Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Mwnaukweli hii umenena, lakini maoni yangu ni kuwa wanaoleta haya si wananchi na wala si kukosa elimu. Wanaoleta haya ni watu wenye elimu na wanafanya kwa manufaa binafsi. Je Mtwara hakuna mtambo wa kufua umeme kwa gesi? Kwanza mimi binafsi nafikiri matumizi gesi kwa kuiunguza na kuzalisha umeme tu haitatusaidia kimaendeleo. Tunahitaji kufanya zaidi ya hapo kuona kuwa gesi yetu inalifaidia taifa. Tusiwaaminishe wananchi kuwa matumizi ya gesi ni kuzalisha umeme tu na kuwa gesi itamaliza kabisa tatizo letu la umeme!
Mie mkuu naona watu wamekata tamaa.

Wameona wanapuuzwa na watawala, hayo mengine yanakuja baada ya hilo. Watu wa Mtwara huko nyuma walikuwa na msimamo imara kisiasa wakiunga mkono serikali kwa kila kitu. Umaskini ndio umewafanya wakate tamaa.

Ni point ya kufanyia kazi bila hata kujali nani yuko behind.

Wenye mamlaka watakuwa na uwezo wa kuchuja ukweli na upotoshaji katika haya. But serikali ikiamua kupuuza au kutumia udikteta, itakuwa kosa kubwa kisiasa.
 
..... Haijaniingia akilini... wanaandamana kuzuia gas isije Dar? inaamaana ikija Dar itaisha wao watakosa au? Hapo najiuliza iwapo kila mkoa utaamua kuzuia mali zilizoko katika maeneo yao ingekuwaje katika Tz? .....

we kweli pilau...wanachotaka ile processing ya ku add value ya gas ifanyike mtwara,hawajasema wanataka kubaki nayo watumie peke yao, so kama ni viwanda vya kuiprocess gas kwa kuuza vijengwe mtwara....pia itakuwa ni ajabu gas inayozalishwa mtwara ikaanza kutumiwa na wanadaslam....faida yake ni kwamba miundombinu kama barabara zitaboreshwa,ajira zitaongezeka,biashara zitafanyika sababu ya population kuongezeka,mzunguko wa fedha utaongezeka pia....cha muhimu zaidi ni mrahaba....sasa wewe pilau bila kachumbari usiwe unaropoka kama kitu ujakielewa.
 
sisi watanzania ni watu wa ajabu sana!leo watalalama,wataandandamana na kutoa kila aina ya hisia zao kupitia mabango ila cha ajabu ukija uchaguzi wanachagua watu wale wale tena kwa kura nyingi tu.sasa sijui tumelogwa au ni uwendawazimu!majibu sipati.

wakichaguliwa wengine si wanaiba??nani kakuambia ccm inashinda kihalali bila hila??
Tandahimba cuf walishinda wakaiba,lindi kuna mbunge wa cuf hata kuiba wakajiskia vibaya

2015 tunaondoa mzimu huu wote uliobakia

na watatoka tuh,ujinga hatutaki sasa
 
Hizi NGOs na vyama vinavyoshabikia maandamano ya watu wachache wa Mtwara watueleze yafuatayo:-

1. Uzalishaji wa gesi unaofanyika Mtwara
2. Watumiaji wa gesi mkoani Mtwara

Wananchi wasikubali kutumiwa na watu wanaotaka kupata maslahi yao kupitia maandamano

Merry X-mass mzee.....
ChristmasTree_zps7a630f9d.jpg
ChristmasTree_zps7a630f9d.jpg
 
we kweli pilau...wanachotaka ile processing ya ku add value ya gas ifanyike mtwara,hawajasema wanataka kubaki nayo watumie peke yao, so kama ni viwanda vya kuiprocess gas kwa kuuza vijengwe mtwara....pia itakuwa ni ajabu gas inayozalishwa mtwara ikaanza kutumiwa na wanadaslam....faida yake ni kwamba miundombinu kama barabara zitaboreshwa,ajira zitaongezeka,biashara zitafanyika sababu ya population kuongezeka,mzunguko wa fedha utaongezeka pia....cha muhimu zaidi ni mrahaba....sasa wewe pilau bila kachumbari usiwe unaropoka kama kitu ujakielewa.

