Wanaume tuacheni 'ubinafsi wa mapenzi'

Mleta mada ni mtu mpumbavu kabisa kwasababu mpumbavu ni mtu asiyeweza kuelewa chochote! Hata vitabu vya dini vimekushinda kuvielewa!

Mfalme Suleiman alikuwa na wake 700, na ipo hadithi kwenye Biblia juu ya mwanamke aliyepelekwa kwa Yesu kwa kosa la kuzini, ulishawahi kujiuliza ni kwanini alipelekwa mwanamke tu wakati kuna mwanaume aliyezini nae?!

Waislamu wanaoa mpaka wanawake wanne, upo hapo?
Jamii mbalimbali wanaume wanaoa wanawake zaidi ya mmoja, upo?
Sasa ni wapi mwanamke aliolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja?

Nikupe tu summary:
Mwanaume akitoka nje ya ndoa athari kubwa ni moja tu ya kupata magonjwa. Mwanamke akifanya hivyo ataleta magonjwa na mitoto haramu kibao huku wewe ukiilea na kujua ni yako!

Ndo maana papuchi ilifichwa mbali sana kuliko dushe!

Siku zote mtu kutokwa povu la omo mdomoni pasipo sababu ya msingi, huwa ni ishara ya mambo mawili: (1) Domo limevunda, (2) Mimba changa.

As such, ngoja nikuletee udongo na limao ulambe lambe.

Back to topic:

Kweli umeshindwa kabsa kuielewa 'thematic area' ya uzi wangu? Basi wewe ni taahira la karne. Ebu soma michango ya wengine walioielewa mada, ndo utajiona jinsi ulivyo 'pumbavu' next levo.

Na kama unashindwa kutofautisha kati ya 'Kuchepuka' na 'Kuongeza mke mwingine' basi wewe ni mpumbavu to the maximum!

By the way, nani kakwambia kuwa hiyo ndoa ya Jamaa ni ya kiislam ????

Endelea kutetea 'uchepukaji' .

- Kaveli -
 
Hahahaa dada'ake. Maneno kuntu yanayomfanya mwanaume awe 'mpole' utadhani mtu alopoteza nauli katikati ya jiji. Ni ukweli mchungu kwetu wanaume... mvamizi kavamiwa!
Maneno yanayomfanya hata dushe ikose ujasiri wa kusimama
 
Em tupe kidogo "reality" ambayo wewe umeiona

Hii ni topic pana sana, na inaweza isielezeke kwa maandishi, ni kitu unachoweza kukielewa pale unaposhiriki.

Kwamba mpaka uwe kwenye industry ndo unapoweza kujua nini kimetokea na sasa nini kifanyike. Naomba tu nireserve comment yangu. Mimi nimeoa, so naomba niwaachie mjadala huu.
 
Mpendwa whether married or not, wote tunahitaji neema ya Mungu ili tusichepuke. Aisee bila hofu ya Mungu, hili suala ni gumu mno na hamna justification ya kucheat
 
Mkuu, sometimes kuzielewa DO's na DONT's za mchezo sio lazima uwe 'mchezaji' .

Pili, wew kama mwanaume na umeoa, siamini kama kweli hutambui kabsa madhara ya kuchepuka!

Tatu, naposoma mwandiko wako, ni kama unajaribu kutoa 'justification' ya kuchepuka!

Mkuu, stick to the code of conduct ya ndoa. Comply with the commandments za ndoa. Tuacheni 'cheap' justifications hapa.

Otherwise, tusiwe tunawalaumu wanawake wakishachange kitabia baada ya mwanaume kuwa 'nunda' ndani ya ndoa.

-Kaveli-
 
sijawahi kucheat hata kuwaza tu sijawahi for me cheating isn't worth it.. ila haya mambo haya kikubwa ni kumuomba Mungu tu kwa akili zetu hatutaweza
kwa andishi lako hili nahisi u njiani katika kulionja tamu la upande wa pili @nickyminaj. Japo ni lazima kumuomba Mungu lakini tunatakiwa akili zetu zifanyekazi yake kabla ya kuuhitaji msaada wa Mungu
 
Mpendwa whether married or not, wote tunahitaji neema ya Mungu ili tusichepuke. Aisee bila hofu ya Mungu, hili suala ni gumu mno na hamna justification ya kucheat

Maneno kuntu! Naona mdau anataka kutoa 'cheap' justification ya kuchepuka.
 
sio hivyo dada, ninachosemea mimi ni kwamba si ruhusa kwangu wala kwake kwa kukuwa sambusa ni ile ile na Utamu ndio ule ule
hapana sambusa zipo za nyama na za viazi, nyingine zina pilipili nyingine zina kotmiri...
 
Hili ni gumu kukubalika.. Mwanaume hata akicheat haimletei picha mbaya bali huongeza muonekano wa Ulijali wake.

Na ndio maana inapotokea la kufumanina mwanamke ndio huonekana mkosefu kwa kuwa ki kawaida inachukuliwa na mwanamke ni kama kioo cha familia na Anapokubali kucheat kwa sababu eti mwanaume anacheat ni doa ambalo halifutiki katika ndoa na maisha yake iwapo utagundulika.

Siku zote licha ya Kumuona mwanamke ni Dhaifu hawezi kitu lakini ukweli usiofichika ni Kwamba mwanamke anachukua sehemu kubwa katika familia na Maisha ya ndoa. Kwahiyo hata kwa upande wake mpaka kufikia kucheat ujue imemchukua Muda mrefu sana.

Kaveli inawezekana utafiti na ule uthubutu wa kuandika bandiko hili umeuchukua juu kwa juu hasa kutokana na Aina ya Wanawake waliopo kwasasa.

Wanawake wa Miaka Hii kabla hajasalitiwa yeye tayari ana wawili, ukija kuanza wewe yeye tayari anatimu nzima ya Mpira.

Kwahiyo katika Kuthamini na Kuheshimu nguvu ya mwanamke kwenye jamii na familia zetu naomba kupingana na wewe katika Hili kuwa unawatafutia matatizo wanawake katika ndoa Zao..

Huwatakii mema katika uhuru na raha za kuaminika katika ndoa zao.

Hutambui kuwa mambo yanapo haribika mwanamke ndio huumia na kuteseka ikiwemo kuonekana kicheche kwa ndugu na Jamaa.

Kurudishwa kwa wazazi wake huku familia yao ikiwa haijiwezi na ilikuwa tegemezi kwa mwanaume husika.

Zipo athari nyingi kwa mwanamke iwapo atakubaliana na Andiko lako otherwise awe anajiweza kiuchumi.
 
Mkuu, sometimes kuzielewa DO's na DONT's za mchezo sio lazima uwe 'mchezaji' .

Pili, wew kama mwanaume na umeoa, siamini kama kweli hutambui kabsa madhara ya kuchepuka!

Tatu, naposoma mwandiko wako, ni kama unajaribu kutoa 'justification' ya kuchepuka!

Mkuu, stick to the code of conduct ya ndoa. Comply with the commandments za ndoa. Tuacheni 'cheap' justifications hapa.

Otherwise, tusiwe tunawalaumu wanawake wakishachange kitabia baada ya mwanaume kuwa 'nunda' ndani ya ndoa.

-Kaveli-

Mkuu siyo kweli kwamba nafanya justification,

Humu ndani walokole ni wengi na mara nyingi sote tunajaribu kuandika maandishi ya kilokole, in an ideal world unachozungumza ni sawa, practically issues ni tofauti.

All in all, ndoa ni nzuri sana mkiishi kwenye misingi.

Cool.
 
hapana sambusa zipo za nyama na za viazi, nyingine zina pilipili nyingine zina kotmiri...
lakini mshindo na Ile sukari uisikiayo wakati wa kufika safari yako ni ule ule pia kumbuka na kutambua kuwa Halua haina makombo mkwe
 
Mwanaume anaoa/kuwa na wake wengi ila sio mwanamke kuolewa/kuwa na wanaume wengi
 
Mkuu siyo kweli kwamba nafanya justification,

Humu ndani walokole ni wengi na mara nyingi sote tunajaribu kuandika maandishi ya kilokole, in an ideal world unachozungumza ni sawa, practically issues ni tofauti.

All in all, ndoa ni nzuri sana mkiishi kwenye misingi.

Cool.

Kwenye maandiko tunaambiwa "Mpingeni shetani naye atawakimbia", lakini kwenye uzinzi issue inakuwa tofauti sana, hatuambiwi "Ipingeni zinaa", tunaambiwa kabisa "IKIMBIENI ZINAA", na pia tunaambiwa " Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu"...ukianza kuleta swagga za kukemea uzinzi utajikuta imeshakucost.

Kila mtu anajijua jinsi anavyostruggle kwenye eneo hili, kazi si haba. Lakini pamoja na ugumu wote tunaouona, still hakuna justification ya cheating. Tena ukiwa Mcha Mungu ndo majaribu yanakufataje ili yakukomaze vizuri ( Tumesamehewa Dhambi na si Majaribu), na sio kama wapendwa hawaanguki, watu wanaanguka lakini wanatubu kwa kumaanisha na mwa neema ya Mungu wananyanyuka tena.

Tunachokikataa hapa ni ile mtu anazini afu anatafuta cheap justification eti " wanaume kucheat ni nature yetu" au mtu anakwambia eti bora wanaume tukicheat tunaleta tu maradhi, wanawake mtatuletea watoto haramu khaa. Hivi mnadhani wanawake hatupendi "varieties? Kumletea mwenzako maradhi ni kitu kidogo?
Mtu anafanya cheating as if ni haki yake ya msingi, kwamba by any means lazima atacheat. Dhambi tunafanya lakini tusijustify. Afu mbaya zaidi ni pale mtu anapoona ni sawa kwake yeye kufanya kitu fulani, ila akifanya mwingine ni dhambi isiyosameheka.

Afu tunapenda kweli kuwaonea walokole, mtu akisema/kukemea kitu fulani ambacho possibly hatupendi kukisikia.... utatusikia tu "huyu naye kujifanya mlokole/ huyu naye anatafuta tu sifa". In reality tunawaonea sana, kwa sababu wanachokiongea sio kwamba wamejitungia wao ili kutukomeshea sisi, nope... wanachokiongea ndicho exactly kilichopo kwenye Maandiko Matakatifu. Hata wakisema wanyamaze au sisi tuhalalalishe kitu fulani, haitobadili ukweli kuwa tutakuwa kinyume na maandiko. Mpendwa tuombe tu neema ya Mungu, bila hivyo hatuwezi chochote
 
Back
Top Bottom