Wanaoifuata Nyota yako ni kina nani?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
WANAOIFUATA NYOTA YAKO NI KINA NANI?

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu Jeusi.

Ni kina Nani hao? Unawajua wanaoifuata Nyota yako?
Neno Nyota linaweza kuwa linachechemea katika fikra za watu wasioamini mambo ya Kiroho hasa ndugu zangu kina Kiranga, hata hivyo wao tutatumia istilahi "Bahati" au "Ngekewa" ili nao tuwachukue pamoja katika andiko hili.

Je, kina Nani wanaifuata Bahati yako?

Wazungu Wana salamu yao "Good Luck" wakimaanisha kila lenye Kheri au bahati njema iwe juu yako.

Na hicho ndicho kiini cha Mada yetu.

Kiroho Neno bahati linaweza kutafsiriwa kama Nyota/ nuru njema n.k.

Jambo zuri huzingirwa na kufuatwa na Nyota yaani bahati. Na Jambo Baya huzingirwa na kufuatwa na MIKOSI.

Nyota au bahati inatabia ya kung'aa, kuonekana hivyo inaweza kuonekana na watu wengi ambao haiwahusu. Hiyo huweza kuleta wivu, husda, kijicho, dhulma na wakati mwingine mauaji.

Ndio maana inashauriwa Jambo lolote zuri ukiwa unalinyemelea ili kulipata itakupasa usipige kelele au kusemasema, na hata ukilipata itakupasa ukae kimya usitangaze tangaze kwani inaweza kuwa hatari kwako.

Kwani hujui ni kina Nani wanaifuata Nyota/bahati yako.
Watu wengi tumekuwa tukifanya makosa yakujirudia rudia na kujikuta Nyota zetu zikichukuliwa na watu wengine.

Niliwahi soma kisa cha Marehemu Musa wa madini wa Kule mtwara, ambacho ni kisa cha kusikitisha Mno.

Kisa cha Musa wa madini ni mfano halisi wa mada yetu ya leo, Musa hakujua ni kina Nani waliokuwa wanafuata Nyota au bahati yake. Walikuwa watu Wabaya na hakika walimdhulumu sio tuu pesa zake Bali waliidhulumu mpaka roho yake.

Katika maandiko, kuna kisa cha Yesu;
Mathayo 2:2
Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

Mathayo 2:3

Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
Mathayo 2:4

Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

Unaweza kusoma Sura yote. Mathayo 2.
Yesu anazaliwa lakini angani inaonekana Nyota ambayo Kwa wanajimu/mamajusi inawapa mshangao ni kitu gani, lakini Jambo Hilo pia Mfalme Herode, Makuhani na Waandishi linawashighulisha kujua Nyota hiyo niya Nani, Mfalme Herode anawatuma Wanajimu/mamajusi waifuatilie hiyo Nyota alafu wailetee habari zake, mamajusi wanasafiri kuifuata Nyota mpaka Bethlehem ya Yuda wanatokea kwenye Boma ambapo ndani yake Kuna mtoto amezaliwa ndiye Kristo.

Wanasujudu na kutoa zawadi kisha wanaondoka lakini Malaika anawazuia wasirudi Kwa Mfalme Herode Kwa maana wakimpa taarifa ya kuzaliwa Kwa Kristo basi mtoto huyo ndiye Yesu atauawa. Hiyo ndio ilikuwa bahati ya Yesu.

Vipi kwako, Wasoma Nyota, wenye macho ya kuona fursa au bahati au Nyota yako je ni kina Nani?

Je kina Nani wakiona Jambo zuri jipya likija kwenye maisha yako labda ni ndoa, mume au mke Mzuri, au kazi nzuri au promotion kazini, je wanaoifukuzia Nyota yako watakubebea zawadi au ndio watakuwa Kama Askari polisi walionusa mchongo wa marehemu mdogo wetu Musa wa madini?

Namna ya kudhibiti wafukuzia Nyota yako.

I. Usipende kuongea na kutoa Siri zako za mafanikio

ii. Sio kila wanaokuja kukupa hongera na pongezi wanakuja Kwa wema, wengine wametumwa kama vile walivyotumwa Mamajusi, sasa vipi wao wasipotokewa na Malaika au wasipopata roho wa Mungu kurudisha ripoti ya mafanikio yako huko walikotumwa?

iii. Kuomba Mungu na kuwa karibu na falme za kiroho.
Maana bila hivyo ni ngumu kutambua ipi ni bahati na upi ni mkosi.

Wapo waliodhani wamepata bahati/Nyota alafu mwisho wakagundua ni mkosi wa maisha. Wanakujutia.

Taikon nimemaliza, sabato imeingia sitajibu maswali.

SABATO NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom