Wananchi walalamikia Mgodi wa Geita kuangamiza mifugo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Date::10/29/2008
Wananchi walalamikia Mgodi wa Geita kuangamiza mifugo
Na Mussa Juma, Geita
Mwananchi

WAKAZI 110 wa Kijiji cha Nyakabale, ambacho kinapakana na mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) wilayani Geita, mkoani Mwanza, wameilalamikia kampuni hiyo kwa kuendelea kutitirisha maji yenye sumu kwenye vijiji vyao na kusababisha mifugo yao kufa baada ya kunywa maji hayo na wengine kubabuka ngozi.

Mbali ya malalamiko hayo, wakazi hao, walionesha kukerwa na uamuzi wa viongozi wa mgodi huo wa kukataa kuwapatia fidia ya baada ya kuchukua mashamba yao kwa ajili ya machimbo hayo.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa maji hayo, yamekuwa yakiingia kwenye visima vya maji wanayotumia na hivyo kuwaathiri wao na mifugo yao.

“Hapa hatuna maji salama, yote yanasumu kutoka kwa wawekezaji, ng’ombe 22 wamekufa, mbuzi na hata mtu mmoja hivi sasa amepoteza maisha,”alisema Lugiko.

Alisema wamiki wa mgodi huo, wanapaswa kudhibiti maji hayo ili mifugo yao, isinywe maji hayo yenye sumu pamoja na kulinda afya za wakazi wa eneo hilo.

Kuhusu mashamba yao, wakazi hao, walisema kampuni hiyo, ilichukua mashamba yao, mwaka 2004 na kwamba waliolipwa fidia hadi sasa ni watu 39 tu.

Naye Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Kavuta Sitta alikiri kwamba wananchi hao, wanadai fidia hiyo kwa miaka kadhaa hivi sasa na hawajalipwa licha ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuagia walipwe.

“Ni kweli wananchi wanadai fidia na hakuna uhusiano mzuri na hawa wawekezaji na sisi kama Serikali ya Kijiji, kweli tumeshindwa,” alisema Sitta.

Wananchi wa kijiji hicho, walisema licha ya kutofidiwa pia wanaishi maisha ya dhiki, hakuna kituo cha afya kwamba barabara waliokuwa wakiitumia imefungwa na mgodi huo na wakitaka kwenda mjini Geita wanalazimika kutemeba umbali wa kilometa 33 badala ya kilometa 8.

Waandishi wa habari ambao wanatembelea migodi katika ziara inayoratibiwa na Jumuiya ya Kikisto Tanzania (CCT) hawakufanikiwa kuonana na viongozi wa mgodi huo, ili kufafanua madai hayo kwa kuwa waligoma kuonana na waandishi wa habari.
 
Back
Top Bottom