WIvu wa mapenzi janga linalohatarisha usalama wa jamii

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Hamjambo wanajf mko vp huko huku ni balida kabisa.Leo nimeona niwachane hawa jamaa wenye wivu wa kupitiliza wa mapenzi hivi kwanza hebu ncheke kwanza hahahaaaaa, hivi wewe kweli uko radhi hat kukill,au hta kudhuru kisa mapenzi.Kupenda kupo ila kiasi na kujidhibiti muhimu.

Nafikiri mmeshawahi sikia au kuona hil mambo.Hivi kwa nin lkn Kuna muda nawaza mpaka nasema daaaaa! Yaani kwenye hizi mambo za mapenzi Kuna watu wamejitoa ufaham balaa.

Kuna mdau mmoja alikuwa anaacha hata kwenda kazini eti kisa wivu(anamchunga mke)jamaa ameajiriwa lakini anachill hata siku kadha eti anamchunga mke,wakati mwingine atoke eti arudi ghafla ili akamfume mke kama labda kaleta mtu ndani akija hola.

"vp mme wangu mbona ghafla Kuna Nini"(mke anauliza). " acha kuuliz nakuja mda wowote ninaotaka kwanza nani usjekut ushaingiza mtu huku"(jamaa😂)Mara oh mara oh ugomvi.

mara kidogo anapekua simu ya mke "nani huyu katuma hii ,meseji"(jamaa) "ni rafiki yangu"(wife)"Nahisi Kuna kitu"(jamaa) Mara oh mara oh ugomvi.

Kuna jamaa yupo radhi agombane na marafiki kisa wivu wa mapenzi(ukiangalia zaidi uthibitisho Hamna)ila kuhisi tu)Ameshawahi kugombana na baba mkwe kisa wivu(baba mkwe alipiga simu usiku kwa mwanae)ikawa balaa nani kpiga,nani kapiga kuja kuthibitisha alikuwa baba mkwe wf ashachezea mikwaju😂

Eti unakuta mtu anakazi ya kupigia masela ake simu kaa mbali na mke wangu kaa mbali na mke wangu uhalisia hamna ni kushuku tu.

Upande mwingine wadada nao punguzeni wivu ,unakuta mdada akishaleta dada wa kz ni kumbaaaana eti asijemchukulia mme,inafika mahali hata anashindwa kutoka eti mfanyakazi asije muibia.Ashagombana na mashosti kisa mumewe "hahahaaaaaaa" kwani yeye ndyo ashakuwa sukari yao narudia Tena "hahahaaaaaaaa"

Halafu nanyie ambao mshaamua kujitenga wivu wa nn Tena.Unakut watu walishaachana ila wivu Tena unaingia km ishakuw hivyo Kila mtu si afanye yake.Unakuta mtu analeta Tena wivu na kumfanyia mwingine matendo mabaya/ukatili ilhali walishajiktaa.(eti kisa kamuona na Fulani)

Wengine kisa wivu wanadiriki hata kuwaendea wenza wao kwa kalmanzila na wanapokosea masharti ndyo kimbembe utaskia flan kawa chizi,mara flan kavurugwa, kumbe mwenza kahusika.

Jamani matukio ya ukatili kutokana na wivu wa mapenzi yamekuwa mengi jamani hebu jamii ijitathmini.

#Ukifuatilia hata kwenye vyombo vya habari matukio yanayotokana na ukatili wa kijinsia yamekuwa mengi, watu wmekuwa killed, wengine wamepata vilema vya kudumu,wengine hawana amani ktk mahusiano jamii Haina budi kubadilika
 
Back
Top Bottom