Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
unaonaje ukaukataa uraia wa tanzania kwanza ili tukubaliane nawe kuwa mtanzania analazimika kukubali chochote eti yuko kwenye kiapo cha aina fulani katika kuitumikia tanzania? Umekuwa ukipinga maagizo sahihi yaliyopitishwa na vyombo halali wakati unafungwa na wajibu wako katika kukubali kila kitu kilichopitishwa "kisheria" ukiwa kama raia wa tanzania, jee uhuru huo wa kufanya hivyo haupo kwa mwengine?
Hivyo unataka wengine wasiwe na uhuru wa kutowa maoni yao eti wamefungwa na viapo? Naona mwenzetu unataka kutuburuza. Na hili kwa huu muungano tu au kwa mambo yote? Pengine wazo lako la kujenga lile daraja linakusumbua>
Ni kweli mkuu, ni lazima muungano ujadiliwe kwa uwazi maana kwa sasa unafanya baadhi ya watanzania wajisikie guilty. The solutuion iso kufunika funika ni kujadili kwa uwazi. Kuna baadhi ya mambo yanatuhusu moja kwa moja, na yanahitaji tuyajadili sisi wenyewe. Inawezekana kabisa kuwa yaliyomo kwenye articles of union yalikuwa ni mawazo ya Nyerere na Karume, na sio mawazo ya wazanzibari na watanganyika.
kipindi cha muungano kuwa fumbo la imani kimepita, ujinga wa kupostpone matatizo unatifanya tukumbane na makubwa zaidi katika siku za baadaye, mfano mzuri umeme. Tuliichekea IPTL sasa imekuja Richmond na Dowans. Muungano itakuja kuwa hivyo.