Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 74,555
- 115,629
Hahaa,Ila wamezalisha vya kutosha mkuu. Yaan mkuu kubali kataa ila madingi yalikua yanaanzisha familia kwa lengle la kuzalisha ndio maana yalikua yanammaindi sana mke anaezaa watoto wa kike tu bila kujali tatizo ni yy au mke. Familia kubwa ndio ilikua na nguvu kiuchumi enzi hizo
Umenikumbusha kitabu fulani cha miaka ya sabini, cha maisha ya Nyerere.
Sasa yule muandishi alifanya kazi nzuri sana ya kuielezea jamii ya Kizanaki na tamaduni zao, kabla hata hajaanza kumuelezea J.K Nyerere mwenyewe, ili upate kujua Nyerere alitokea jamii gani na maisha yake yalianza kwa mafunzo gani.
Katika kuielezea ile jamii, alielezea ndoa, akasema kuoa wake wengi ilikuwa kitu cha kawaida kabisa, kwa sababu ilikuwa ni njia rahisi ya kuongeza familia iwe kubwa. Na ikitokea mke akaleta wivu au kukataa wake wenza, alionekana mtu wa ajabu kabisa asiyependa maendeleo ya familia.
So, ulivyosema ni kweli kwamba walikuwa wanazidisha nguvukazi ya familia. Na familia kubwa ndiyo ilikuwa fahari.
Unaambiwa baba yake J.K Nyerere alikuwa na wake 22 huko, yani kama anakuwa nao wote pamoja, akikaa kwa mke mmoja wiki mbili harudii mke karibu mwaka mzima.
Hapo lazima asaidiwe tu, maana hamna jinsi!