Wananchi Msata wafunga barabara itokayo Arusha

Kulala barabarani ni kuwavuruga/kuwasumbua wapita njia wasiohusika bure. Stratergy nzuri ingekuwa kumfungia njia mbunge au diwani wao.
 
hii nchi sasa ni migomo tu hadi kieleweke, wanatakiwa walale siku jk anapoenda kwao bagamoyo
 
Nimepita hapo leo kama nilivyoahidi jana , Kuna matatizo ya kiuongozi katika
Vijiji hivyo , Wengi wa wanavijiji wanamlaumu kiongozi mmoja wa chama
tawala eneo Kwa kupandisha Bei ya Maji Katika Gari moja ambalo huwa
linasambaza maji katika vijiji hivyo , Yaani maji yanachukuliwa Wami
wanauenda kuwauzia wanavijiji na wauzaji ndio hao viongozi wao , Kwenye
vijiji hivi pia kuna miradi ya maji inayofadhiliwa na NGO zingine lakini
sikuweza Kuwasiliana na NGO hizo kutokana na Muda wangu mchache , Lakini
wanavijiji wameonyesha kuamka na kutaka mabadiliko kwenye Eneo lao .
 
Oyaa!! Msata kuna maji tena mengi sana ya bomba, yanatoka Mto Wami, yanapita Msata then Chalinze.

Huu uzushi, labda kama wamegomea madudu mengine sio maji.

Tanzania ina maji mengi tu, sio Msata pekee - Maziwa makubwa matatu, Maziwa madogo madogo mengi tu na Mito na Vijito.

tatizo ni kwamba hayo maji hayajafikishwa kwa wananchi! Msata ninayoifahamu mimi ni asilimia 5% wanaopata maji ya bomba! Bomba kupita eneo fulani sio kigezo cha ile sehemu kupata maji ya bomba - labda kwingineko na sio Tanzania - nenda kule Kahama ulizia ule mradi wa bomba kutoka ziwa victoria umepitia katika vijiji vingapi na je hivyo vijiji vinapata maji ya bomba?
 
Nimepita hapo leo kama nilivyoahidi jana , Kuna matatizo ya kiuongozi katika
Vijiji hivyo , Wengi wa wanavijiji wanamlaumu kiongozi mmoja wa chama
tawala eneo Kwa kupandisha Bei ya Maji Katika Gari moja ambalo huwa
linasambaza maji katika vijiji hivyo , Yaani maji yanachukuliwa Wami
wanauenda kuwauzia wanavijiji na wauzaji ndio hao viongozi wao , Kwenye
vijiji hivi pia kuna miradi ya maji inayofadhiliwa na NGO zingine lakini
sikuweza Kuwasiliana na NGO hizo kutokana na Muda wangu mchache , Lakini
wanavijiji wameonyesha kuamka na kutaka mabadiliko kwenye Eneo lao .

Picha mkuu....!
 
Kwa mujibu wa magazeti ya leo eneo hilo ni MKATA na sio MSATA na tatizo ni kuwa kuna mheshimiwa mmoja alikuwa anatumia gari lake na kuwauzia wananchi dumu shilingi 500 ndipo akajitokeza mwingine ambaye alianza kuwazia wananchi dumu shilingi 300 ambapo fitna zilifanywa na gari lake kukamatwa ndipo wananchi wakaamua kuwa ... imetosha! Tukiamua, Tunaweza!
 
Back
Top Bottom