

Thanks for your input madam, umenigusa kwa kiasi kikubwa sana,
 
naweza kuwa na mke mmoja lakini siyo mwanamke mmoja

kuhusu mke kuchepuka achepuke tu lakini nisijue

(ole wake)ibaki hivi hivi
Umemaliza yote. Akichepuka ahakikishe hakamatwi akidakwa atajutraaa.
 
kwa andishi lako hili nahisi u njiani katika kulionja tamu la upande wa pili @nickyminaj. Japo ni lazima kumuomba Mungu lakini tunatakiwa akili zetu zifanyekazi yake kabla ya kuuhitaji msaada wa Mungu
kwamba nipo njiani kutoka nje? no thanks.. though mimi ni binadamu, nakubali am not perfect ibra, anything might happen ndo mana nasema kumtegemea Mungu kuna faida mno, mtu mwenye hofu ya Mungu anaweza kukabiliana na jaribu hilo. Hofu ya Mungu ikiwa ndani yako hata mawazo yako na akili zako vitafanya kazi kulingana na yeye..
 
kwamba nipo njiani kutoka nje? no thanks.. though mimi ni binadamu, nakubali am not perfect ibra, anything might happen ndo mana nasema kumtegemea Mungu kuna faida mno, mtu mwenye hofu ya Mungu anaweza kukabiliana na jaribu hilo. Hofu ya Mungu ikiwa ndani yako hata mawazo yako na akili zako vitafanya kazi kulingana na yeye..
nakubaliana kwa asilimia zote na wewe kuwa hofu ya Mungu ni silaha pekee ya kutulinda juu ya mawazo na akili Zetu.. Daima unapokuwa na hofu ya Mungu hata Matendo yako yatakuwa mfano mzuri kwa Jamii. Nampongeza mwanaume mwenzangu anayekumiliki
 
nakubaliana kwa asilimia zote na wewe kuwa hofu ya Mungu ni silaha pekee ya kutulinda juu ya mawazo na akili Zetu.. Daima unapokuwa na hofu ya Mungu hata Matendo yako yatakuwa mfano mzuri kwa Jamii. Nampongeza mwanaume mwenzangu anayekumiliki
hahaha aah jamani asante
 
Ni kweli wanaume kwenye hili ni wabinafsi waliopindukia namuunga mkono mtoa mada 100%
 
Hii ni topic pana sana, na inaweza isielezeke kwa maandishi, ni kitu unachoweza kukielewa pale unaposhiriki.

Kwamba mpaka uwe kwenye industry ndo unapoweza kujua nini kimetokea na sasa nini kifanyike. Naomba tu nireserve comment yangu. Mimi nimeoa, so naomba niwaachie mjadala huu.
Nakubaliana na wewe,nilimuuliza bro wangu mbona mke wako mzuri tena ana maadili mazuri tena unasema kumpata ilikua shida na unampenda sana lakini una michepuko na wanawake wengine kwanini?
Akanijibu kua mdogo wangu alafu uoe ndo utanielewa..

Nikagundua kwenye ndoa kuna vitu vingi vinavyotokea na kusababisha hivo.
 
Back
Top Bottom