Tunateseka kwenye foleni Kibaigwa (Dodoma) kwa zaidi ya saa tano, inadaiwa kuna msafara wa kiongozi

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Tangu asubuhi ya leo mida ya Saa 12 asubuhi (Januari 30, 2024) tumeweka kwenye foleni hapa maeneo ya Kibaigwa (Dodoma) na hatujui kinachoendelea, taarifa ambazo si rasmi inadaiwa kuna msafara wa Kiongozi wa Serikalini.

Jiulize kwa muda wote huo zaidi ya Saa tano inaelekea 6 hours hakuna magari yanayopita, hii ni sawa kweli? Shughuli za watu zinasimama kwa ajili ya msafara wa kiongozi kwa muda wa zaidi ya saa tatu, hii ni sawa kweli?

Makamu wa Rais alipiga marufuku Wananchi kusimamishwa muda mrefu kisa tu kiongozi anapita lakini naona dawa bado haijawaingia Makamu wa Rais Dkt. Mpango apiga marufuku Polisi kufunga Barabara kwenye Misafara

Sasa angalia tunavyoteseka:

9c6132b2-b5ab-4446-91e2-4c22e07d1ff0.jpg


8d57136b-152d-456c-94db-036ad0eaded1.jpg

086c13b5-d57e-4d13-9746-ce6a1d64df45.jpg

144ad42b-3e12-49f3-8fe5-a81aaf9368be.jpg

c47e21e2-224b-427a-90d8-025259c971ab.jpg
 
Hii tabia ya inakera kweli mimi nashauri wangefunga ata upande moja wa Barabara ili kupunguza foleni hizi Hali kama hii imezoeleka ,mtu anaeenda kutafuta riziki ya kula watoto anakaa daladala masaa 6 cjui jioni akirudi huyo kiongozi anaepita kama atamsaidia
 
Tatizo lililojitokeza ni mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Kongwa mkoani Dodoma, eneo la Mtanana kujaa maji na kusababisha kufungwa kwa muda kwa barabara ya Morogoro kwenda Dodoma kwa sababu ya usalama wa watumiaji.

Hii si mara ya kwanza kuwa na foleni ndefu wanapozuia magari kupita eneo hilo kama tujuavyo sote; kwamba msafara wa kutoka Morogoro unaweza kufika hata Pandambili si Kibaigwa tu, na kutoka Dodoma ukifika Narco Kongwa!

👇🏽👇🏽👇🏽

View: https://www.instagram.com/p/C2uArDCvNLD/?igsh=MWh6dHVud3N4eXowYw==
 
Back
Top Bottom