Wanaume tuacheni 'ubinafsi wa mapenzi'

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,117
8,137
Wanaume (married or unmarried) ndo tunaongoza zaidi kwa kuchepuka na kugegeda nje, kuliko wanawake.

Ila tunapogundua kuwa wake zetu nao kumbe wanagawa nje, tunakuwa mbogo sana na kuzua timbwili zito. Is that fair? Ni ubinafsi.

Me nadhani tunawafanyia unfairness wake zetu. We kama unagonga nje, basi ruhusu pia na mkeo agongwe nje. Yes..., muosha huoshwa!!

Unageuka kuwa CIA wa 'nyendo' za mkeo wakati we mwenyewe umeinvest kwenye 'mbunye' tatu za ziada huko nje, na unazihudumia fully! Ni ubinafsi and unfairness.

Wewe kama ni 'mambo mengi' , basi usinune wala kumaindi unapogundua kuwa mkeo pia ni 'unga wa ngano'.

WHY nimeandika hivyo? Angalia true story ifuatayo:

Rafiki angu mmoja hivi, ni mambo mengi na ana michepuko miwili ambayo me mwenyewe naifahamu. Mke wake amekuwa akilalamika sana kuhusu 'uhuni' wa mumewe, na mara kadhaa nimesuluhisha migogoro kati yao.

Sasa jana jioni baada ya mishe za town, nikawa na washkaji tumekaa mahala 'uswazi' tunarelax na kupeana 'ramani' za jiji. Mada zilikuwa ni Siasa, Vijana tutoke vipi maisha haya, Kuzamia ng'ambo kwenda 'kuchukua maisha', Mademu vicheche wa mtaani kwetu ili tusije nasa kwenye grid ya Taifa kwa sarakasi zetu za kila siku, n.k. Mihogo ya kuchemsha na uji-ulezi wa mama 'ntilie ulikuwa ukisindikiza 'kikao' chetu jioni hiyo kijua kinaanza kuzama.

Mara ghafula, tukasikia zogo kubwa sana mtaa wa pili huku wananchi wakimiminika kuelekea eneo la tukio. Tukahisi tayari mwizi keshaingia kumi na nane huko, fasta sana tukanyanyuka na vikombe vyetu nkononi kuelekea eneo la tukio ili tukamthibiti mwizi by R.I.P endorsement! Maana huku 'site' kwetu wezi na walozi ndo MAADUI zetu nambari one ambao wanatunyima usingizi, na tumeshawawekea WANTED ya maisha. Wale maadui watatu wa kitaifa (ujinga, maradhi, umasikini) tumeshawazoea na tushaamua kuishi nao tu kama 'good neighbors' na maisha yanasonga.

Ile kufika kwenye tukio, kumbe sio mwizi bhana. Ni babu mmoja ivi (mtu mzima ovyo) wa pale mtaani. Babu kadakwa kwenye uchochoro anapiga 'chabo' kwenye dirisha la jamaa mmoja ivi na mkewe walohamia kitaani recently. Babu katulizwa chini na wahuni wa mtaa anachezea makofi. Mtaa umefunga utadhani kuna 'shuhuli' ya kumtoa mwali. Akina mama wenye 'screen za chogo' wamevaa kanga-moko na 'utamu' unaonekana transparently, wanapayuka na kucheka kishankupe wakipunga vidole juu. Daaah uswazini ni kutamu jamani. hahaha

Wananchi wanasema babu hiyo ndo tabia yake. Huwa giza likiingia tu anaanza 'ziara za kustukiza' dirisha kwa dirisha zilizopo chochoroni ili 'ale deo' live. Wanasema babu keshadakwa mara nyingi tu, mpaka mke wa babu aliamua kuondoka kwao baada ya fedheha hizo. Basi tukacheka sana na kuenjoy zengwe za uswahilini, na tukaanza kurudi kwenye 'maskani' yetu.

Tukiwa njiani, ndo nakutana na yule rafiki angu mwenye michepuko miwili, anatoka job. Hana furaha kama nilivyomzoea. Anaonekana kabsa yupo off mood. Nikamuuliza vipi kiongozi, mbona dizaini kama haupo sawa? Nikamjoke: unaonekana una mawazo wakati hudaiwi ata kodi ya chumba, nini tatizo? (huyu mwana kwao ni njema kiaina, familia bora a.k.a msosi wa drafti. Siku ya harusi yake, wazazi wake walimzawadia nyumba nzima iliyopo huku 'uswazini' ili aanzie maisha. So hajuwi adha za kupanga chumba/nyumba).

