Wanaharakati wahimiza uchangiaji fedha kudhibiti, Ukimwi, Malaria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
Wanaharakati na wadau wa masuala ya kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu wametoa wito kwa serikali na wadau wengine kote duniani kutoa ahadi kwa hiari za kuchangia fedha zisizo pungua dola za Kimarekani bilioni 20 zinazohitajika katika mfuko wa Fedha wa Dunia kwa mwaka 2011 hadi 2013.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Elimu Kwa Watoto (Cheso), Richard Shilamba, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika wiki ya hitimisho la wanaharakati na wadau wengine wa masuala ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu.

Shilamba amesema kwamba endapo wafadhili na wadau wengine wataahidi na kutoa fedha hizo katika mfuko huo kutaziwezesha serikali zote duniani kufikia malengo ya Millenia.

"Kwa taarifa Mfuko wa Fedha Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria tangu kuanzishwa mwaka 2001 umekwishatoa jumla ya dola za Kimarekani bilioni19.3 na takribani nchi 144 wamenufaika na fedha hizi, Tanzania ikiwemo na fedha hizo zimeokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 4.9 na zinaokoa vifo vya watu 3600 kila siku hapa Tanzania," alisema.

Aidha, Shilamba amesema kupatikana kwa fedha hizo kutoka kwa wadau na wanaharakaiti wa magojwa hayo zitakazowekwa katika mfuko wa Fedha wa Dunia kutasaidia pia katika kukamilisha ajenda 10 za watoto ili kukamilisha malengo ya Millenia ifikapo mwaka 2015.

Alisema miongoni mwa ajenda hizo 10 za watoto ni pamoja na kuwekeza katika elimu ya awali kwa watoto, kuwekeza katika lishe bora, kuwekeza ili kuokoa maisha ya watoto, kuwekeza katika usafi kiafya na mazingira mashuleni na mahali zitolewapo huduma za afya, kuwekeza elinu bora kwa watoto wote, kuwekeza ili kuwa na shule salama, kuwekeza ili kupunguza mimba za utotoni na kuwekeza kwa watoto waishio na ulemavu.



CHANZO: NIPASHE

Umasikini nao unachangia kuwepo kwa haya maradhi na Serikali haitilii mkazo ili kuyatokomeza hayo maradhi hapa kwetu yamekuwa kama Donda kuu lisilo pona yaani Maradhi ya Ukimwi Malaria na Kifua kikuu yanauwa watu wengi sana hapo kwetu .
 
Wabongo bwana, maneno meeengiiii...... ngoja wapate hizo pesa kama utawaona au kuwasikia tena.................
 
Back
Top Bottom