Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Mkuu nakuunga mkono kwa hoja yako! Dar imejaa, haikaliki sasa hivi kwa sababu ya kulundika kila kitu huko! Maendeleo yawafuate watu na sio watu wanyang'anywe rasilimali kisha waanze kuzifuata Dar!

imagine watu wanawaza kujenga flyovers Dar kwingine watu hawana maji wala dispensary! Huu ni ushetani. Natamani mafuriko yarudi Dar
 
MAFILILI ,Acha kutuona sisi Maboya narudia tena ,wewe unataja tu majina ya watu na vyeo vyao,mbona hao unaowataja hatuwaoni wakizungumza lolote kuhusu hii Saga?,Huyo M bunge Murji amefuatwa Ofisini kwake awaoneshe wana Mtwara Mkataba wa kusafirisha Gas anasema hata yeye hana (ukumbuke huyu ndiye aliyesema wana Mtwara wamekubari Gas iondoke tu hawana tatizo) ,Mayor hana majibu yoyote,Hiv MAFILILI hawa watu wanakupa nini wewe?
 
Maslahi ya kitaifa unayoongelea wewe ni yapi zaidi ya haya ya kuwawezesha wananchi kwa kutumia rasilimali za Nchi?

Hawa wamakonde waachane ne umimi watambue gesi ni maalisili ya kitaifa kwa faida ya watanzania wote waliotapaa sehemu mbalimbali za nchi
 
Tatizo sio kutompelekea mlaji..tatizo hapa ni kwa nini production isifanyike mtwara walau wananchi wa huko waambulie hata ajira ili waweze kuendesha maisha yao!.....

'production' gani unazungumzia maana mpaka sasa inafanyikia Mtwara. Ikiwa ni matumizi ya product - yaani gas - si raisi kwa idadi yote kutumika Mtwara, ndiyo maana lazima ingine iwe 'exported' kwa walaji wengine. Sasa Mtwara wadai mapato ya hii 'exportation' na siyo kuzuia. Hii inahitaji kubadili mfumo wetu wa utawala na uchumi.
 
MAFILILI: CHADEMA inahusika vipi tena hapo we ukilala ukiamka unawaza CHADEMA tu, wao wamekwambia GAS kwanza vyama na siasa baadaye.

Mkuu unajua kuna watu chadema inawakosesha usingizi kabisa,kila kitu kinachohusu HAKI lazima waseme ni CHADEMA kama ni hivyo basi CCM ipo kwa ajili ya DHULUMA NA WIZI.
 
=Thesi;5315429]Hivi hiyo gesi ikibaki mtwara bila kupelekwa Dar ndo itawafaidia nini? Rasilimali ni vizuri ikajulikana ni za nchi wala siyo Mkoa, Wilaya au kanda. Kama Mtwara ungekuwa jiji lenye watu wengi na matumizi makubwa na fursa ya kutumia gesi ikapelekwa Dar na kuacha Mtwara hapo kungekuwa na tatizo.


Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu


Good move kama wameruhusiwa...but waangalie wasivunje tu sheria!

Sera ya Majimbo ya CHADEMA ndiyo suluhisho ya haya mambo. Tukisema mnasema tunaleta ukanda. After all Dar es Salaam ishakuwa congested na utitiri wa viwanda. Ni wakati sasa viwanda vijengwe nje ya Dar es Salaam ili ku-balance maendeleo. Na unga mkono hoja, kiwanda kijengwe Mtwara. After all itatusaidia kupunguza mafoleni hapa mjini maana wafanyakazi wa hicho kiwanda watabaki huko huko Mtwara na Magari yao.

TUMBIRI (Upanga, Dar es Salaam - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com

Nakala: Mwita Maranya, Daudi Mchambuzi, Sikonge, etc
 
Mtwara hamna lenu,mulikuwa wapi muda wote mradi ulipoanza mpaka umekamilika nyie ndio munapinga? Si niliwaona mukimwimbia Jk mapambio siku aliyokuja kuzindua mradi? Au siku ile mlidhani gesi itatoka dar ije mtwara kupitia bomba hilo?mutaandamana!mutapigwa na gesi itaondoka na mtabaki na vibatari vyenu!!maafisa wa Tiss wapo njiani wanakuja kumjua kiongozi wa maandamano hayo.Tumewasikia,Tutawafikia.
 