muulize atuambie vizuri,yy ni pilau au bwabwa??
Ss tunakula vyote vyote mapilau na mabwabwa kama yeye

kama hajui kinachozungumzwa apige kimya,watu tunatetea kizazi chetu kijacho,hiki cha kwetu kishagharimika na hawa mafisi ahadi wa ccm
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

Wawakilishi hawafnyi ya wananchi bali ya chama na binafsi. Wacha people zifunguke kudai chao
 
we kweli pilau...wanachotaka ile processing ya ku add value ya gas ifanyike mtwara,hawajasema wanataka kubaki nayo watumie peke yao, so kama ni viwanda vya kuiprocess gas kwa kuuza vijengwe mtwara....pia itakuwa ni ajabu gas inayozalishwa mtwara ikaanza kutumiwa na wanadaslam....faida yake ni kwamba miundombinu kama barabara zitaboreshwa,ajira zitaongezeka,biashara zitafanyika sababu ya population kuongezeka,mzunguko wa fedha utaongezeka pia....cha muhimu zaidi ni mrahaba....sasa wewe pilau bila kachumbari usiwe unaropoka kama kitu ujakielewa.

Mkuu wamche pilau aende shimoni..manake ni jana tu tumemla nadhani sasa hivi atakuwa keshapelekwa choo cha shimo!!!! Lol
 
mkoa wangu upo nyuma sana, hizo tetesi za kukataliwa hawa wa ghasia zilianza kama mzaha sasa zinajitokeza. gas inapelekwa dar wenyewe hatufaidiki wapi na wapi?

Hapo red ni kwamba huyo Hawa Ghasia alikataliwa tangu mwanzo wa kuogombea kwake 2005 wakati JK alipokwenda Mtwara kwenye kampeni ya Urais. Wananchi walimwambia JK aondoke na Hawa Ghasia hawamtaki. Lakini kwa vile Ghasia ni swaiba wa Salma JK, ikabidi ilazimishwe agombee na ashinde kwa hali yoyote. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Utumishi na kule aliendeleza ghasia tu. Juzijuzi walimzomea na Mkuchika wake. Hao wote, Ghasia na Mkuchika ni baadhi ya viongozi mabomu wa JK. Mtwara kazaneni na kupigania haki yenu.
Kule Kahama kuna mgodi mkubwa wa dhahabu - Buzwagi - lakini ndege inatua mgodini na kubeba dhahabu kupeleka Ulaya na mji wa Kahama ni mbovu sijapata kuona. Barabara ni mashimo tu, hali ya wanakahama ni duni. Huo ndio utaratibu wa Serikala ya Magamba.
 
Naomba na ajitokeze mtu na
aeleze faida ya Gesi ya Mtwara kubaki Mtwara...

Pia aeleze hasara za gesi ile kupelekwa katika miji mingine kama
Darisalama....Kwa watu wa Darisalama, kwa watu wa Mtwara na Kwa
Watanzania wote....

kama noma na iwe noma,mjadala huu haujaanza leo,serikali ya ccm ni kiziwi,mtwara komaeni,mtaji wa maskini ni rasilimali za nyumbani kwake.
 
Wawape Umeme wa uhakika kupitia gas Yao, wapike chakula kupitia gas Yao kwanza kabla ya mkoa mngine kufaudika na gas hiyo na progress zote zifanyike mtwara Na sio Dar ili watu wapate Ajira na pato litokanalo na gas liwanufaishe wao kwanza, maji safi, barabara nzuri, shule za uhakika na hospitali zenye dawa na watendaji bora kwanza, that's it. Wamakonde wakiweza hata wamasai wataweza.

.
muulize atuambie vizuri,yy ni pilau au bwabwa??Ss tunakula vyote vyote mapilau na mabwabwa kama yeyekama hajui kinachozungumzwa apige kimya,watu tunatetea kizazi chetu kijacho,hiki cha kwetu kishagharimika na hawa mafisi ahadi wa ccm
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

nanii nduguuu yakooo weweeeee inamaana chadema ndio wameandaaa maandamanooo tumiaa akili nduguu yanguu watuu wanaakili si kamaa unavyofikiriaaa m4c with no apologic
 
safi sanaaaaaaaaaaa!!! na mlima Kilimanjaro ungekuwa mobile haki ya nani ungekuta uko nje ya nchi hii kwa ulafi wa watu fulani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom