Wanaosababisha mgongano CCM kung'olewa

..mbona Mwinyi na Kinana waliuza Loliondo kini hawakufukuzwa?

No wonder propaganda ya kuwa wanaomkosoa Kikwete wanafanya hivyo kwa kuwa ni Muislamu inafanikiwa. Mbaya zaidi ni kuwa watanzania wengi wanaelekea kuingia katika mtego huo wa udini ambao mwisho wake ni kupelekea katika uchaguzi ujao watanzania walio wengi kupiga kura kuegemea DINI ZAO na hivyo KURASIMISHA TANZANIA INAYOAMINI KATIKA UDINI.

Hivi hadi leo hatujaweza kung'amua kuwa hakuna ardhi, pori wala mbuga ya wanyama iliyowahi kuuzwa? Hivi inakuaje kukodishwa kwa mbuga mmoja wakati wa mwivnyi ndio kuonekane hadi leo na huku tunajua wazi wakati wa enzi ya BENJAMINI maelefu ya ekari za mapori na mbuga zetu yamekodishwa kwa wageni wakiwemo haohao waarabu waliolaaniwa enzi hizo. Inakuwaje kuwa anapohusika MUARABU ambao kwa mantiki za kitanzania ni MUISLAMU iwe kashfa ya kudumu lakini anapokodishwa/kuuziwa MZUNGU ambae kwa mantinki ya kitanzania ni Mkristo iwe ni issue ya kupita?

Ndugu zangu tuwe makini na hiz sumu za chuki za kijamii ambao tunaendelea kuzipanda kwa kujua ama kutokujua....

Hali ya nchi ni mbaya kuliko tunavyotaka kujidanganya, na tukikosa umakini katika kushughulikia masuala yenye religious ama ethnic sensitivities, tutaifikisha nchi hii pale ambapo MAFISADI WAKUU wanasubiri tuifikishe, ili waweze kuhatamisha MFUMO FISADI wao kwa nguvu za giza walizojiandaa nazo

omarilyas
 
Watanzania nani katuloga?? CCM imeoza siku nyingi, na bado tunaikumbatia tu. Eti tunajadili Lowassa na kundi lake watimuliwe! halafu ndio iweje? Wakishatimuliwa Lowassa na wenzake, CCM ndio itakuwa safi? Nani aliye iacha CCM ichafuke kama sio CCM yenyewe?

CCM imeshindwa kuongoza, imeshachoka na haina dira wala mwelekeo unaoeleweka. Sera zake ni tamu lakini ni za uongo. Tunasubiri watoke mafisadi hawa wachache ili tujipe moyo kuwa ni chama cha wananchi, eti? Haya, Juzi juzi Ndullu katumia Shilingi Bilioni moja na theluthi kutengeneza kiota, huyu naye sio fisadi, au ni maamuzi yake ndio ya kifisadi? mbona hayuko kwenye List? Au wakitoka wale huyu atasafishika 'naturally?' na atakuwa na maamuzi ya kizalendo?

Na Mkapa naye si ni mjumbe wa kudumu kwenye NEC na CC, yeye tunataka abaki?. List ni kubwa sana, na hiyo haihalalishi CCM kuendelea kutawala Tanzania.

Suluhisho ni kuikataa CCM yote. Mwenye masikio na asikie.
 
Kamati ya Mzee Mwinyi ina wajumbe watatu Mzee Mwinyi,Pius Msekwa na Abdul Rahman Kinana,ina maana hii habari kama ni ya kweli then imevujishwa na mmoja wapo wa hao watatu?Au hii kamati ina wajumbe zaidi ya hao waliyowezesha kuvujisha habari hizi na kumfikia Kubenea???Sipati picha!
Sir Leem,
Picha iko wazi yeyote kati ya hao wajumbe au wakutubi wao wanaweza kuvujisha habari hiyo ni moja ya mbinu mashuhuri inaytumiwa na Wanasiasa Duniani kote na madhumuni yake huwa ni kupima maji kwa kusikiliza maoni na kuangalia riekshen za wadau.
 
siku hizi siamini chochote cha kubenea... naona kama ana hallucinate tu kwenye public, sijui ile acid ilimuathiri ubongo!!!??
 
