Wanasiasa waliowania nafasi za Urais mara nyingi na kushindwa zote Barani Afrika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
1. Raila Odinga (KE): Amewania mara ya 5 na kuangushwa zote

Odinga, mwanasiasa mkonge na mpinzani wa muda mrefu alikuwa anaungwa mkono na Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta ambaye pia ni mtoto wa rais wa kwanza wa taifa hilo, hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Lakini hili si jaribio la kwanza la kuutaka urais kwa Bwana Odinga anayetajwa kama baba wa demokrasia kwenye taifa hilo. Akiwa na miaka 77 sasa hii ilikuwa mara ya 5 sasa na mara zote ameangushwa, kama ilivyokuwa kwa baba yake, Jaramogi Oginga Odinga, ambaye pamoja na juhudi kubwa alizofanya dhidi ya ukoloni wa waingereza, lakini hakufanikiwa kuwa rais.

Ingawa awali alisema uchaguzi wa mwaka huu 2022 litakuwa jaribio la mwisho kwake, lakini baada ya Mahakama kuthibitisha ushindi wa Ruto aliandika katika mtandao wake wa twitter kwamba anaheshimu uamuzi wa Mahakama lakini hakubaliani nao.

2. Profesa Ibrahim Lipumba (TZ): Amewania Urais mara 4
Ni mchumi na mmoja wa wanasiasa wa upinzani wa muda mrefu nchini Tanzania, akikiongza chama cha CUF tangu mwaka 1995, kabla ya kutofautiana na katibu wake Mkuu, Maalim Seif mwaka 2015 alipojiuzulu lakini akarejea tena kwenye nafasi hiyo anayoishika mpaka sasa.

Amewania urais mara nne, tangu mfumo wa vyama vingi uanze Tanzania katika miaka ya 1990 na mara mbili alishika nafasi ya pili. Katika uchaguzi mkuu wa 1995, alikuwa wa tatu, Uchaguzi wa 2000 alishika nafasi ya pili nyuma ya Hayati Benjamin Mkapa wa CCM aliyekuwa madarakani.

Akajitosa tena katika uchaguzi wa 2005, na kushika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 11.68% ya kura nyuma ya Jakaya Kikwete. Uchaguzi wa 2010 akashika nafasi ya 3 nyuma ya Kikwete tena akipata asilimia 8.3% ya kura. Umaarufu wake umetetereka katika miaka ya hivi karibuni, na kukomaa kwa chama kingine cha upinzani cha CHADEMA na ACT- Wazalendo, kumezidi kumuweka mbali na harakati za urais.

3. Warren Kizza Besigye Kifefe (Uganda): Amewania Urais Mara 4
Amewania kuanzia Uchaguzi wa Mwaka 2001, 2006, 2011, na 2016 na mara zote akiangushwa na Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye amekuwa Rais wa #Uganda tangu Januari 26, 1986

Ni mmoja wa wanasiasa wa upinzani waliokumbana na 'kasheshe' nyingi kutoka utawala wa Yoweri Museveni mwenye miaka umri wa 77.

Japokuwa katika uchaguzi uliopita wa Januari, 2021 hakuwania urais, alimuunga mkono Bobi Wine ambaye aliangushwa pia na Museveni aliyekuwa anawania urais kwa mara ya 6 na anayekwenda kutawala Uganda kwa miaka 40.

4. Morgan Tsvangirai (Zimbabwe): Amewania Urais mara 3
Kama kuna mwanasiasa Zimbabwe aliyethubutu 'kumsumbua' kisiasa Mwanasiasa aliyekaa madarakani kwa muda mrefu, Robert Mugabe basi ni Morgan Tsvangirai. Uchaguzi wa 2002 alipata asilimia 42% ya kura dhidi ya 55.2% za Mugabe aliyekuwa anapeperusha bendera ya chama cha ZANU-PF na kutengeneza nguvu kubwa ya upinzani kupitia chama chake cha MDC.

Tsvangirai alikaribia kushinda urais katika uchaguzi wa mwaka 2008 alipopata asilimia 47.9% ya kura dhidi ya 43.2% za Mugabe, ambazo zilipelekea kuwepo kwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Juni 27, 2008.

Hata hivyo Tsvangirai alisema alishinda uchaguzi huo kwa asilimia kubwa ambazo hukupaswa kuwepo kwa marejeo. Kukazuka ghasia kubwa na baadaye aliamua kujitoa Juni 22, 2008, wiki moja kabla ya siku ya kupiga kura. Mugabe akaenda kushinda kwa zaidi ya asilimia 90%.

Uchaguzi wa 2013 alipata asilimia 34.3% dhidi ya 61.8% za Mugabe, Tsvangirai alikataa matokeo na katika kusaidia kuleta utulivu, iliundwa Serikali ya Umoja wa kitaifa akawa Waziri mkuu chini ya utawala wa Mugabe kati ya mwaka 2009 -2013.

5. Seif Sharif Hamad - Zanzibar: Amewania mara 6 hadi kufikia 2020
Baada ya kuwa Waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa miaka 4 na kushika nafasi mbalimbali katika utawala wa CCM, baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania, Maalim aliondoka na baadhi ya wana CCM na kwenda kuanzisha chama cha CUF na kuwania urais wa Zanzibar mwaka 1995.

Akashindwa na Mgombea wa CCM, Salmin Amour aliyeshinda kwa asilimia 49.76% dhidi ya 50.24% za Maalim. CUF ilikataa matokeo. Akawania tena urais wa visiwa hivyo mwaka 2000 akabwagwa na Amani Karume, kukatokea ghasia zilizopelekea vifo vya watu kadhaa.

Akajaribu tena mwaka 2005 akabwagwa na Karume na mara ya tano akajitosa mwaka 2010 dhidi ya Dr Shein akashindwa.

Mwaka 2015 uchaguzi ulifutwa na mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Zanzibar, Salim Jecha kwa sababu ya kujaa kasoro katika wakati ambao upande wa maalim Seif ulidai kushinda wazi.

Na uliporudiwa mwezi Machi 2016, Maalim Seif aligoma kushiriki tena uchaguzi na kumfanya Dr Shein kuendelea kushika kiti cha urais.
 
A. Mrema alianza kupambania mwaka 1995, akaendelea mwaka 2000,...
R.I.P Mpambanaji
 
Hii si maana halisi ya DEMOKRASIA YA MAGHARIBI ambayo eti nasi waafrika ni "wafuasi" wake. Wenzetu wenye demokrasia yao akishindwa mara moja tu anatafuta hamsini zingine, si kulazimisha uongozi
 
Sababu huko mtu anashinda kihalali tatizo huku huwezi sema Besigye alishindwa 2007 au Tsvangirai hakushinda Urais 2008!! Hizo Ndio hupelekea wagombee tena na tena maana wanaamini wakishinda ila waliibiwa.

NB: Mtoa mada ukimtoa lipumba hao wengine wote walikua wakishinda ila wanaporwa ushindi so hiyo heading Yako ni misleading kidogo.

Mfano Tsvangirai alishinda 2008 raundi ya kwanza though hakufika 50% so ikabidi waende round 2 sasa hapo kivipi "alishindwa"?

Maalim alishinda wazi kabisa 2015 ila uchaguzi baadae ukafutwa sasa kivipi unasema hakuwahi shinda?

Same to Odinga alishinda 2007 ila Kibaki aliapishwa kwa mabavu how ameshindwa?
 
Yote uliyosema Ni kweli kbsa vzr sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Aisee umekuja na fact nzuri san good thing Ni kwamab watu wote wanalijuwa hilo

Back
Top Bottom