Wanaosababisha mgongano CCM kung'olewa

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Na Saed Kubenea

KUNDI la vigogo waandamizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) limepanga kujiondoa ndani ya chama hicho iwapo masharti yake hayatakubaliwa, MwanaHALISI limeelezwa.

“Kama hatukusikilizwa, tutatoka. Tutaunda chama chetu au tutajiunga na moja ya vyama vilivyopo,” ameeleza mmoja wa viongozi wanaoshinikiza mabadiliko.

Mpasuko huo mpya na wa aina yake unalenga kushinikiza kuondolewa nafasi za uongozi, vigogo ambao wamewahi kutuhumiwa ufisadi ndani ya chama.

Kamati Kuu (CC) ya CCM inakutana mjini Dar es Salaam Jumamosi hii na Halmashauri Kuu (NEC) itakutana Jumatatu ijayo ambako hoja hizi zinatarajiwa kuwekwa wazi na “huenda kutolewa maamuzi.”

Mkakati wa kuhama CCM umepewa nguvu na taarifa za Kamati ya Ali Hassan Mwinyi zilizovuja hivi karibuni. Taarifa zinasema kamati imependekeza viongozi wanne waandamizi wavuliwe uongozi ili kurejeshea chama hadhi yake mbele ya umma.

Wanaotajwa kuondolewa uongozi ni mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz; mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi.

Taarifa zinasema ripoti ya mwisho ya Kamati ya Mwinyi, iliyopelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete, inawatuhumu Rostam, Lowassa na Karamagi kwa kujenga makundi ya kujisafisha ambayo yameonekana kudhoofisha chama na serikali.

Kwa upande wake, Chenge anatuhumiwa kwa “kuaibisha” chama kutokana na tuhuma nzito za ufisadi ambazo zinamkabili.

Wakati Lowasa, Rostam na Karamagi wanatumuhiwa ufisadi katika mkataba wa Richmond, Chenge anakabiliwa na tuhuma za ununuzi wa rada ya kijeshi.
“Hawa jamaa wamejenga mtandao wa kujisafisha. Ni mtandao huu ambao ni kiini cha matatizo yaliyopo ndani ya chama na serikali hivi sasa,” chanzo cha habari cha gazeti kimeeleza.

Kamati ya Mwinyi inasema kuondolewa nyadhifa za uongozi kwa vigogo hao wanne, kunaweza kurejesha utulivu na hadhi katika chama wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu, ameeleza mtoa taarifa.

MwanaHALISI limeelezwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Mwinyi walikuwa makini kuhusu taarifa zinazotaja CCM kuhusishwa na fedha zilizoibwa Benki Kuu (BoT) kupitia kampuni ya Kagoda.

Katika mazingira ambapo chama kimeshindwa kujieleza kinagaubaga na kueleweka kuwa hakikutumia fedha za Kagoda – kampuni inayotajwa kumhusisha Rostam Aziz – Kamati imeona kuwa anayetuhumiwa aondolewe uongozi ili “kulinda chama.”

Taarifa zinasema wanaoshinikiza mapendekezo ya kamati yaheshimiwe vinginevyo watahama CCM, ni pamoja na wabunge ambao wamekuwa wakijitambulisha kwa kupinga ufisadi.

Hata hivyo, taarifa zimeeleza kuwa mpango wa kuanzisha chama kipya au kujiunga na kilichopo, utaweza kufanywa iwapo tu vikao vya juu vya CCM vilivyopangwa kuanza mwishoni mwa wiki hii, vitashindwa kuchukua hatua zilizopendekezwa dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na CCM hivi karibuni, vikao vya Kamati ya Maadili, CC na NEC vitafanyika kati ya 23 na 26 Januari 2010.

Mjumbe wa mkakati wa “mafisadi wabaki” au “wapinga ufisadi watoke,” amesema tayari mkakati wa ama kuanzisha chama kipya au kujiunga na chama kimojawapo cha upinzani hapa nchini umeiva.

“Tunasubiri vikao ili kuamua nini cha kufanya. Kama CCM itaendelea kulea mafisadi, tutarudi kutoka Dodoma (bungeni) na chama kipya. Na iwapo tutashindwa kukisajili kutokana na muda kuwa mfupi, tutajiunga na moja ya vyama vya upinzani vilivyopo,” amesema mjumbe huyo wa NEC.