Sir Leem,
Picha iko wazi yeyote kati ya hao wajumbe au wakutubi wao wanaweza kuvujisha habari hiyo ni moja ya mbinu mashuhuri inaytumiwa na Wanasiasa Duniani kote na madhumuni yake huwa ni kupima maji kwa kusikiliza maoni na kuangalia riekshen za wadau.

Tatizo kubwa linalowasumbua ndugu zetu wa CCM ni mapesa waliyoruhusu kuchotwa pale BOT na hao jamaa zao, pamoja na mipesa iliyotokana na mikataba tata, hao jamaa wakazitumia kwa malengo ya chama na zilizobaki wakatumia kujenga ngome yao ndani ya NEC & CC ya CCM, sasa imekuwa sawa na CCM wamefungulia jini toka kwenye chupa na sasa kulirudisha ndani ya chupa imekuwa taabu kwelikweli, hilo wanalo na wakikosea kidogo tu jini litawanyonya damu yao na kuwafikisha wasikokutaka wakati sie tukikenua
 
si acid mkuu, pesa haishindwi kitu -

na ile acid ilikuwaje akamwagiwa? Jamaa mmoja kanibip kuwa alikuwa anamzamia mke wa mtu na wala haihusiani na issue za kisiasa.

Huyu jamaa hata gazeti lake siku hizi sisomi kabisa. Naliona kama la king'unge vile.
 
No wonder propaganda ya kuwa wanaomkosoa Kikwete wanafanya hivyo kwa kuwa ni Muislamu inafanikiwa. Mbaya zaidi ni kuwa watanzania wengi wanaelekea kuingia katika mtego huo wa udini ambao mwisho wake ni kupelekea katika uchaguzi ujao watanzania walio wengi kupiga kura kuegemea DINI ZAO na hivyo KURASIMISHA TANZANIA INAYOAMINI KATIKA UDINI.

Hivi hadi leo hatujaweza kung'amua kuwa hakuna ardhi, pori wala mbuga ya wanyama iliyowahi kuuzwa? Hivi inakuaje kukodishwa kwa mbuga mmoja wakati wa mwivnyi ndio kuonekane hadi leo na huku tunajua wazi wakati wa enzi ya BENJAMINI maelefu ya ekari za mapori na mbuga zetu yamekodishwa kwa wageni wakiwemo haohao waarabu waliolaaniwa enzi hizo. Inakuwaje kuwa anapohusika MUARABU ambao kwa mantiki za kitanzania ni MUISLAMU iwe kashfa ya kudumu lakini anapokodishwa/kuuziwa MZUNGU ambae kwa mantinki ya kitanzania ni Mkristo iwe ni issue ya kupita?

Ndugu zangu tuwe makini na hiz sumu za chuki za kijamii ambao tunaendelea kuzipanda kwa kujua ama kutokujua....

Hali ya nchi ni mbaya kuliko tunavyotaka kujidanganya, na tukikosa umakini katika kushughulikia masuala yenye religious ama ethnic sensitivities, tutaifikisha nchi hii pale ambapo MAFISADI WAKUU wanasubiri tuifikishe, ili waweze kuhatamisha MFUMO FISADI wao kwa nguvu za giza walizojiandaa nazo

omarilyas

ingekuwa vyemaa kama na wewe ungeongeza majina ya wale ambao unaamini hawakuchukuliwa hatua hivyo kufanya hoja ya kuwachukulia hatua wakina lowasa, rostam, chenge na karamagi kuwa mfu.

badala yake umeamua kuingiza mtizamo wa udini!

kwani lowasa, rostam, chenge na karamagi ni dini gani? kwani nawe ungeongeza kwamba na mkapa pia hakuchukuliwa hatua bila kuingiza hoja ya udini ingekuwa mbaya?
 
Unaambiwa CCM wanajiamini weacha tu. Wasema hata kama CCM wataweka msukule au nyani kugombea nafasi yoyote wao wataula tu! Sijui wanapata wapi kibri hiki. Nadhani hawajui histotia ya Malawi, Zambia, Mexico, na wapi kule vyama vikongwe vilipigwa chini kama utani vile!

Leka
 
ingekuwa vyemaa kama na wewe ungeongeza majina ya wale ambao unaamini hawakuchukuliwa hatua hivyo kufanya hoja ya kuwachukulia hatua wakina lowasa, rostam, chenge na karamagi kuwa mfu.

badala yake umeamua kuingiza mtizamo wa udini!

kwani lowasa, rostam, chenge na karamagi ni dini gani? kwani nawe ungeongeza kwamba na mkapa pia hakuchukuliwa hatua bila kuingiza hoja ya udini ingekuwa mbaya?

Nilichofanya mimi nikutoa angalizo kuwa kama hatujawa makini tukaepuka kutumia kauli mbiu ambazo zimezungukwa na kiwingu cha udini kama hili suala la LOLIONDO - MWINYI - KINANA tutaendelea kucheza mikononi mwa MAFISADI....

Na huo ni mtizamo wa jumla ambao wakati mwengine huwa na ukweli kiasi hata kama ni kiduchu. Sasa kama hatutakuwa makini na kuepuka kucheza katika mitego hiyo ni wazi mwisho wa siku tutakuwa ni "sisi" tulioharibikiwa na "wao" wanapeta...

Tatizo tumeshajingea utamaduni wa kuogopa kulizungumzia suala hili kwa uwazi na kukimbilia kuwabambikia wale wanaothubutu kulizungumzia lebo ya UDINI...

Tukubali tusikubali wapo wengi wanaoamini kuwa Rais Kikwete na utawala wake "unapigwa vita" kwa kuwa rais ni Muislam. Ni wazi kuna mkono wa propaganda chafu katika hili, lakini pia historia ya yaliyotokea wakati wa Mwinyi ambayo baadaye mengi yalikuja kujipambanua na kuonyesha uwepo wa mikakati ya fitina na uwongo, pamoja na matamshi na matendo ya baadhi ya watu wasiojali kuonyesha umakini katika hili katika nyakati hizi, kwa kiasi kikubwa imewezesha kufanikisha propaganda chafu hizo.....

Kwa hiyo kwangu mimi ni angalizo tu kuwa tuwe makini katika michango yetu huku tukitambua hali ya kisiasa na kijamii ilivyo hivi sasa.....

Ndugu omarilyas

Ufisadi hauna dini fisadi ni fisadi tu hata kama angekuwa baba yangu hata awe askofu au imamu fisadi kwangu ni fisadi tu usijaribu kuingiza udini wakati tunazungumzia mustakabali wa nchi hatumtetei kiongozi yeyote kwa dini yake haijalishi Mwinyi ni mwislam au mkristo

Mbona wakristo wanamponda Nyerere na Mkapa kwa aliyoyafanya na yeye ni mwislam acha hizo naona wewe ndiye unataka kuchochea udini hapa hata hayo majina yaliyotajwa kwani wote ni waislam Lowassa ni mwislamu usilete propaganda chafu za udini.
 
Jamani mimi nimebeba maboksi sasa nahisi nazeeka na nguvu zinaniishia
Ntawezaje kuingia kwenye payroll ya mafisadi nikirudi bongo?
Just ushauri
 
Jamani mimi nimebeba maboksi sasa nahisi nazeeka na nguvu zinaniishia
Ntawezaje kuingia kwenye payroll ya mafisadi nikirudi bongo?
Just ushauri

Wakati ule ukiwa na nguvu ulikimbia kwenda kujenga uchumi ulaya badala ya kujenga wa nchi yako sasa umezeeka unataka kutuletea mzigo kaa huko huko wakulee wajomba zako maana wamekuchuma kodi zako nyingi huku nyumbani kodi yako inaonyesha zero.
 
Eee lakini tangu uhuru jamani ukotuuuu si utoke ?? Mpaka ufukuzwe?? Real sorryyyyyy!!!
 
..mbona Mwinyi na Kinana waliuza Loliondo kini hawakufukuzwa?

..mimi naona CCM wavunje chama tu. wote wameoza.

Mimi nadhani hili la CCM kuwa chama cha mafisadi lilidhihilishwa na LOwassa mbele ya bunge pale aliposema kuwa " Kama tutachunguzana wote humu hakuna atakayepona" maana yake ni kwamba alikuwa anakili kuhusika na tuhuma za Richmond lakini alikuwa anashangaa kwa wenzie kumtoa kafara wakati nao wana madudu yao mengi anayoyajua!!!
 
Jamani,

hii taarifa ya "facts 1" haionekani kama ina ukweli wowote! Hicho kichwa cha habari ni "statement of fact" ambayo ndani ya maelezo haina uthibitisho kwamba habari imepatikana wapi na vipi!