Basi ndo akaanza kutiririka yale yanayomnyima amani ya moyo. Anasema kwamba mke wake kabadilika sana kitabia tofauti na siku za nyuma. Anadai kuwa mkewe kaanza kuugawa 'mzinga wa asali' nje, washika dau wasiojulikana tayari weshaanza 'kuupakua' bila hiana, na inamuuma sana!!

Swali la kwanza nilomuuliza... Je una uhakika gani kuwa shemeji kaanza kugawa nje, au una hisi tu? Akanijibu kuwa baada ya kuanza kudetect behavioral change kwa mkewe, ameanza kumfanyia 'udukuzi' wa kina kwenye nyendo zake za kila siku, na ameconfirm kabsa kuwa now mkewe anagegedwa nje.

Swali la pili nilomuuliza .... Hivi wale mademu zako michepuko, bado upo nao? Akanijibu hivi: ''Aaarg wale nipo nao mguu ndani mguu nje. Afu uyo mmoja nae ananizingua tu''

Swali la tatu nilomuuliza.... Hivi mkuu, wewe una michepuko miwili, na mkeo alishalalamika sana kuhusu hiyo tabia yako, so WHY hutaki yeye agongwe nje? WHY wewe inakuuma sana yeye kugawa mbunye nje?

Jamaa akakosa jibu. Akawa speechless for some seconds, akainamisha kichwa dizaini kama ana-double-click his folder of thinking. Then akaaga anaenda kulala !

Mie nikarudi zangu kijiweni kwa majobless wenzagu tukaendelea 'kuielewa mitaa' huku tunakamatia kitu 'wali nazi' cha mama ntilie aliepo hapo jirani.

MY TAKE:

Wanaume tuacheni ubinafsi katika mahusiano ya kimapenzi. Wanawake nao wana mioyo ya nyama kama sisi. Otherwise We should heed to the compliance of the principle of social justice in order to smoothen things progressively in our encounters ... 'Treat others the way you like to be treated'.

Kuruka ruka sio dawa ya urimbo.


- Kaveli -
 
Mleta mada ni mtu mpumbavu kabisa kwasababu mpumbavu ni mtu asiyeweza kuelewa chochote! Hata vitabu vya dini vimekushinda kuvielewa!

Mfalme Suleiman alikuwa na wake 700, na ipo hadithi kwenye Biblia juu ya mwanamke aliyepelekwa kwa Yesu kwa kosa la kuzini, ulishawahi kujiuliza ni kwanini alipelekwa mwanamke tu wakati kuna mwanaume aliyezini nae?!

Waislamu wanaoa mpaka wanawake wanne, upo hapo?
Jamii mbalimbali wanaume wanaoa wanawake zaidi ya mmoja, upo?
Sasa ni wapi mwanamke aliolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja?

Nikupe tu summary:
Mwanaume akitoka nje ya ndoa athari kubwa ni moja tu ya kupata magonjwa. Mwanamke akifanya hivyo ataleta magonjwa na mitoto haramu kibao huku wewe ukiilea na kujua ni yako!

Ndo maana papuchi ilifichwa mbali sana kuliko dushe!
 
Mleta mada ni mtu mpumbavu kabisa kwasababu mpumbavu ni mtu asiyeweza kuelewa chochote! Hata vitabu vya dini vimekushinda kuvielewa!

Mfalme Suleiman alikuwa na wake 700, na ipo hadithi kwenye Biblia juu ya mwanamke aliyepelekwa kwa Yesu kwa kosa la kuzini, ulishawahi kujiuliza ni kwanini alipelekwa mwanamke tu wakati kuna mwanaume aliyezini nae?!

Waislamu wanaoa mpaka wanawake wanne, upo hapo?
Jamii mbalimbali wanaume wanaoa wanawake zaidi ya mmoja, upo?
Sasa ni wapi mwanamke aliolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja?

Nikupe tu summary:
Mwanaume akitoka nje ya ndoa athari kubwa ni moja tu ya kupata magonjwa. Mwanamke akifanya hivyo ataleta magonjwa na mitoto haramu kibao huku wewe ukiilea na kujua ni yako!

Ndo maana papuchi ilifichwa mbali sana kuliko dushe!
mkuu kwa Povu hili, inaonekana wewe ni mkurugenzi mtendaji katika sekta ya mipango ya kando
 
naweza kuwa na mke mmoja lakini siyo mwanamke mmoja

kuhusu mke kuchepuka achepuke tu lakini nisijue

(ole wake)ibaki hivi hivi
 
Back
Top Bottom