Wanahabari wa Iringa kumuweka kitimoto Mbunge wa Iringa Mjini!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Na Francis Godwin-Iringa

Wakati kesho mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi kumlalamikia mbunge huyo .

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliyasema hayo leo wakati akizunguza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku hiyo ya Uhuru wa Vyombo duniani .

Alisema kuwa mdahalo huu katika ya wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini na mbunge huyo wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa utafanyika katika ukumbi wa Highlands ukumbi uliopo katikati ya mji Iringa kutoa nafasi kwa wananchi wote kufika.

Hata hivyo alisema kuwa mdahalo huo ulipangwa kuwahusisha pia wabunge wa CCM akiwemo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ambao wameonyesha kuwa na uzuru katika siku hiyo .

Alisema kuwa wakati mbunge Kabati akiomba kutofika kutokana na kuwa katika vikao jijini Dar es Salaam mbunge Filikunjombe kwa siku hiyo atakuwa nje ya nchi hivyo kufika kwao itakuwa vigumu.

Mwangosi alisema sherehe hizo za siku ya uhuru wa vyombo vya habari zitahusisha wanahabari wote bila kujali ni wanachama wa IPC ama si wanachama.

katika hatua nyingine Mwangosi alisema kuwa IPC inasikitishwa na vitendo vitisho vinavyotolewa na wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa kwa wanahabari wa vyombo mbali mbali wanaofika kusikiliza madai yao katika migomo mbali mbali.

Alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa na tabia ya kuwaita wanahabari wakati wa migomo yao na mara baada ya kufika na kuripoti wamekuwa wakiwatishia kuwavunjia vifaa vyao vya kazi kwa madai kuwa kwanini wanahabari hao wamewafuata watuhumiwa katika madai hayo na kuwahoji kinyume na wao wanavyotaka kuzungumza wao pekee.

Mwangosi alisema kuwa tayari wanahabari hao wamepata kutoa vitisho kwa mwandishi wa TBC Iringa , Chanel Ten, gazeti la Mtanania ,Habari leo , Radio Ebony Fm ,Radio Country Fm na wanahabari wengine wengi .

Hivyo amesema kuwa iwapo wanafunzi hao wataendelea na tabia hiyo wanahabari hawatakuwa tayari kwenda kuwasikiliza pale wanapohitaji uwepo wa vyombo vya habari katika mambo yao.

Kwa upande wake katibu wa IPC Frank Leonard alisema kuwa mbali ya kumweka mbunge Msigwa pia wanahabari hao watashiriki katika usafi Hospitali ya mkoa wa Iringa pamoja na shughuli nyingine za kijamii mjini Iringa .

Wananchi wengi wanamlalamikia msingwa?

Waambieni lilikuwa kosa kubwa kumchagua, na bado maana wana miaka 3 mbele, kwa hiyo watalalamika kwa miaka 3

ijayo. Wapinzani wengi ni makelele tu hawana uwezo wa kutekeleza wanapopewa nafasi za uongozi.

Waambie warudi kundini kama wanataka ahadi zinazotekelezeka.
 
Mambo ya Tanganyika yanakuwashia nini??
 
Wananchi wengi wanamlalamikia msingwa?

Waambieni lilikuwa kosa kubwa kumchagua, na bado maana wana miaka 3 mbele, kwa hiyo watalalamika kwa miaka 3

ijayo. Wapinzani wengi ni makelele tu hawana uwezo wa kutekeleza wanapopewa nafasi za uongozi.

Waambie warudi kundini kama wanataka ahadi zinazotekelezeka.

Unajitahid kweli kweli! Hivi kwa kila post moja Mwenezi wa magamba anakulipa bei gani?! au umepangiwa post ngapi kwa siku?
 
hii habari ya uwongo kabisa hizi picha zilipigwa katika maandamano wakatinpinda amekwenda Iringa. what a shame
 
Wananchi wengi wanamlalamikia msingwa?

Waambieni lilikuwa kosa kubwa kumchagua, na bado maana wana miaka 3 mbele, kwa hiyo watalalamika kwa miaka 3

ijayo. Wapinzani wengi ni makelele tu hawana uwezo wa kutekeleza wanapopewa nafasi za uongozi.

Waambie warudi kundini kama wanataka ahadi zinazotekelezeka.
kama,maisha bora kwa kila mtz,train ya umeme mza dar,ajira ml5
 
sijaelewa agenda ya kikao nini coz kichwa cha habari ni kumuweka mbunge kikao ila kilichoandikwa kwenye habari ni uadui baina ya waandishi na wanafunzi wa mkwawa.
Habari haijakaa sawa.
 
