Dejane
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 49,697
- 68,707
Kila mara mnalalamika na kufungua nyuzi za kusema wanawake wanapenda watu wenye pesa na uwezo mkubwa,nimekuwa nikiangalia kuna watu kama watatu wana uwezo kipesa na kiuchumi wapo Poa ,ni wale wanaume anakuoa unakaa nyumban tu kila kitu kitaletwa unachotaka utapata na hata ikitokea wamekufa wana makampuni yashakuwa makubwa utatunzwa .lakin hao wanaume watatu tofauti nnaowafaham vyema wake zao waliwakimbia na sio mmoja walioa wakaenda wakaongeza tena wamekimbiwa tena ,unajiuliza hawa wanakosa nin mpaka wanakimbia na mahitaji wanapata kila kitu wakati huku kuna wanawake wameolewa na wanaume bado wanajitafuta na hawatoki kwa ndoa zao,au uhuru hakuna maana ile ya kuletewa kila kitu ndani hakuna mashoga na kuzurura labda wanahitaji .huwa najiuliza sana wakati wadada wanasaka mabwana matajiri wengine wanawakimbia
Basi kuna kitu zaidi ya pesa wanawake wanahitaji au mnasemaje?maana wengine waachwa kwa ufukara wao ,wengine wanazo wanakimbiwa.
Nin shida 🫣
Basi kuna kitu zaidi ya pesa wanawake wanahitaji au mnasemaje?maana wengine waachwa kwa ufukara wao ,wengine wanazo wanakimbiwa.
Nin shida 🫣