Wananchi Msata wafunga barabara itokayo Arusha

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kuna taarifa nimepata dakika si chache zilizopita kuwa wananchi maeneo ya Msata wamelala barabarani ili kudai maji kwani serikali haiwasikilizi walichoona ni bora kufanya ni kufunga barabara itokayo Tanga/Arusha kwa kulala barabarani. Magari hayawezi kwenda Dar wala Moshi/Tanga mpaka kitakapoeleweka.

Habari zaidi tutaendelea kufahamishana
 
Watanzania wa sasa sio wa wa miaka 10 iliyopita, kama serikali haitoi huduma muhima ni kuoma tuu mpaka kieleweke
 
Wakati huo huo muda si mrefu raisi wao amesema ameboresha kwa kiwango kikubwa sana "maisha bora ya mtanzania"!!
 
Niliwahi kuonya kuhusu serikali kuamua kupanua barabara ile bila kutoa huduma zingine za msingi kama hizo , gharama za kupanua barabara hizo si zingeweza kutosha kuwaongezea wananchi hao huduma wanazozitaka ?

Angalia hata hizo karakana za kupanua hizo barabara yaani ziko maeneo ya misitu wanachafua mazingira kabisa kule gharama zake ni kuwa mno kuweka karakana kule hata kama ni karibu na maeneo husika ya kutanua barabara hiyo kesho nitapita njia hiyo mimi mwenyewe nishuhudie
 
Wataondolewa na FFU muda si mrefu kama kawaida, lakini "Message sent"
 
Hivi msata ni jirani zake!? Mara hii alishawasahau kama hawana maji! kazi kweli kweli
 
Wale walilala barabarani Tanga walifanikiwa madai yao? na wazee wa EA nao je walifanikiwa? kama ndivyo basi hiyo ndo itakuwa stail ya kudai tunachotaka.
 
Niliwahi kuonya kuhusu serikali kuamua kupanua barabara ile bila kutoa huduma zingine za msingi kama hizo , gharama za kupanua barabara hizo si zingeweza kutosha kuwaongezea wananchi hao huduma wanazozitaka ?

Angalia hata hizo karakana za kupanua hizo barabara yaani ziko maeneo ya misitu wanachafua mazingira kabisa kule gharama zake ni kuwa mno kuweka karakana kule hata kama ni karibu na maeneo husika ya kutanua barabara hiyo kesho nitapita njia hiyo mimi mwenyewe nishuhudie

Usisahau digital camera utuwekee picha!
 
Hebu fanya utafiti kama lile bomba kubwa linalopeleka maji Bagamoyo toka mtambo wa Ruvu Juu, linapita Msata. Kama ni hivyo, then ni halali yao kufunga barabara maana wamechoka na upendo wa mama 'boga' ambaye anasuka sana mikeka lakini wanae wanalala chini. Mabomba yapite wapi na maji wapate nani?.Wakisikilizwa watahamasisha vile vijiji ambavyo umeme wa grid ya taifa inavipitia kupeleka umeme sehemu nyingine na wao wakibaki gizaniNa mwisho kabisa inaweza kuwafungua macho watanzania wengi zaidi itakapofika Octoba 2010 kila mmoja akasema "Sidanganyiki".
 
Hivi msata ni jirani zake!? Mara hii alishawasahau kama hawana maji! kazi kweli kweli
Oyaa!! Msata kuna maji tena mengi sana ya bomba, yanatoka Mto Wami, yanapita Msata then Chalinze.

Huu uzushi, labda kama wamegomea madudu mengine sio maji.
 
Hebu fanya utafiti kama lile bomba kubwa linalopeleka maji Bagamoyo toka mtambo wa Ruvu Juu, linapita Msata. Kama ni hivyo, then ni halali yao kufunga barabara maana wamechoka na upendo wa mama 'boga' ambaye anasuka sana mikeka lakini wanae wanalala chini. Mabomba yapite wapi na maji wapate nani?.Wakisikilizwa watahamasisha vile vijiji ambavyo umeme wa grid ya taifa inavipitia kupeleka umeme sehemu nyingine na wao wakibaki gizaniNa mwisho kabisa inaweza kuwafungua macho watanzania wengi zaidi itakapofika Octoba 2010 kila mmoja akasema "Sidanganyiki".

Bomba la Ruvu juu halipeleki maji Bagamoyo,Linaanzia Mtambo wa Mlandizi (Ruvu Juu) na kuambaa na Morogoro Road mpaka Kimara-DSM.
Bagamoyo wanapata maji toka Mtambo wa Ruvu chini ambao upo mbele ya Bagamoyo na yanapita na Bagamoyo Road mpaka Matank ya UCLAS.
Pengine Msata walipaswa wapate maji toka Mtambo wa Wami ambao unapeleka maji Chalinze.
 
Oyaa!! Msata kuna maji tena mengi sana ya bomba, yanatoka Mto Wami, yanapita Msata then Chalinze.

Huu uzushi, labda kama wamegomea madudu mengine sio maji.

Inawezekana uzushi kwa kuwa kama Chalinze wanapata maji toka wami,iweje wao wakose na yanawapita?
 
..Hiyo ni kali wanafanana na waliokosa usafiri wa RITES toka India kwenda Kigoma. Pamoja na hayo mkuu wa kaya kasema hayo yote sawa maadamu mnaonyesha hisia zenu kwake jambo ambalo ameliita muhimu sana lakini si kutatua matatizo yenu...

kidumu .....
 
Oyaa!! Msata kuna maji tena mengi sana ya bomba, yanatoka Mto Wami, yanapita Msata then Chalinze.

Huu uzushi, labda kama wamegomea madudu mengine sio maji.
I see,

You might be right and also wrong :)

RC wa Shinyanga alisaidia kuweza kuongea na wananchi wakaachia njia.

Ni kuwa walikuwa wanauziwa maji na mtu mmoja wa eneo hilo kwa Tshs 500/= kwa dumu moja, akaja mwekezaji mzalendo mwingine akawa anauza kwa Tshs 300/= kwa dumu hivyo wengi wa wananchi wakamkimbia mwekezaji wa awali kwakuwa alikuwa aghali. Tatizo likaja baada ya mwekezaji mpya huyo wa maji mwenye bei pungufu kuwekewa mizengwe na kulazimishwa kuondoka eneo hilo kitu ambacho raia waliona ni uonevu kwao na wakaona suluhu ni kulala barabarani ili kutuma ujumbe serikalini.

Wameondoka eneo hilo na tukio limechukua takribani saa 1 unusu hivi.
 
Kwa sasa hivi ili kufikisha ujumbe serikali dawa ndo hiyo mnafunga barabara mpaka kieleweke
 
Kwa sasa hivi ili kufikisha ujumbe serikali dawa ndo hiyo mnafunga barabara mpaka kieleweke
Nafikiri itafutwe Strategy nyingine ,serikali ishakuwa sugu,Wazee wa iliyokuwa East Africa Corporation walifunga barabara na wakachuniwa vilevile.Masikini wazee wale sijui walifikia wapi na madai yao?
 
Back
Top Bottom