Septemba mwaka jana NEC iliunda Kamati ya watu watatu iliyoongozwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuchunguza kile kilichoitwa “mpasuko” ndani ya Bunge na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa na Spika wa zamani wa Baraza la Kutunga Sheria la Afrika Mashariki, Abdulrahman Kinana.

Tayari Kamati ya Mwinyi imepeleka mapendekezo yake kwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Gazeti hili linaweza kuthibitisha kwamba kamati ya Mwinyi imependekeza kuvuliwa nyadhifa kwa walau vigogo wanne wa chama hicho ili kurejesha umoja na mshikamano ndani ya chama, jambo ambalo kama litafanikiwa, basi mpango mzima wa kuanzisha au kuhama chama unaweza kuyeyuka.

Mtandao wa kuondoa mafisadi katika chama umeanza kujipanga kwa kutafuta wajumbe wa NEC wa kuwaunga mkono kutoka katika mikoa mbalimbali. Miongoni mwa wanaotafutwa kufikiwa ni makatibu wa CCM wa mikoa.

Hata hivyo, mpango wa kuvua nyadhifa za uongozi watuhumiwa wa ufisadi, unatarajiwa kupata upinzani mkali ndani ya NEC kutokana na kundi la watuhumiwa kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya kikao hicho na hivyo kuwapo uwezekano mkubwa wa mmeguko.

“Hofu yangu kubwa ni kwamba mara baada ya CC kujadili mapendekezo hayo, vigogo hao watapata taarifa na wataanza mipango ya kukabiliana na hoja hizo. Kwa hiyo vita hapa itakuwa kwenye NEC,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema mpango wowote kati ya hiyo miwili – ule wa kufukuza mafisadi au ule wa kushughulikia watuhumiwa wa ufisadi, unaweza kukipasua chama. Hii itategemea jinsi mwenyekiti Rais Kikwete atakavyocheza karata zake, amesema mjumbe wa NEC na kuongeza, “aamue kife au kipone.”

Source:
Gazeti la MwanaHALISI
 
Jamani,

hii taarifa ya "facts 1" haionekani kama ina ukweli wowote! Hicho kichwa cha habari ni "statement of fact" ambayo ndani ya maelezo haina uthibitisho kwamba habari imepatikana wapi na vipi!

Inaonekana ni hisia na uzushi tu! Labda atakayeiamini ni yule anayefikiri kwa kutumia masikio yake (ya kusikiliza uzushi na fitina!) na mikono yake (ya kupokea chochote cha kuhongwa!), badala ya kufikiri kwa ubongo ulio kichwani! Hata Mwandishi wenyewe anatia shaka kuwa labda ametumiwa tu! Hana "credibility" yoyote!

Labda kuna hisia kuwa "wapiganaji wa ufisadi" (sijui fisadi ni nani na nani anamwambia mwenzake fisadi!) watabamizwa katika taarifa ya Kamati ya Mzee Mwinyi na hivyo wanatapatapa kwa kutupa habari za uzushi za maamuzi ya Kamati ya Mwinyi kabla hayajatolewa, na kutaka kutudanganya kuhusu kuanzishwa kwa "Chama Cha Jamii" (CCJ) kutaka kuyumbisha msimamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC)! Ni porojo tu hizi za magazeti kama "Sema Usikike", "Kulikoni" na "MwanaHalisi"! Tusubiri ripoti ya Mzee Mwinyi na maamuzi ya NEC. Tusidanganyike!

Bwassa
 
If these people won't go then ufisadi Tanzania hautakwisha.....what can we do to get rid of these openly fisadis?
 
If these people won't go then ufisadi Tanzania hautakwisha.....what can we do to get rid of these openly fisadis?

Hakuna sehemu duniani ambako mafisadi hakuna. Inategemeana ni mafisadi gani. Usiote ndoto chovu kwmaba kuna siku mafisadi wataisha Tanzania. No way!
 
Hakuna sehemu duniani ambako mafisadi hakuna. Inategemeana ni mafisadi gani. Usiote ndoto chovu kwmaba kuna siku mafisadi wataisha Tanzania. No way!
it depends on the of its pipo, everything is possible under the sun, by the will of the ALMIGHTY GOD, if we culd decide, yes we can
 
Jamani, uungwana mgumu. Mtu unatuhumiwa hivi, kweli hata haya huoni - hata kama umeonewa? mpaka ufukuzwe? Muungwana ni kitendo bwana. Sio mpaka rais akune kichwa kukutafutia sababu na kuundia kamati kibao. Kamati ya kwanza inatosha.
 
..mbona Mwinyi na Kinana waliuza Loliondo kini hawakufukuzwa?

..mimi naona CCM wavunje chama tu. wote wameoza.
 
Nafikiri hili ni tatizo la kitaifa. Lilianza toka awamu ya kwanza, ikaendelea awamu ya pili na tatu. Ni njia ya kuwatuliza wananchi hata kama kamati haitakuja na ripoti. Tatizo watu sasa wamejanjaruka na wanfatilia issue kuliko zamani. Hivyo inabidi may be waje na strategy nyingine au wakae kimya kuliko kudanganya wananchi na kamati.
 
Jamani,

hii taarifa ya "facts 1" haionekani kama ina ukweli wowote! Hicho kichwa cha habari ni "statement of fact" ambayo ndani ya maelezo haina uthibitisho kwamba habari imepatikana wapi na vipi!

Inaonekana ni hisia na uzushi tu! Labda atakayeiamini ni yule anayefikiri kwa kutumia masikio yake (ya kusikiliza uzushi na fitina!) na mikono yake (ya kupokea chochote cha kuhongwa!), badala ya kufikiri kwa ubongo ulio kichwani! Hata Mwandishi wenyewe anatia shaka kuwa labda ametumiwa tu! Hana "credibility" yoyote!

Labda kuna hisia kuwa "wapiganaji wa ufisadi" (sijui fisadi ni nani na nani anamwambia mwenzake fisadi!) watabamizwa katika taarifa ya Kamati ya Mzee Mwinyi na hivyo wanatapatapa kwa kutupa habari za uzushi za maamuzi ya Kamati ya Mwinyi kabla hayajatolewa, na kutaka kutudanganya kuhusu kuanzishwa kwa "Chama Cha Jamii" (CCJ) kutaka kuyumbisha msimamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC)! Ni porojo tu hizi za magazeti kama "Sema Usikike", "Kulikoni" na "MwanaHalisi"! Tusubiri ripoti ya Mzee Mwinyi na maamuzi ya NEC. Tusidanganyike!

Bwassa

Tuwekee ukweli tuchungulie na sisi huko ndani.

Hakuna sehemu duniani ambako mafisadi hakuna. Inategemeana ni mafisadi gani. Usiote ndoto chovu kwmaba kuna siku mafisadi wataisha Tanzania. No way!

Wapi huko duniani ambako mafisadi hawachukuliwi hatua? Tunafahamu China wananyongwa, USA wanakwenda jela nk .

Nafikiri hili ni tatizo la kitaifa. Lilianza toka awamu ya kwanza, ikaendelea awamu ya pili na tatu. Ni njia ya kuwatuliza wananchi hata kama kamati haitakuja na ripoti. Tatizo watu sasa wamejanjaruka na wanfatilia issue kuliko zamani. Hivyo inabidi may be waje na strategy nyingine au wakae kimya kuliko kudanganya wananchi na kamati.

Blame culture, where does it stop?
 
To be honesty CCM need changes and revolution soon as possible jamani kwani hii ni dhahili kuwa kuna tataizo, na wengi wao wanatumia huu muda kufanya political games zao hapo kuwachanganya wananchi, lazima hapa watu mjiulize CCM kama ndio chama kikubwa TZ na viongozi wake ndio haooo kila kukicha kashifa mwataka kutuambia wanasingiziwa tuuu kila siku jamani au? pia mwonapo hii hali ni kuwa viongozi wengi ndani ya CCM wamepungukiwa na fikra za siasa na kusambaza chuki na fitna hii ni wazi kuwa siasa inawashinda hao viongozi waliopo.

wakati sasa umefika wajaribu kujistili sasa wasije aibika na uzeee huu wote wanataka nini ambacho hawajakipata katika maisha yao ya uongoziiiii jamani? kuna nini kwenye uongozi wa kitanzania?? ni kweli kutaka kuwaongoza watanzania au kuna lao jamboooo??

Mfano mdogo tuuu tokea twasoma those 1980's mpaka sasa wana CCM wengi bado wapo na nyazifa zoa hakuna mabadiriko yoyote mwinyi kila siku yuko kwenye NEC & CC Marehumu Simba wa vita nae alikuwa anaudhuria jamani Kingunge ati nae? what wrong with this old politician? Chama ni chao nasi tuanzishe chetu au? maana nasi tumejiunga na CCM na tumewakuta na kustaaafu hawataki je wanataka nini? juzi wameambiwa ni zamu ya vijana wazee basi wamekuja juu hoo kwani mie ni mzee jamani ni alama za nyakati ndizo zawambia mpisheni sio uzee tu.

Just tizama nchi za ulaya ni kiongozi gani yupo kwenye madaraka eg tokea enzi za kina R.Nixon,Jimmy C,JF Kennedy, G Bush, kwa clintoni naweza sema ni viongozi wa chini au wako kwa Military ambako ni muhumu sana kwani ndiko kwa play part kubwa ya ulinzi wa nchi sasa hapa kwetu toka enzi za uhuru mpaka leo watu ni wale wale no changes jamani?

sasa kwnini wasikutwe na hizo kashifaaaaa bwana uongozi kwa wabunge mawaziri etc iwe just 10 to 12 yrs period.
 
Jamani,

hii taarifa ya "facts 1" haionekani kama ina ukweli wowote! Hicho kichwa cha habari ni "statement of fact" ambayo ndani ya maelezo haina uthibitisho kwamba habari imepatikana wapi na vipi!

Inaonekana ni hisia na uzushi tu! Labda atakayeiamini ni yule anayefikiri kwa kutumia masikio yake (ya kusikiliza uzushi na fitina!) na mikono yake (ya kupokea chochote cha kuhongwa!), badala ya kufikiri kwa ubongo ulio kichwani! Hata Mwandishi wenyewe anatia shaka kuwa labda ametumiwa tu! Hana "credibility" yoyote!

Labda kuna hisia kuwa "wapiganaji wa ufisadi" (sijui fisadi ni nani na nani anamwambia mwenzake fisadi!) watabamizwa katika taarifa ya Kamati ya Mzee Mwinyi na hivyo wanatapatapa kwa kutupa habari za uzushi za maamuzi ya Kamati ya Mwinyi kabla hayajatolewa, na kutaka kutudanganya kuhusu kuanzishwa kwa "Chama Cha Jamii" (CCJ) kutaka kuyumbisha msimamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC)! Ni porojo tu hizi za magazeti kama "Sema Usikike", "Kulikoni" na "MwanaHalisi"! Tusubiri ripoti ya Mzee Mwinyi na maamuzi ya NEC. Tusidanganyike!

Bwassa

Doubting Thomases walikuwapo hata ufisadi wa EPA,Richmond na mwingineo ulipowekwa hadharani kwa mara ya kwanza.Ni rahisi kuyalaumu magazeti kama Mwanahalisi yanayofanya kazi kwa vitisho vya kufungiwa kama si kumwagiwa tindikali yanapogusa interest za wakubwa.Uzuri wa habari iliyowekwa hadharani ni kwamba msomaji halazimishwi kuiafiki.

Hata tukikubaliana kuwa habari hii imeandikwa kutokana na hisia tu za mwandishi/gazeti,je kwa mawazo yako unadhani Kamati ya Mwinyi ingepaswa kuja na solution gani itakayokuwa thabit na mwafaka kwa manufaa ya muda mrefu ya CCM?Je hudhani kuwa Lowassa,Rostam,Chenge na Karamagi walistahili kutoswa zamani hizo?

Kuna "hisia" zinazopaswa kuonekana kichekesho kwa mfano gazeti likija na habari kuwa JK anataka kuhama CCM,au Ridhwani Kikwete ana mpango wa kuunda chama chake.Yani hata kuambiwa Papa Benedict ni Mkatoliki bado ni hisia?
 
Jamani,
hii taarifa ya “facts 1” haionekani kama ina ukweli wowote! Hicho kichwa cha habari ni “statement of fact” ambayo ndani ya maelezo haina uthibitisho kwamba habari imepatikana wapi na vipi! Inaonekana ni hisia na uzushi tu! Labda atakayeiamini ni yule anayefikiri kwa kutumia masikio yake (ya kusikiliza uzushi na fitina!) na mikono yake (ya kupokea chochote cha kuhongwa!), badala ya kufikiri kwa ubongo ulio kichwani! Hata Mwandishi wenyewe anatia shaka kuwa labda ametumiwa tu! Hana "credibility" yoyote! Labda kuna hisia kuwa “wapiganaji wa ufisadi” (sijui fisadi ni nani na nani anamwambia mwenzake fisadi!) watabamizwa katika taarifa ya Kamati ya Mzee Mwinyi na hivyo wanatapatapa kwa kutupa habari za uzushi za maamuzi ya Kamati ya Mwinyi kabla hayajatolewa, na kutaka kutudanganya kuhusu kuanzishwa kwa “Chama Cha Jamii” (CCJ) kutaka kuyumbisha msimamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC)! Ni porojo tu hizi za magazeti kama “Sema Usikike”, “Kulikoni” na “MwanaHalisi”! Tusubiri ripoti ya Mzee Mwinyi na maamuzi ya NEC. Tusidanganyike!