Na Francis Godwin-Iringa

Wakati kesho mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi kumlalamikia mbunge huyo .

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliyasema hayo leo wakati akizunguza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku hiyo ya Uhuru wa Vyombo duniani .

Alisema kuwa mdahalo huu katika ya wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini na mbunge huyo wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa utafanyika katika ukumbi wa Highlands ukumbi uliopo katikati ya mji Iringa kutoa nafasi kwa wananchi wote kufika.

Hata hivyo alisema kuwa mdahalo huo ulipangwa kuwahusisha pia wabunge wa CCM akiwemo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ambao wameonyesha kuwa na uzuru katika siku hiyo .

Alisema kuwa wakati mbunge Kabati akiomba kutofika kutokana na kuwa katika vikao jijini Dar es Salaam mbunge Filikunjombe kwa siku hiyo atakuwa nje ya nchi hivyo kufika kwao itakuwa vigumu.

Mwangosi alisema sherehe hizo za siku ya uhuru wa vyombo vya habari zitahusisha wanahabari wote bila kujali ni wanachama wa IPC ama si wanachama.

katika hatua nyingine Mwangosi alisema kuwa IPC inasikitishwa na vitendo vitisho vinavyotolewa na wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa kwa wanahabari wa vyombo mbali mbali wanaofika kusikiliza madai yao katika migomo mbali mbali.

Alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa na tabia ya kuwaita wanahabari wakati wa migomo yao na mara baada ya kufika na kuripoti wamekuwa wakiwatishia kuwavunjia vifaa vyao vya kazi kwa madai kuwa kwanini wanahabari hao wamewafuata watuhumiwa katika madai hayo na kuwahoji kinyume na wao wanavyotaka kuzungumza wao pekee.

Mwangosi alisema kuwa tayari wanahabari hao wamepata kutoa vitisho kwa mwandishi wa TBC Iringa , Chanel Ten, gazeti la Mtanania ,Habari leo , Radio Ebony Fm ,Radio Country Fm na wanahabari wengine wengi .

Hivyo amesema kuwa iwapo wanafunzi hao wataendelea na tabia hiyo wanahabari hawatakuwa tayari kwenda kuwasikiliza pale wanapohitaji uwepo wa vyombo vya habari katika mambo yao.

Kwa upande wake katibu wa IPC Frank Leonard alisema kuwa mbali ya kumweka mbunge Msigwa pia wanahabari hao watashiriki katika usafi Hospitali ya mkoa wa Iringa pamoja na shughuli nyingine za kijamii mjini Iringa .

Mkuu mbona heading yako haiko consistent na content uliyoiweka? Mkuu tafuta heading proper na sio hiyo. Umewatisha watu as if it is ernomous problem kati yenu na mbunge and na wananchi kwa ujumla. Umenikumbusha baadhi ya heading wana-habari huandika mfano: CCM YAIKAMATA VIBAYA CHADEMA ARUMERU,nk. Rudi upya.
 
Kiganyi, sidhani kama kuna ukweli wowote kati ya heading, content na hizo picha. Ni vitu vitatu vinavyojitegemea kabisa. Sana sana naweza kusema kuna mchezo wa kisiasa hapo juu ya mch.Msigwa
 
Wananchi wengi wanamlalamikia msingwa?

Waambieni lilikuwa kosa kubwa kumchagua, na bado maana wana miaka 3 mbele, kwa hiyo watalalamika kwa miaka 3

ijayo. Wapinzani wengi ni makelele tu hawana uwezo wa kutekeleza wanapopewa nafasi za uongozi.

Waambie warudi kundini kama wanataka ahadi zinazotekelezeka.

Fortunately, moja ya kati ya ahadi "zinazotekelezeka" ni "maisha bora kwa kila Mtanzania" ambayo kila mwananchi wa kipato cha chini- na ndio wapiga kura walio wengi- ameiona! Naomba uendelee kuikazia ahadi hiyo kuwa imetekelezeka na Chama chako kitaendelea kutawala milele.
 
labda kama hao waandishi wana maslahi ya kisiasa otherwise msigwa ni mchapakazi na kila anachofanya huwataarifu wapigakura wake kupitia mikutano ya hadhara au redio overcomers.
 
Back
Top Bottom