Inaonekana ni hisia na uzushi tu! Labda atakayeiamini ni yule anayefikiri kwa kutumia masikio yake (ya kusikiliza uzushi na fitina!) na mikono yake (ya kupokea chochote cha kuhongwa!), badala ya kufikiri kwa ubongo ulio kichwani! Hata Mwandishi wenyewe anatia shaka kuwa labda ametumiwa tu! Hana "credibility" yoyote!

Labda kuna hisia kuwa "wapiganaji wa ufisadi" (sijui fisadi ni nani na nani anamwambia mwenzake fisadi!) watabamizwa katika taarifa ya Kamati ya Mzee Mwinyi na hivyo wanatapatapa kwa kutupa habari za uzushi za maamuzi ya Kamati ya Mwinyi kabla hayajatolewa, na kutaka kutudanganya kuhusu kuanzishwa kwa "Chama Cha Jamii" (CCJ) kutaka kuyumbisha msimamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC)! Ni porojo tu hizi za magazeti kama "Sema Usikike", "Kulikoni" na "MwanaHalisi"! Tusubiri ripoti ya Mzee Mwinyi na maamuzi ya NEC. Tusidanganyike!

Bwassa
Hapo hamna uongo wala fitina yeyote,labda ndugu yangu unayebisha wewe ndiyo walewale mafisadi wadogo mnaotaka CCM iendelee ili muwe mafisadi wakubwa.
Ni nini kisichojulikana kuhusu Rostam,Chenge,Karamagi na Lowasa?Hao wote ni mafisadi papa katika nchi hii-na endapo CCM kama inataka kuleta image nzuri mbele ya umma wa waTZ basi hawana budi kufumba macho na kuwang'oa hao na wengine kibao.Akina Kingunge familia zao zimeifisidi stendi ya Ubungo weeee mpaka basi alafu wanajiita wazee wa Chama!
 
It could sound great if the names who want to shift to another political party could be disclosed, how many are they, what they have done to the Tanzanians up to this point and time? And not keep on shouting as they doing now, Let them make a move, who are they by the way. It doesn’t make sense at all for a group of people for their own interest want to make the Tanzanians to believe that without them, nothing will be done, absolutely that ridiculous ideas. We Tanzanians we have to be very careful with sewage politics (Siasa za maji taka).Jamani si waondoke tu, kwa nini kila siku wanasema wataondoka lakini wamekaa tu ? Kama Nyerere alikufa na chama bado kipo,sasa hao wanataka kumtisha nani kama siyo uroho wa madaraka ? Hizi kelele zote ni mbio za urais 2015.
 
Mkuu na hicho kiingereza chako cha ki Idd Amin,kwani shida iko wapi mazee katika kutumia kiswahili lugha yetu ya taifa?
 
Kikwete hana ubavu wa kumfukuza yoyote ndani ya CCM. Kama angekuwa na ubavu huo angeshawafukuza wengi katika chama hicho hasa wale wenye tuhuma nzito dhidi yao za kifisadi. Sasa hivi yuko yuko tu hana authoritative power yoyote ile na hii inasababisha kuwa na misukosuko mingi ndani ya chama hicho ambayo hatujawahi kuiona tangu enzi za TANU na Afro Shirazi Party.

Najua Nyerere alikua hakubaliki na jumua fulani, vile vile ilikua hivyo kwa Mwinyi na Mkapa.
Sidhani kama Kikwete anaweza ongea kwenye jumuia za kaskazini, kusini nk na akaungwa mkono na watu wakafanya kweli asemacho.

Badala ya Mzanzibar ama Mmasai nk, ingefaa raisi ajae awe Mchaga au Msukuma, kwa kua ni wengi na basi support yao kwa raisi itaongeza kujiamini kwa raisi na ufanisi utaongezeka. TZ naamini tumeganyika lakini hatutaki kukubali hicho kitu.

Daima maendeleo yanaanzia kwenye point moja yenye mwamko, umoja na nguvu na baadaye kusambaa, TZ haiwezi jengeka yote kwa mpigo.

Kikwete yupo tu hana base na ndio maana hana nguvu ya kuamua mambo mazito. Chini ya Nyerere CCM ilikua moja na ilishikwa hatamu na Nyerere pekee, lakini CCM ya leo ni mchanyato ambao hata hauwezi kumpa nguvu Kikwete.
 
Back
Top Bottom