Wanafunzi UDSM wachafua hali ya hewa ujio wa JK

Mtoto Wa Mbale

JF-Expert Member
May 15, 2011
457
300
Wanafunzi UDSM wachafua hali ya hewa ujio wa JK

Source: Mwananchi Thursday, 20 October 2011

By Fidelis Butahe;

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) jana walichafua hali ya hewa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho baada ya kumzomea Rais Jakaya Kikwete.

*Rais Kikwete ambaye alikuwa ameambatana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa pamoja na viongozi wengine wa Serikali alikutwa na zomeazomea* hiyo saa 6:23 mchana wakati akiingia katika Ukumbi wa Nkrumah ambapo yalifanyika maadhimisho hayo.* Wanafunzi hao mbali na kumzomea Rais huyo wa awamu ya nne pia walikuwa wamebeba* mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba, “Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi, hatukutaki ondoka,”. *

Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yameandikwa, ‘’Wao walisoma bure sisi tunalala nje, Miaka 50 ya uhuru mikopo hatupati, Tusiilipe Dowans, Wanafundisha UDSM makazi Bagamoyo je ni haki?, Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi. *

Awali wanafunzi hao walionekana wakiwa wameshika mabango hayo lakini walizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa kama ni ujumbe tayari ulishafika hivyo waendelee na shughuli nyingine.

digg

* Hata hivyo, wanafunzi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walizunguka nyuma ya Ukumbi wa Nkrumah na kuyaficha mabango hayo, huku wengine wakijipanga tayari kwa kumpokea Rais Kikwete ambaye alikuwa bado hajafika eneo hilo.

* Mara baada ya Rais Kikwete kufika chuoni hapo alikwenda kusaini katika kitabu cha wageni na wakati akielekea katika ukumbi huo huku akipunga mkono, wanafunzi hao walikuwa kimya. *

Rais Kikwete wakati akiendelea kuwapungia mkono wanafunzi hao, walianza kumzomea na kutoa mabango yao waliyokuwa wameyaficha huku wakiimba, “Kama sio juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi”.*

Polisi waliokuwa eneo hilo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana* walilazimika kutumia busara kuwanyamazisha wanafunzi hao ambao waliendelea kuzomea na kuimba licha ya kuwa Rais Kikwete alikuwa ameshaingia katika ukumbi huo.

*Wakati shughuli za maadhimisho hayo zikiwa zinaendelea wanafunzi hao walikuwa bado wakiimba nyimbo hizo na kuzomea, mpaka walipoombwa kutoendelea kuimba na baadhi ya polisi ambao waliwaeleza kuwa kuzomea hakuwezi kuwaletea mikopo vyuoni, bali wajenge hoja za msingi na kuziwasilisha sehemu husika.

*Hata wakati Rais Kikwete akisoma hotuba yake na kugusia maendeleo ya chuo hicho pamoja na uboreshwaji wa utoaji mikopo vyuoni, wanafunzi hao waliokuwa wakifuatilia hotuba hiyo kupitia Televisheni kubwa walikuwa wakizomea. *

“Hivi Rais anajua jinsi tunavyopigika hapa chuoni, wengine inaonekana tumepewa mikopo, lakini mpaka leo hatujapata, hivi anajua tunaishi vipi huyu, anajua tunalala wapi,” walisikika wakisema baadhi ya wanafunzi.
* Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika alisema kuwa kilichofanywa na wanafunzi hao kinatakiwa kutazamwa kwa macho mawili.

*Mnyika alisema kuwa ahadi zilizotolewa na Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya chuo hicho zinatakiwa kutekelezwa na kufafanua kuwa hata katika utawala wa Mwalimu Nyerere matatizo vyuoni yalikuwapo na kwamba dawa ni kuyatatua.

* Akizungumzia kitendo cha wanafunzi hao kumzomea Rais Kikwete mbele ya Rais Museveni, Mnyika alisema kuwa hilo ni jambo la kawaida kwa kuwa Museveni amewahi kusoma katika chuo hicho na anajua harakati za wanafunzi.
* “Wakati Museveni akisoma alikuwa na kikundi chake ambacho kilikuwa na msimamo mkali na kutoa kauli za kimapinduzi kwa viongozi mbalimbali wa Afrika, Museveni anakijua hiki chuo,
 
Mimi nilishangaa alipotoa ahadi ya kundelea kutoa mikopo ili hali wafunzi wengi wamekosa mikopo na wengine wameshindwa kufika hata chuoni4
 
Back
Top Bottom