A
Anonymous
Guest
Mimi ni Afisa Afya, katika moja ya majukumu yangu ya kutoa chanjo, nimebahatika kufika katika moja ya kijiji ndani ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita, mbacho kinaitwa Kamengo.
Nilipofika hapo kiukweli inasikitisha sana Watoto hawapati huduma ya shule na clinic kwa wakati kutokana na changamoto ya mto kupitisha maji katika njia wanayopita.
Wakati wa mvua inafikia muda wanakaa wiki bila kwenda shule, hii changamoto inafahamika kwa viongozi, ila hakuna jitihada zilizofanyika kuwasaidia Wanafunzi hao.
Mimi mwenyewe nilienda kutoa huduma ya kiafya kijijini hapo, sitamani kurudi huko, je, hao Watoto watasoma kweli kwa hali kama hiyo?
Muda huo Mtoto akikosa shule anapigwa faini ya mfuko wa simenti, jamani kweli?
Mimi naomba tuwasaidie ndugu zetu hao si kwa lengo baya.