Wanasiasa wakipiga magoti na kulia mbele zetu tuwahurumie?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,398
1,265
Team,

Salaam!

Nimeona video moja ya Naibu Waziri anayehudumia akitokea mkoa wa Kagera akiwa ktk mkutano amepiga magoti na kuanza kutoa hotuba huku akilia machozi kama mtoto mdogo.

Sasa nachouliza kwa Naibu Waziri huyu mpaka anapiga magoti mbele ya umma wa watu waliohudhuria mkutano wake kuna tatizo gani linalomsokota kisiasa?

Wakilia tuwahurumie na kuwarudisha madarakani?

Mnaoota kuwa Wanasiasa na pengine kuwa wabunge jifunzeni kutonenepesha mifugo wkt wa kuingia mnadani - huenda mkawa mmechelewa sana.

Lkn kwa upande wa vyama epukeni dhambi ya kurudisha majina ya wagombea ambao wameanguka ktk kura za maoni - kufanya hivyo ni kujiandalia upinzani hata kabla ya safari kufika.

Ovaaaa!
 
Team,

Salaam!

Nimeona video moja ya Naibu Waziri anayehudumia akitokea mkoa wa Kagera akiwa ktk mkutano amepiga magoti na kuanza kutoa hotuba huku akilia machozi kama mtoto mdogo...
Wakiinuka toka walipopiga magoti wanatunyea viganjani
 
Team,

Salaam!

Nimeona video moja ya Naibu Waziri anayehudumia akitokea mkoa wa Kagera akiwa ktk mkutano amepiga magoti na kuanza kutoa hotuba huku akilia machozi kama mtoto mdogo...
Wanaolia wengi ni wale ambao majimbo yao yana shabikia wapinzani na wanajua hawataweza kushinda kuanzia Mara, Arusha, Mbeya, Bukoba.... matatizo yako hapo
 
Team,

Salaam!

Nimeona video moja ya Naibu Waziri anayehudumia akitokea mkoa wa Kagera akiwa ktk mkutano amepiga magoti na kuanza kutoa hotuba huku akilia machozi kama mtoto mdogo...
Ni Mwana CCM mwanzako na kutoka Kakonko mpaka Bukoba Mjini sio mbali,nenda mtafute na umuulize kilichokuwa kinamliza ni kipi
 
Team,

Salaam!

Nimeona video moja ya Naibu Waziri anayehudumia akitokea mkoa wa Kagera akiwa ktk mkutano amepiga magoti na kuanza kutoa hotuba huku akilia machozi kama mtoto mdogo...
Umhurumie nini mwanaume analialia mbele za wanawake, wakati anaweka kibindoni milioni 12 kila mwisho wa mwezi?huyo amekosa ujasiri ni kumweka pembeni. Hata hanawake huwa hawalii vile mbele za watu. anajifanya ana uchungu sana na bukoba?

Kwanza pale bukoba sio nchi ya wahaya, ni ya Watanzania na pale kuna kabila zote, ilikuwaje aanze kuongea kihaya pale kwenye mkutano?

Kwano bukoba wachaga, wasukuma, waha wa kigoma na wengine hawajajenga na kupafanya nyumbani kwao? Dogo kazingua kishenzi.
 
Wajanja hao, wameshajua watanzania ni mazuzu, tunadanganyika kwa vitu vya kipuUzi puuzi.
 
umhurumie nini mwanaume analialia mbele za wanawake, wakati anaweka kibindoni milioni 12 kila mwisho wa mwezi?huyo amekosa ujasiri ni kumweka pembeni. Hata hanawake huwa hawalii vile mbele za watu. anajifanya ana uchungu sana na bukoba?

Kwanza pale bukoba sio nchi ya wahaya, ni ya Watanzania na pale kuna kabila zote, ilikuwaje aanze kuongea kihaya pale kwenye mkutano?

Kwano bukoba wachaga, wasukuma, waha wa kigoma na wengine hawajajenga na kupafanya nyumbani kwao? Dogo kazingua kishenzi.
Do you mean kakosea kuzungumza kihaya?
 
Tabia ya wanasiasa kurudi majimboni kuanza kuleta vituko kuelekea uchaguzi mkuu ni utoto na jambo lilishapitwa na wakati..Jamii za leo sio za zamani .Mwaka 2025 utakuwa mgumu sana kwa wabunge na sidhani kama ugumu huo ulishashuhudiwa Miaka ya nyuma..Miaka yote unakula starehe zako Dodoma tu Dar unasahau umetumwa utatue shida za watu..
 
Do you mean kakosea kuzungumza kihaya?
amekosea kuzungumza kihaya kwasababu Bukoba hawaishi wahaya tu, na wapiga kura wake sio wahaya tu, kuna wapiga kura wasukuma, wajita, wachaga na makabila mengine mengi wanaishi na wamefanya bukoba kama nyumbani kwao, wamejenga pale, wana biashara pale na hawajui kihaya. kuzungumza kihaya kwenye mkutano wa makabila yote yanayoishi bukoba ni ubaguzi wa kikabila na hayo makabila mengine hayapaswi kuja kumpa kura tena kwasababu amewabagua. mimi nimeishi bukoba miaka michache na sijui kihaya kabisa, ningekuwa nimeenda pale kwa moyo wote kwamba nikamsikilize akaongea kile kihaya ningejisikia vibaya sana, kumbe watu wa muhimu pale ni wa kabila lake tu?
 
Ehh kwani wao wanakuhurumia

Uchaguzi ukikaribia sinema zinakuwa

Nyingi sana

Ova
 
Uchaguzi umekaribia Show la Wanasiasa linaanza, mchana watajifanya kujipendekeza kwa Wananchi usiku wa manane watakuwa kwa Waganga kuoga Dawa na kuchanjwa Chale za Ngekewa.
 
Back
Top Bottom