Mimi mwenzenu mgumu kuelewa, hebu nisaidie tafsiri ya hii kauli "Gesi haitoki Mtwara NG'O"

Ina maana dhahabu zinazochimbwa Kahama, zisitoke Kahama, Almasi za Mwadui zinabaki Mwadui?

Maharage yakitoka Mbeya kwenda Mtwara, sisi wa Dar tunatakiwa tuchaji kodi ya barabara?

Wananchi wa Mtwara wanataka final production ifanyike mtwara ili na wao wapate fursa mbalimbali za kiuchumi.sasa wakisafirisha gesi ghafi wananchi wa Mtwara watanufaikaje?
 
'production' gani unazungumzia maana mpaka sasa inafanyikia Mtwara. Ikiwa ni matumizi ya product - yaani gas - si raisi kwa idadi yote kutumika Mtwara, ndiyo maana lazima ingine iwe 'exported' kwa walaji wengine. Sasa Mtwara wadai mapato ya hii 'exportation' na siyo kuzuia. Hii inahitaji kubadili mfumo wetu wa utawala na uchumi.
Shida imeanzia kwenye kuelimisha wananchi nini kinafanyika na wao wanafaidikaje.

Kwa mfano mitambo ya kufua umeme wa gesi imejengwa Dar, kwa nini isingejengwa Mtwara?

Hii inakuwa political issue mkuu. Kama watu hawaelewi waelimishwe na si kulaumiwa. Watu wa Mtwara wanaona wamebaguliwa katika maendeleo ya nchi. Wanataka waone hatua za wao kushiriki maendeleo hayo.
 
MAFILILI ,Acha kutuona sisi Maboya narudia tena ,wewe unataja tu majina ya watu na vyeo vyao,mbona hao unaowataja hatuwaoni wakizungumza lolote kuhusu hii Saga?,Huyo M bunge Murji amefuatwa Ofisini kwake awaoneshe wana Mtwara Mkataba wa kusafirisha Gas anasema hata yeye hana (ukumbuke huyu ndiye aliyesema wana Mtwara wamekubari Gas iondoke tu hawana tatizo) ,Mayor hana majibu yoyote,Hiv MAFILILI hawa watu wanakupa nini wewe?

Nabwada uwe mkweli; hivi gesi ikisafirishwa hadi DSM, nyie watu wa Mtwara mtashindwa kuendelea na shughuli zenu za uzalishaji mali. Mie nafikiri mnatumia pasipo wenyewe kujitambua.
Manufaa ya kuwepo kwa gesi yameshafika Mtwara kama vile kuwepo kwa shughuli nyingi za kuingiza kipato tofauti na kabla ya gesi kama vile radio fm ziko nyingi, nyumba za kulala wageni zina soko, biashara kwa ujumla zinalipa siku hizi.
Muelewe gesi inayopangwa kupelekwa DSM ni ziada.
Kiwanda cha cementi kinachojengwa Mtwara hakitaweza kumaliza matumizi ya gesi iliyoko Mtwara hivyo haitakuwa rahisi kurudisha gharama za uzalishaji
 
Maandanano ni haki ya kikatiba, ukiona mtu anaandamana anajitambua, usiyejua umuhimu wa gas kubaki mtwara nenda shule ukatoe ujinga, soma historia kukua kwa miji kunatokana na nn, urbanasation miji kama Johanesburg, Captown, Pritoria imeendelea kwa sababu gani, ss wamakonde wa leo si wajana tunahitaji kupiga hatua na kuacha kukimbilia mjini, gas kwanza vyama baadaye.
 
Ssi watanzania tuna mapungufungu katika support pale inapohitajika ,Wanamtwara Big up sana Gesi ibakie mtwara .Faida kibao mtapata kama jamii zilizozungukwa na migodi .Naamin hakuna siasa ndani ya hili .
 
ikipelekwa Dar ndio issue ya ukanda inakufa?? kwa nini kila kitu Dar?? umeme ukifuliwa huko hautafika Moshi au Iringa au Mara?
 
Naipenda nchi yangu Tanzania, ukombozi wa kweli u karibu zaidi. Dhulma na unyanyaswaji umetufundisha somo kubwa na sasa tumeamka hakuna kulala tena ni mapambano mpaka kieleweke.
 
DSC02574.JPG
 

Similar Discussions

46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom