Wanahabari wa Iringa kumuweka kitimoto Mbunge wa Iringa Mjini!



Na Francis Godwin-Iringa

Wakati kesho mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi kumlalamikia mbunge huyo .

Hayo maneno yako na picha uliyotumia ndiyo yanaleta wasiwasi, kukutana na waandishi si tatizo ila umeongezea chumvi 'wananchi wengi wanalalamika' halafu hiyo picha ni ya kesho wakati watakapokutana naye? what is the use of it.
 

nadhani uandishi wa style hii usio na uhusiano kati ya heading na habari kusika ndiyo chanzo cha waandishi kutofautiana na hao wanafunzi wa mkwawa.
Nadhani lengo la mleta hoja ni kumchafua Mbunge wa Iringa Mjini kwa kutumia habari tofauti. Utakumbuka jana kuna mtu alipost thread inayosema Msigwa hajafanya lolote Iringa watu wakamletea picha za hospitali mpya aliyokabidhi vitanda, mleta hoja hakuonekana tena.
 
Niseme tu ukweli ni mapema sana Waandishi wa habari kuwachonganisha watu wa IRINGA na mbunge wao Msingwa kwan ni mtu makini,tatizo ninaloona hapa baadhi ya watu wa Iringa mama Mbegga aliwazoesha vibaya kuwanunulia pombe watu na sio maendeleo hivyo kuwafanya waamini Msigwa afanyi maendeleo.Mimi nilisoma Iringa pale Mwembetogwa na nikiwa katika likizo ya chuo nilienda Iringa,pamoja na mambo mengine nilipata nafasi ya kuzungumza na Mbunge Msigwa kuna mambo alikuwa anazungumza na leo ameanza kufanya.Alisema nanukuu "Naamini sana kusaidia jamii na siyo mtu mmojammoja" na siku zote anaangalia Maendeleo endelevu,Lakini Iringa ya leo sio ya mwaka 2009 wakati naanza pale Mwembetogwa kidato cha tano kwani miongoni mwa mikoa inayokuwa kwa kasi.
Ndugu zangu wana Iringa tushirikiane kikamilifu katika maendeleo kwani waandishi wetu baadhi wanatumiwa vibaya sana katika kipindi hiki cha mfumuko wa bei.

** * * * * * * * * * * * * * * * * KUWENI MAKINI MAKINI WANA IRINGA,MSIGWA AMEONGOZA MIAKA 3 MNATAKA AMALIZE MATATIZO YA MIAKA LUKUKI ILIYOPITA TUMPE MDA.AU KWA KUWA MNAJUA HATA ANAPOKAA ANGEKUWA MKUU WA MKOA KILIMANJARO TUNGESEMAJE?MAENDELEO SHIRIKISHI.Asante.
 
Ndugu wana JF msiamini hii thread kwani kwa kiwango kikubwa ina upotoshaji
1. Picha na Francis Godwin- Hii picha ni kweli ni ya wanahabari lakini ilipigwa wakati wanahabari wakiandamana takribani miezi miwili iliyopita kupinga kile walichokiita kunyanyaswa na Mkuu wa Mkoa hivyo kuitumia katika habari hii si sahihi.
2. Mtiririko wa habari si mzuri kwani heading na story haviendani.
Kwa maoni yangu muanzisha thread aseme na ban ili mchezo kama huu ukome.
 
Hii ni kazi ya mbunge wa viti maalum chadema iringa chiku abwao maana aliweka nia yake ya kumshughulikia msigwa jimboni kwa sababu alisababisha cc ya chadema imvue chiku uenyekiti wa cdm mkoa iringa.
 
offtopic kidogo jamani: sioni update yoyote kuhusu mnyika naomba aleuona Uzi wake au mwenye update anijulishe?
 


Na Francis Godwin-Iringa

Wakati kesho mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi kumlalamikia mbunge huyo .

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliyasema hayo leo wakati akizunguza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku hiyo ya Uhuru wa Vyombo duniani .

Alisema kuwa mdahalo huu katika ya wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini na mbunge huyo wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa utafanyika katika ukumbi wa Highlands ukumbi uliopo katikati ya mji Iringa kutoa nafasi kwa wananchi wote kufika.

Hata hivyo alisema kuwa mdahalo huo ulipangwa kuwahusisha pia wabunge wa CCM akiwemo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ambao wameonyesha kuwa na uzuru katika siku hiyo .

Alisema kuwa wakati mbunge Kabati akiomba kutofika kutokana na kuwa katika vikao jijini Dar es Salaam mbunge Filikunjombe kwa siku hiyo atakuwa nje ya nchi hivyo kufika kwao itakuwa vigumu.

Mwangosi alisema sherehe hizo za siku ya uhuru wa vyombo vya habari zitahusisha wanahabari wote bila kujali ni wanachama wa IPC ama si wanachama.

katika hatua nyingine Mwangosi alisema kuwa IPC inasikitishwa na vitendo vitisho vinavyotolewa na wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa kwa wanahabari wa vyombo mbali mbali wanaofika kusikiliza madai yao katika migomo mbali mbali.

Alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa na tabia ya kuwaita wanahabari wakati wa migomo yao na mara baada ya kufika na kuripoti wamekuwa wakiwatishia kuwavunjia vifaa vyao vya kazi kwa madai kuwa kwanini wanahabari hao wamewafuata watuhumiwa katika madai hayo na kuwahoji kinyume na wao wanavyotaka kuzungumza wao pekee.

Mwangosi alisema kuwa tayari wanahabari hao wamepata kutoa vitisho kwa mwandishi wa TBC Iringa , Chanel Ten, gazeti la Mtanania ,Habari leo , Radio Ebony Fm ,Radio Country Fm na wanahabari wengine wengi .

Hivyo amesema kuwa iwapo wanafunzi hao wataendelea na tabia hiyo wanahabari hawatakuwa tayari kwenda kuwasikiliza pale wanapohitaji uwepo wa vyombo vya habari katika mambo yao.

Kwa upande wake katibu wa IPC Frank Leonard alisema kuwa mbali ya kumweka mbunge Msigwa pia wanahabari hao watashiriki katika usafi Hospitali ya mkoa wa Iringa pamoja na shughuli nyingine za kijamii mjini Iringa .


unalipoti waandishi WA habari huku hujui juandika habari ! Ww moms!
 
Wananchi wengi wanamlalamikia msingwa?

Waambieni lilikuwa kosa kubwa kumchagua, na bado maana wana miaka 3 mbele, kwa hiyo watalalamika kwa miaka 3

ijayo. Wapinzani wengi ni makelele tu hawana uwezo wa kutekeleza wanapopewa nafasi za uongozi.

Waambie warudi kundini kama wanataka ahadi zinazotekelezeka.
haya mambo si ya muungano wala si ya jimbo lililo zanzibar-wewe kitu gani kinakuwasha mpaka unaingilia mambo ya iringa?iringa na Chumbuni-Zanzibar wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom