Wanandoa, hivi mliwezaje kukubaliana kutokushikiana simu kuepusha magomvi yasio ya lazima?

Macbook pro

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
665
902
Habari ganj wanafamilia wa MMU, Ni muda sana umepita tangu nilete maada yangu kuomba ushauri. Poleni kwa changmoto za maisha NA misiba iliyoikumba nchi yetu pendwa.

Niende kwenye maada, mie na MWENZA wangu ambaye sasa hivi tuna takiribani miaka miwili pamoja na mwaka mmoja wa Ndoa. Kama mnavyofahamu nyakati zimebadilika sana, Mambo katika jamii zetu yamebadilika sana.eo kunayo mitandao ya kijamii ambayo imeifanya dunia kuwa kama mtaa kama sio Kijiji kabisa. Kila siku watu tunapata marafiki wapya katika maeneo mbali mitandao ya kijamii ikiwemo bila kusahau maeneo tunayotumia muda mrefu katika masaa yetu kujitafutia ridhiki.

Mie ninao marafiki wa jinsia tofauti tofauti ambao ni marafiki tu kwa maana ile ya Rafiki na si vinginevyo.
Mke wangu sio mtu wa kueleweka njseme hivyo, kuna muda kulitokeaga ugomvi ambao ulikuwa kwa sababu ya SIMU na hii ilitokea baada ya yeye kuchukua SIMU na kuangaza kufungua meseji za kawaida na WhatsApp na halo ugomvi ukaibuka.

Kosa langu ni "kumsifia mdada anamguu mzuri" na kwa sababu yeye mama yangu sijui kwa sababu hakujaliwa mguu wa Bia (Ila kajaliwa chura na umbo tu zuri Ila miguu yake ni ya kawaida) basi ikawa kesi tena kesi kweli kweli.

Na sio hivyo tu eti analalamika kwaninj Kila mwanamke ninayechati naye namwita "Mama" au "Boss" kisa hayo majina huwa namwita.
Sasa haya magomvi yakawa kama yameisha baada ya kumuomba msamaha. Mie hua sipendi kushika SIMU yake hata SIMU yake ikiita ataikuta mie sihangaiki nayo kabisa.
Hapa juzi kati daah, ile nimerudi home late mida ya saa tank kasoro alikuwa amechukia kisa nimerudi late.

Mie ninafanya kazi kwenye Pharmacy ambako ikifika usiku saa nne tunafunga ofisi. Turudi huku, Nimerudi home nikakuta chakula mezani nikala na nikawa nimeenda bafuni kuoga bafuni (Chumba ni Master) nikiwa naoga ikaingia meseji kwenye SIMU ndogo akanyanyuka kutoka kitandani haraka akawahi akasome meseji alipofungu meseji akakutana na meseji ya M- Pawa na nyingine ambayo haijafunguliwa ilikuwa inatoka kwa Mshikaji wangu nahisi ilichelewa kufika.

Kapekua SIMU yote hapakuwepo dudu lolote akaomba SIMU kubwa nikamfungulia password akaanza upekuzi. Yaani Kila meseji zenye jina la kike alikuwa anafungua na bahati mbaya anakuta nimemsifia mdada kwenye picha aloweka status na kumwita Mama ambayo yeye anataka nimuite yeye tu . Ila baadae anafungua inbox ya mdada huwa tunautani basi kakuta utani fulani na pia nimemwambia kuwa kama Ningekuwa Mwislam ningeoa Mke wa pili ambaye ni yeye. Halo ndipo ugomvi ukaanza tena. Na aliingia kote Ila ndio hivyo tena. Sasa hivi amenuna anataka aende kwao eti akili inikae sawa maana sitaki kuachana na tabia yangu ya kusifia wadada.

Mimi hii tabia ya kugombana kisa SIMU inanikera na mpaka anasema kwanini nachati na wadada sana daah. Huu naona kama niko jera kusema ukweli. Sasa najiuliza Inawezekanaje ukamwambia mwenza WAKO kuwa tusishikiane simu na akaelewa. Uhuru wa kuwa na faragha kwenye Ndoa haupo au ni kwamba ukioa hiyo faragha haipo??
 
Simu ya mkononi ni Mali ya mwenye simu na si vinginevyo.

Acha ashike akichoka ataacha.

Atakachokutana nacho ameyataka mwenyewe, wewe huhusiki.

Bila hata kuambiwa na mtu, Mimi sishiki simu ya mwenzangu Hadi niwe ninataka kuhakikisha jambo ambalo naona Kuna mwenendo tofauti, nikikuta namkumbusha Kuna maradhi naendelea na hamsini zangu.

Akibadilisha password na Mimi nabadilisha ya kwangu, na naificha hata uvunguni ili na yeye apate pressure , yaani nikiona anaanza kuwa makini na simu Mimi nafanya kusudi nazidisha umakini wa uongo.

Naweza kuingia jikoni nikaacha simu alipo Kisha narudi mbio kuchukua simu.

Basi ili mradi wote roho ziwe juu juu yaishe, nabaki nacheka
 
Mbinu zako ni noma sana, Ila nimezipenda
 
Mimi huwa nakagua siku moja moja. Ni vizuri kwa afya ya mapenzi yenu na ndoa kwa ujumla. Unataka nisijue mienendo yako na ww usijue yangu? Sasa maana ya mwili mmoja ni nini. Huku kushika simu ya mwenza wako hata kwa siri inaonyesha pia unajali na una mapenzi na huyo mtu,ikifikia stage kila mtu na awe na time yake hapo hakuna mapenzi wala ndoa.

Ww kama unajali mm sikukatazi kuchat na wanawake wengine ila heshima kwangu lazima iwepo...that means futa msg zako zote za ajabuajabu urudipo nyumbani,kweli kukuta msg kama hizo kwny simu ya mume na umeziacha tuu ni kama dharau.

Ndo maana vijana wa sasa ndoa zenu zinavunjika baada ya muda mfupi kwa sbb mnavimbiana sana ww unaleta uwanaume wako kwmba hupangiwi na mke nae hana uvumilivu amelelewa kiyai yai hajapitia shuruba na stress anaona isiwe tabu anasepa.
 
Umenena vyema, hii nimeichukua na nimepanga tu niwe naweka reminder ukikaribia muda wa kwenda home inikumbushe kufuta meseji za ajabu.
 
" stalking" Ni kitu kibaya Sana kwenye mahusiano maana hapo lazima mmoja atanasa kwenye mtego.

Ushauri wangu Ni vizuri kuwa wawazi( transparent) kwa wenzetu ili kuepusha ugomvi kwenye ndoa yenu.
Kuwa wazi kwamba vipi?? Uwe wazi kwamba nachati na marafiki wa like au niaje??
 
maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua 🤔🤔🤔

Back
Top Bottom