Wanasheria, hukumu ya DOWANS na doctrine ya RES JUDICATA

Maombi ya kusajiri Tuzo yapo mahakamani tayari na muamuzi ameshapangiwa. Kwa wale wepesi nadhani mtakuwa mmeshapata nakala ya Tuzo. Kwa hisani yenu kama kuna yoyote anayo naomba muiwasilishe hapa ili tuwee kuitwalii na kutoa maoni yetu kwa ukamilifu. Nasikia Mh Raisi leo amewaomba wanasheria wapigane kadili iwezekanavyo ili Dowans wasilipwe.

Kwa mjadala unavyokwenda naona tuna wataalamu wa kutosha wa international commercial arbitration. Kama tutajadili bila ushabiki na kwa uaminifu wa kitaaluma nadhani tutakuja na jibu sahihi la kukabiliana na tatizo hillo, kama jibu lipo
 
Nilikuwa namaanisha kwamba Award isipokuwa registered DOWANS hawatakuwa na haki ya kulipwa? Na kama watakuwa na haki ya kulipwa bila registration, sasa maana ya registration ni nini?

Nafikiri maana ya registration kwa local court nukuipatia hukumu nguvu za dola! i.e. kwamba weweze kuenforce payment, hata wakienda polisi au majembe kwenda kutaifisha mali ya tanesco sheria za nchi zitakuwa zinawaruhusu kwani court ya tanzania itakua imetambua award; other bila registration watashindwa kutumia vyombo vya dola!
 
Back
Top Bottom