Wananchi tunaanza mgomo rasmi leo (PAKI GARI BARABARANI) kwa pamoja tunaweza kubadilisha nchi

huku Moshi balaa tupu! Mafuta yapo lakn kuuza hawataki, yaan inaonekana wamechimbwa mkwara mzito. Nimemtumia rafiki yangu masawe, wamegoma, anyway ameniambia niache dumu ataniletea jion. Nitafanyeje sasa! Watu hata undugu haupo kwa hili. Wana umoja wa achabu hawa wawekezaji.
 
that is done,nimeshahamasisha na wenzangu wote ofisini,bila kusahau na gesi pia imepanda bei, JK kubali umeshindwa
...Sipati picha huyu mkuu wa kaya wetu kama kichwani mwake haya yanayotokea Tz anayachukuliaje? Inasikitisha viongozi wa magamba wanachulia suala la mtu kupewa uraisi kama ni zawadi kila mtu anaweza kupewa tu matokeo yake ndio haya nchi kama haina kiongozi mambo shaghalabagala....Mwisho wa mwezi unamuona kwenye runinga eti uchumi unakuwa kwa kasi.....Mungu utuokoe na hili jinamizi....
 
Hawa viongozi wetu sijui vipi! Yaani hali ni ngumu lakini hawatoi tamko lolote.
 
Japo yote uliyoyataja juu yetu ni ya kweli kwa kiasi kikubwa sana kwetu; LAKINI KIUKWELI ROHO INANIUMA sana juu ya kauli hizi!!!!!!!!!!!

ujumbe huu si kwa watanzania ninaowafaham mm.watz
1.Ni waoga
2.Wazembe wa kufiri
3.Wanafanya maamuzi kinjaa njaa i.e mwenye hela ni tishio mpaka ikulu.
4.Hawajajua nguvu ya mitandao ya kijamii.
5.Akili zao zimefunikwa na magamba la chama
Kwa hyo ndugu yangu utaenda peke yako
 
Watanzani labda wengine, hawana ujasiri wa kugoma. Wapo wapo tu, watalalamikaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeee,
Mwisho kama kawaida watamsingizia Mungu
 
Jaji Makame, ni hapa ndipo ulipotufikisha mara baada ya kusaidia kukwapuliwa kwa kura zetu hapo mwaka jana. Natamani kukuona sura yako ulivyo kwa wakati huu ambapo taifa la Tainzania moja kwa moja tunaelekea shimoni kwa msaada wako wewe!!!!!!!!!
...Huyu mzee namchukia sana. bado nina kumbukumbuku siku alipokuwa anatangaza matokeo yauraisi akiwa ameshusha miwani yake ile i wish angekuwa karibu yangu nadhani ningemkosea adabu kabisa. Watu wanaendekeza njaa zao huku wanatuharibia nchi..
 
Watanzani labda wengine, hawana ujasiri wa kugoma. Wapo wapo tu, watalalamikaaaaaaaaaa weeeeeeeeeeee,<br />
Mwisho kama kawaida watamsingizia Mungu
<br />
<br />
Weye ndio unaonesha uoga! Stop being negative au usichangie post! Mnanikera aaghrrrr!!!!!!!
 
Haya sasa, utani utani huu mwisho kweli
wandugu naomba kuwataarifu kwamba leo tutaanza mgomo rasmi wa kuikataa serikali kwani imeshindwa kufanya maamuzi muhimu kwa taifa kama vile mafuta, umeme ufisadi na kero nyingine mbali mbali ambazo wanazijua wamefikishiwa bila majibu.

so leo ifikapo saa 11 jioni muda wa kutoka maofisini ukishaingia kwenye main road funga vioo vyako zima gari shuka kuashiria kuikataa serikali na kuishiwa mafuta. kumbuka huu ni wito kwa watanzania wote na tunaimani tuko pamoja kwa ni sasa tumechoka serikali isiyokuwa na maamuzi muhimu na magumu.


PAKI GARI HAPOHAPO KWENYE MAIL ROAD MARA BAADA YA KUINGIA KWA MAIROAD. WATANZANIA KWA PAMOJA TUNAWEZA
 
Nafikiri tutafute njia ya kuanda maandamano na migomo, i believe tutafanikiwa tu.
 
Main roads zimejaa magari yaliyotelekezwa?? Ni saa kumi na mbili sasa...
 
Ndugu zangu watanzania wenzangu nimeamini ni waoga sana. jana mimi nilifika bagamoyo road maeneo ya kati ya victoria na makumbusho nikapaki gari nikawasha double hazard nikashuka sikuona hata mmtu mmoja aliyefanya hivyo kwa dakika takriban kumi na saba.
 
Back
Top Bottom