Wananchi waandamana kushinikiza serikali kutekeleza ahadi

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Nov 18, 2009
473
40
Wakazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyankulu (BGMCL) Wilaya ya Kahama mkoani hapa, wameandamana katika Kijiji cha Segese na kufanya uharibifu mkubwa wa barabara kuu iendayo mgodini kwa lengo la kushinikiza serikali kutekeleza ahadi iliyotolewa na vingozi wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Diwani Athumani, alisema wananchi hao waliandamana mwishoni mwa wiki bila kibali na kuchimba mtaro mkubwa katika barabara ya Kakola. Alisema licha ya kuchimba na kuharibu barabara hiyo kwa nia ya kuzuia magari kwenda au kutoka katika mgodi huo, wakazi hao waliweka vizuizi vya mawe na magogo barabarani.

Watu walishuhudia tukio hilo walidai kuwa polisi walifyatua risasi za mpira na za moto hewani na mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanakijiji hao na kusitisha maandamano hayo.

Inadaiwa kuwa sababu kubwa ya maandamano hayo ni kuwasilisha madai na malalamiko yao serikalini dhidi ya utekelezaji wa ahadi za viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake mwishoni mwa mwaka jana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Miongoni mwa ahadi hiyo ni kuwajengea barabara ya lami, kuondoa kero ya maji na uharibifu wa mazingira unaodaiwa kufanywa na mgodi huo.
Kamanda huyo alisema polisi wamewatia mbaroni watu 40 kwa tuhuma hizo.

Athumani alisema kati ya hao, 31 waliachiwa baada ya kuhojiwa na wengine wanaendelea kushikiliwa na kwamba watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.


CHANZO: NIPASHE
 
Kuna siku Serikali ambayo si sikivu itakuja kuelewa kilio cha wananchi ambao ndiyo wenye NCHI yao
 
Back
Top Bottom