Wanajeshi wa Russia waingia kambi ya wanajeshi wa Marekani nchini Niger

LINGWAMBA

JF-Expert Member
Sep 30, 2023
460
1,076

Screenshot_20240504-173107.jpg

Wanajeshi wa Russia wameingia katika kambi ya Jeshi la Anga la Niger ambayo pia ina wanajeshi wa Marekani baada ya serikali ya Niger kuamuru vikosi vya jeshi la Marekani kuondoka nchini humo.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amethibitisha tukio hilo leo Ijumaa huku akisema kuwa hakuna wasiwasi mkubwa kwani wanajeshi wa Russia hawatawafikia wanajeshi wa Marekani wala vifaa vyao.
Siku ya Alhamisi, afisa mwandamizi wa kijeshi wa Marekani ambaye hakutaka jina lake litajwe alifichua kwamba wanajeshi wa Russia tayari walikuwa kwenye Kituo cha Jeshi la Anga cha 101 karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani huko Niamey, mji mkuu wa Niger, lakini hawakuwa wakiingiliana na vikosi vya Marekani.
Taarifa za kutumwa askari wa Russia kwenye kambi hiyo ya jeshi la anga la Russia ziliibuka baada ya Niger kuifahamisha Marekani mwezi Machi kwamba inapaswa kuwaondoa haraka iwezekanavyo wanajeshi wake 1,000 walioko nchini humo.
Tukio hilo linawafanya wanajeshi wa Marekani na Russia kukaribiana sana na hivyo kuzidisha taharuki katika uhusiano wa kijeshi na kidiplomasia ambao umedorora kati ya nchi hizo mbili hasimu kutokana na mzozo unaoendelea nchini Ukraine.
Wanajeshi wa Marekani ambao wanatazamiwa kuondoka Niger hivi karibuni, tayari wametakiwa na serikali ya Chad kuondoka nchini humo mara moja, huku jeshi la Ufaransa likifukuzwa pia kutoka Mali na Burkina Faso katika miezi ya hivi karibuni.
Mnamo Machi, serikali ya Niger ilisema kwamba ilibatilisha makubaliano ya kijeshi na Marekani ambayo yaliruhusu wanajeshi wa Marekani kuwa kwenye ardhi yake.
 
Sidhani Kama Kuna taharuki, pamoja na uhasama wao wanajua mipaka yao ndio maana ni nadra kusikia wamekwaruzana Syria.
Yaani waziri wa ulinzi wa usa ana taharuki lakini ww upo namtumbo unasema hakuna haja ya taharuki kwa kifupi ww unajua masuala ya ulinzi na usalama kuliko waziri wa ulinzi wa usa hv unajua uturuki alinyimwa f-35 fighter jet sababu kwenye kambi zake ana mifumo ya Russia ya ulinzi wa anga USA wakahofia hyo mifumo ikikaa pamoja itasoma udhaifu wa mifumo yao na hicho ndio kikubwa wanachohofia.
 
Sidhani Kama Kuna taharuki, pamoja na uhasama wao wanajua mipaka yao ndio maana ni nadra kusikia wamekwaruzana Syria.
Jana tu huko Syria walikutana na magari yao ya kivita dereva wa Urusi akagusishia gari lake kwenye gari la kivita la marekani wakati yakikimbizana jangwani kitendo kilichopelekea gari la marekani kubiringita na kuumiza wanajeshi wake wanne
 
Jana tu huko Syria walikutana na magari yao ya kivita dereva wa Urusi akagusishia gari lake kwenye gari la kivita la marekani wakati yakikimbizana jangwani kitendo kilichopelekea gari la marekani kubiringita na kuumiza wanajeshi wake wanne
Urusi huwa wanawafanyia sana vitimbwi wanajeshi wa Marekani.

Huko syria hzo mambo zinatokea sana kuna kipindi walikuwa wanatishiwa kama kugongwa hv kama sijasahau.
 
Hao wamarekani kama hawaja ondoka
itafikia hatua
watachukuliwa hata kwenda kupika na kuosha vyombo na ilivyo michoko sasa ITAKUBALI QMMAQE
 
Back
Top Bottom