Bwassa

Mkuu you are very right thinking this way, lakini kumbuka hii ni Tanzania na ni zaidi ya uijuavyo. With this thinking in mind EPA neva existed so did Richmond, Deepgreen, Meremeta etc.

Nilichojifunza in the last 3 to 4 yrs, Kila habari in Tz just ipe 50/50 na ikiwezekana 30/70 with the later being very likely it is true. Just stay tuned.................
 
Upuuzi mtupu!Why the heck are they beating around the bushes?Kibaya kilichopelekea ufisadi ni kipi kati ya chama na watu?
Certainly jibu linaweza kuwa ni watu kwa upande mmoja,then watu hao wamekwenda kinyume na taratibu na sera za chama?If so then kwanini wasitumie vifungu husika kuwashughulikia watuhumiwa hao?
Lets say kwa upande mwingine ni lichama la ccm halifai,sasa kama wanajuwa kuwa thats the case kwanini wasijiondoe?Ama wanataka kuondoa tabaka moja la mafisadi na kupachika jingine simultaneously?
Kusema eti either tunabaki ama tunaondoka depending on the fates of so and so people,how is that the way to fix ufisadi?
Kuna anayeweza kuni convince ni kivpi huu upuuzi utaleta mabadiliko?
Natanguliza shukran.
 
Thanks mkuu JMushi and afterall why are we busy discussing matters in the CCM as if it is one and only one to take us tho the promise land????????
 
Mwaka huu kama CCM itatoka nitaamini ni chama dume maana imezungukwa na matatizo kibao kwa sasa hakuna mtu ndani ya CCM anayeweza kumkemea mwenzake kama enzi za mchonga Karume kaota mapembe hakuna mtu wa kumwambia NO si Kikwete si Msekwa si Mwinyi si Malecela wala Makamba.

CCM Zanzibar haziivi na CCM bara wameamua kufanya mambo yao hawataki kuingiliwa Balaza la wawakilishi nalo limeamua kuondoa baadhi ya vipengele vya muungano yakiwemo mafuta hatujasikia tamko lolote toka SMT.

Pia CCM ina mtihani mkubwa kuhusu hili la kamati ya Mwinyi vile vile pia inatishiwa na ujio wa CCJ kweli mwaka huu ikitoka ni chama dume lakini inategemea na umahili wa mwenyekiti wake ambaye anaonekana kuogopa kukemea maovu yanayoendelea.
 
..mbona Mwinyi na Kinana waliuza Loliondo kini hawakufukuzwa?

..mimi naona CCM wavunje chama tu. wote wameoza.

Kikwete hana ubavu wa kumfukuza yoyote ndani ya CCM. Kama angekuwa na ubavu huo angeshawafukuza wengi katika chama hicho hasa wale wenye tuhuma nzito dhidi yao za kifisadi. Sasa hivi yuko yuko tu hana authoritative power yoyote ile na hii inasababisha kuwa na misukosuko mingi ndani ya chama hicho ambayo hatujawahi kuiona tangu enzi za TANU na Afro Shirazi Party.
 
1-Hawa wanne hawana makubaliano na wananchi-wanayo na CCM
2-Wananchi peke ndio wenye nguvu ya kuondoa hawa vigogo- wametokea wapi hawa?
But and then what.....kamati itasusa kama hawa hawaondoki?

bila bila
 
Kamati ya Mzee Mwinyi ina wajumbe watatu Mzee Mwinyi,Pius Msekwa na Abdul Rahman Kinana,ina maana hii habari kama ni ya kweli then imevujishwa na mmoja wapo wa hao watatu?Au hii kamati ina wajumbe zaidi ya hao waliyowezesha kuvujisha habari hizi na kumfikia Kubenea???Sipati picha!
 
Back
Top Bottom