Wanamuziki waliowahi kutoa nyimbo zilizokuwa mbele ya wakati wao

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,359
22,921
WANAMUZIKI WALIOWAHI KUTOA NYIMBO ZILIZOKUWA MBELE YA WAKATI WAO

Nawasalimu kwa jina la chama pendwa CCM. Namshukuru Mungu tumefika leo salama. Ninafurahi kuufunga mwaka nikiwa nimeandika uzi mzuri wa kisomi. Siku za hivi karibuni wengi wenu mmenisihi niseme neno kuhusu tamko la Spika Ndugai dhidi ya uongozi wa Rais Samia Suluhu kuhusu mikopo. Kwa kifupi kabisa niseme kwa lugha ya kibeberu "The message is right but Ndugai is a wrong messenger".

Turudi sasa kwenye lengo la uzi. Hapa ni majina ya wanamuziki na nyimbo walizotunga ambazo ni kali hadi leo na zitaendelea kwa kali. Ni kama vile hawakuwatungia watu wa wakati wao. Walikuwa mbele ya muda. Hii list ni wanamuziki wa aina zote, wa zamani na wa sasa. Twende pamoja;

1. Papa Wemba;
Haina ubishi hayati Papa Wemba toka Congo alikuwa mbele sana ya muda wake. Vibao MARIA VALENCIA, SHOW ME THE WAY na WAKE UP (feat Koffi) ambavyo havikuwa na masebene ya kilingala ambavyo hadi leo vikipigwa ni moto. Vilitoka wakati masebene yakiwa ndo habari ya mjini... hitsongs karibu zote zilikuwa ni sebene za hatari. Lakini leo hii zile sebene hazina nafasi mbele ya hivyo vibao.

2. R Kelly;
Huyu mwamba toka Chicago USA ambaye ni mfalme wa R&B kafanya kila kitu alichotakiwa afanye kwenye muziki. Wimbo wake FIESTA nauchukulia kama wimbo ulitoka kabla ya wakati. Ladha yake ni tamu hadi leo.

3. Tabora Jazz Band;
Hawa wakali wa miaka ya 70 walitoa hitsong RANGI YA CHUNGWA ambayo hadi leo kwenye sherehe za harusi huwa inapendwa. Watu wazima wanaelewa zaidi.

4. Kilwa Jazz Band;
Hitsong yao ni NAOMBA NIPATE LAU NAFASI. Kaisikilize hutajutia.

5. Mbilia Bel;
Huyu mama yetu kutoka DRC ni legend asiyechuja. Ana nyimbo nyingi kali za rhumba lakini wimbo wake NAKEI NAIROBI hadi leo hii ukipigwa ni balaa.. ni rhumba moja matata sana. Halafu huyu mama mbona hazeeki? Bado ana shepu moja matata sana ingawa sura inamsaliti kwa kuanza kuonyesha uzee.

6. King Crazy GK;
GK akiwa na East Coast Team walitoa hits nyingi lakini TUTAKUKUMBUKA DAIMA na HII LEO hata zikipigwa leo bado zina utamu wa hali ya juu.

7. Rose Muhando;
Huyu mama nadhani anakubalika nje ya Tanzania kuliko ndani. Hadi mwaka 2014 pale Nairobi city centre ilikuwa ni ngumu kutembea hata mita 300 bila kusikia wimbo wake ukipigwa. Kwangu mimi NIPE UVUMILIVU ni wimbo ambao utaishi siku zote.

8. Ali Kiba;
MAPENZI YANA-RUN DUNIA ni wimbo bora wa muda wote.

9. Koffi Olomide;
Wimbo SI SI SI akimshirikisha mwanadada Coumba Gawlo ulitungwa wakati ukiwa hauhitajiki sana. Lakini miaka kadhaa baadae ndo thamani yake inazidi kujulikana. Pia kibao ANDRADA ni hit ya muda wote. Viva Koffi.

10. Shilole/Shishi baby/Shishi Trump;
Huyu mkali wa bongo fleva ana hitsongs nyingi sana ila wimbo wake PAKA LA BAR ndo wimbo bora wa muda wote. Huu wimbo ulitoka kabla ya wakati wake. Mkausikilize tena.

NB: Hiyo list sijaiweka kwamba wa kwanza ndo bora zaidi. PIA WANAJF TUNAWEZA TUPIA NYIMBO BORA ZA WAKATI WOTE ILI TUKASIKILIZE.
 
The One and Only 2Pac, unaweza kumsikiliza siku nzima na usimchoke coz his punchlines hit harder
images (5).jpeg
 
Huu uzi upo hapa kwa hisani ya wazee wa JF
Hongereni mababu zetu....ila ukweli ni kwamba nyimbo nyingi hapo juu zina wahusu wazee isipokuwa No 6,7,8 na 10.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom