Wanaume naomba ushauri wenu make mume wangu simuelewi

dagaa

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
290
379
habari zenu wapendwa
mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 5 na nina mume wangu wa ndoa zaidi ya miaka sita. ila mume wangu simwelewi kitu kimoja inafika kipindi akaninunia na asikwambie sababu na ukimuuliza nini mbaya unaweeza ukalamba
hata vibao. si mara moja ili swala kujitokeza ndo mana nimeona nilete jamvini. na anakuwa na majibu ya mkato na hasira endapo nitamuuliza kitu. yani nakuwa sina thamani kwake. na naweza nikawa nyumbani na apigi kwa simu yangu anapiga ya dada na anaweza sa nyingine akarudi usiku wa manane na yupo chakali. sasa na jiuliza uu ni ugonjwa ama pepo. akiwa ajaninunia yupp sawa na ni mume mwema. ila haiwezi pita miezi 3 ajaninunia.

je mnahisi ana tatizo gani? mi nampenda sana mume wangu. ila kama binadamu akiwaga na khali hiyo nami uwa naumia mpaka sa nyingine nawaza yasiyo wazika.
 
Mumeo anafanya kazi gani? Tuanzie hapo kwanza maana kuna kazi ni balaa!
 
Nahisi ana ka bibi mdogo mtaani(MCHEPUKO) but jaribu kukaa nae hasa akiwa na furaha umuulize kinachomsibu mpaka anakosa raha na kununa baadhi ya cku
 
watu wengine wapo hivyo,first hypothesis.yaani wanajisikia kununa tu bila sababu na mara nyingi watu wa aina hii hurudi sawa bila kubembelezwa au kuliwazwa na mtu mwingine.sindano huchomokea ilipoingilia hivyo akinuna mwenyewe basi yeye mwenyewe atajiweka sawa.mara nyingi huwa hawapendi kuulizwa kwa nini yuko hivyo kwani yawezekana jibu akawa hana.

swala la pili inawezekana wewe ndiye tatizo.ikiwa mumeo anawivu jaribu kuangalia mavazi yako,ukaribu wako na wanaume wengine pamoja na kmjali.
 
Maisha tu dada..hiyo ndio ndoa ww akiwa amenuna usimuulize jikaze mpk hasira zikiisha endelea na maisha.
 
Yawezeka na akawa na tatizo la kisaikolojia huenda kuna mambo yanamsumbua lakini hataki kusema. Ebu nikuulize,je, uliwahi kumuuliza kuhusu suala hilo wakati anapokuwa katika hali nzuri ? Kama umewahi kumuuliza alijibuje? Kama hujawahi, muulize maana wakati wa amani ndio muda muafaka wa kuchimbua chanzo cha tatizo.
Ikibidi waulize hata wazazi wake au ndugu yeyote wa karibu huenda mumeo akawa na tatizo ambalo watu wa karibu wanalijua.
 
atakuwa anastress za maisha huyo hivyo kisaikolojia hayuko sawa, ni vema ukaongea nae kimahaba nini tatizo...kaa nae pindi anapojirud na kuonekana mwenye furaha!!!!
 
Mumeo ana tatizo linamtatiza

Lakini hajui namna ya kulitatua,namna anayotumia kukabiliana na tatizo lake sio nzuri kwani anaongeza tatizo badala ya kulitatua

Cha kufanya:
Jaribu kuwa mpole sana kwake na muoneshe kumjali na upendo mkubwa hilo litamfanya atulize mihemko aliyonayo,wakatio ukifanya hayo jaribu kukagua shughuli zake na jitahidi kuwa karibu nae na mpe moyo kwenye yale anayofanya,kitendo hicho kitamfanya akuone kama msaada sana kwake na itafikia mahali atakuambia yanayomsibu

Kuwa nae karibu na kuonesha kumjali na mapenzi makubwa kutamfanya akuone mke mpya kwake na kutamfanya ajisogeze karibu sana na wewe,huyo anaonekana anahitaji liwazo na mahali pa kutolea dukuduku lake na hata msaada wa kimawazo na ushauri,ukimfanyia hayo atakuona msaada sana na atakuambia yanayomsibu

Asipokuambia tafuta siku ambayo atamuona ana furaha kisha kwa upendo na utulivu muulize na kama hataonekana kuwa muwazi mwache na tafuta siku nyingine tena umuulize,endelea hivyo na hatimae atakuja kukuambia kinachomsumbua na kukijua ni hatua moja muhimu ya kuendea utatuzi

Akisha kuambia basi kuwa nae bega kwa bega kutafuta suluhu!
 
Kuna watu wakiwa na stress hawapendagi kuulizwa kulikoni.

Na wewe kwa vile unampenda inakuuma ukimuona vile ndio maana unamuuliza.

Next time just try to keep your distance, uone kama hali itabadilika.
 
Mumeo ana tatizo linamtatiza

Lakini hajui namna ya kulitatua,namna anayotumia kukabiliana na tatizo lake sio nzuri kwani anaongeza tatizo badala ya kulitatua

Cha kufanya:
Jaribu kuwa mpole sana kwake na muoneshe kumjali na upendo mkubwa hilo litamfanya atulize mihemko aliyonayo,wakatio ukifanya hayo jaribu kukagua shughuli zake na jitahidi kuwa karibu nae na mpe moyo kwenye yale anayofanya,kitendo hicho kitamfanya akuone kama msaada sana kwake na itafikia mahali atakuambia yanayomsibu

Kuwa nae karibu na kuonesha kumjali na mapenzi makubwa kutamfanya akuone mke mpya kwake na kutamfanya ajisogeze karibu sana na wewe,huyo anaonekana anahitaji liwazo na mahali pa kutolea dukuduku lake na hata msaada wa kimawazo na ushauri,ukimfanyia hayo atakuona msaada sana na atakuambia yanayomsibu

Asipokuambia tafuta siku ambayo atamuona ana furaha kisha kwa upendo na utulivu muulize na kama hataonekana kuwa muwazi mwache na tafuta siku nyingine tena umuulize,endelea hivyo na hatimae atakuja kukuambia kinachomsumbua na kukijua ni hatua moja muhimu ya kuendea utatuzi

Akisha kuambia basi kuwa nae bega kwa bega kutafuta suluhu!

asante sana kwa ushauri wako mpendwa... japo nimeshajaribu njia hiyoila khali inaendelea kujitokeza we fikilia miaka yote khali hiyo inakuwa inamtokea.... mpaka nami akiwa amenuna siangaiki nae naumia tu..
 
We nawe mpe nafasi kununa kukiisha endelea naye! Unadhani kuna binadamu atakuwa anacheka muda wote?
Zingine ni sababu za kukosa hela, zingine ni kumwagwa na michepuko au kuifumania! Zingine ni stress za kazi na ups & downs za maisha!
Well said Cyan6
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom